Msaada: Nilifunga ndoa ya kidini, nahitaji cheti cha ndoa cha serikali

Msaada: Nilifunga ndoa ya kidini, nahitaji cheti cha ndoa cha serikali

Wakuu msiwe wabishi cheti cha Bakwata kwa sasa hakitambuliwi serikalini.Mimi ni mtumishi nina akili timamu msidhani hapa naandika kitu nisichokijua.
Kama mtu hujui namna ya kunielekeza ni vema ukatulia tu
Hapo ktk cheti cha BAKWATA, nimekuelewa. Hata Mimi ninacho.

Unaposema hakitambuliki na Serikali ndio sikuelewi.

Mimi ni mtumishi wa Serikali. Na nakitumia mpk sasa hivi. Nimefanya kazi ktk government authority, nimekitumia kupata stahiki zote ikiwemo matibabu kupitia NHIF, wife na watoto.

Nikahama authority, nipo huku wizarani. Nakitumia kupata stahiki zangu kama kawaida. Labda utuambie ni wapi huko hakikubaliki?
 
Ukisema hivyo napata picha kwamba ndani ya serikai idara zinatofautiana.
Mimi nipo kwenye mambo ya ulinzi na usalama, huku hivyo vyeti vinasumbua.
 
Kuna vyeti vya Bakwata kama Bakwata, na kuna vyeti vya serikali
Waliooa wanajua hili, uliza mashekhe watakwambia.
Kuna mashekhe pia wanakua na vyeti vya Bakwata na serikali ila ni wachache sana pia ni vigumu kuwajua maana katika kata nzima vyeti vya serikali unaweza kukuta kapewa shekhe mmoja tu.

Kuna watu wana comment utoto hapa, sio kila jambo utalijua hata encyclopedia haijui kila kitu.
Sasa wewe kumbe unajua kuna vyeti vya BAKWATA na vya serikali. It is very simple rudi kwa sheikh akupe uwe navyo vyote viwili Cha BAKWATA kinachotambuliwa na BAKWATA na cha BAKWATA kinachotambuliwa na serikali.
 
Ukisema hivyo napata picha kwamba ndani ya serikai idara zinatofautiana.
Mimi nipo kwenye mambo ya ulinzi na usalama, huku hivyo vyeti vinasumbua.
Pole sana. Wife wangu yeye ni mtumishi pia, TAMISEMI, anakitumiana hiki hiki cha BAKWATA, hajawahi kusumbuliwa!
 
Sasa wewe kumbe unajua kuna vyeti vya BAKWATA na vya serikali. It is very simple rudi kwa sheikh akupe uwe navyo vyote viwili Cha BAKWATA kinachotambuliwa na BAKWATA na cha BAKWATA kinachotambuliwa na serikali.
Cha Bakwata ni kimoja nchi nzima, ila kuna baadhi ya mashekhe hua wanapewa vyeti vya serikali( karatasi zake ni kama vyeti vya kuzaliwa), sasa kazi ni kumjua ni shekhe gani katika kata yako anapewa hivyo vyeti maana maisha yetu watumishi ndo kama unavyojua kwenu masasi kazi uko Bukoba
 
Habari zenu wadau wenzangu.

Miaka michache iliyopita nilifunga ndoa ya kidini na nikapata cheti cha kidini(BAKWATA), kwa sasa nalazimika kupata cheti cha ndoa kutoka serikalini (kazini kinahitajika), naomba kujua utaratibu ukoje kwa mtu ambae tayari alishafunga ndoa na anahitaji cheti cha serikali na gharama zikoje?

Asanteni.
mkuu cheti ni hicho hicho tu ila kama unataka kujua kama ndoa yako imesajiliwa tayari na ritha ndiyo uende ukaulize wakuambie kama tayari na kama bado wafanye utaratibu wa kusajili
 
Habari zenu wadau wenzangu.

Miaka michache iliyopita nilifunga ndoa ya kidini na nikapata cheti cha kidini(BAKWATA), kwa sasa nalazimika kupata cheti cha ndoa kutoka serikalini (kazini kinahitajika), naomba kujua utaratibu ukoje kwa mtu ambae tayari alishafunga ndoa na anahitaji cheti cha serikali na gharama zikoje?

Asanteni.
Peleka cheti chako RITA watakupa cha serikali
 
hapana ni vile vile tu mkuu sema unatakiwa kuhakikisha kama ritha washapata taarifa zako za ndoa kama unapata usumbufu wowote
Hahahaaaaa
Kwa sasa viko tofauti kabisa, cheti cha Bakwata kina mpaka maandishi ya kiislam(arabic) cha serikali karatasi yake inafanana na cheti cha kuzaliwa(vile vyeti vya miaka ya nyuma)
 
Kwa kawaida cheti cha ndoa ni cha serikali. Ukifunga ndoa msikitini/Kanisani unapewa cheti cha ndoa cha serikali. Sasa sijui mleta mada alifungia ndoa wapi ambako hawakuwa na vyeti vya serikali...
alomfungisha ndoa ujue hajasajiliwa huyo ndoa feki hyo
 
Kiuhalisia hivi vyeti vinatakiwa kuwa na nguvu moja bila kujali kama kimetolewa serikalini, msikitini au kanisani. Hivyo alokikataa hicho cheti alitakiwa akueleze mapungufu yake na ufanye nini ili ndoa yako itambulike kazini kwako. Kama hupati maelezo ya kukidhi basi nenda kwa msajili wa ndoa ? RITA? Wakuelekeze nini cha kufanya. Pia hapo kazini kwako waulize waliokutangulia wao wamefanyaje.
Hapa sio kwamba watu wanakubishia lakini kimantiki vyeti vyote hivyo vinatakiwa kuwa na nguvu sawa kisheria. Kwa hiyo ama cheti siyo kile kinachotambuliwa au umekutana na ofisa kauzibe au kuna ubaguzi. Unaweza pia kwenda kwa mwanasheria itatoa mwanga na utatuzi. Ubarikiwe.
 
Cha Bakwata ni kimoja nchi nzima, ila kuna baadhi ya mashekhe hua wanapewa vyeti vya serikali( karatasi zake ni kama vyeti vya kuzaliwa), sasa kazi ni kumjua ni shekhe gani katika kata yako anapewa hivyo vyeti maana maisha yetu watumishi ndo kama unavyojua kwenu masasi kazi uko Bukoba
Ulizia utamjua tu huyo sheikh anayeficha vyeti vya serikali usichoke wewe.atafutaye hachoki.
 
Mimi ninacho jua mtu ukifunga ndoa unatakiwa ukaisajili RITA, mkipeana talaka pia inatakiwa ikasajiliwe RITA, mtu akifa, kifo kinatakiwa kikasajiliwe RITA. Haya mambo matatu watu wengi hawafanyi hivyo kuikosesha serikali takwimu halisi za ndoa, talaka na vifo.

Hivyo kasajili ndoa yako RITA
 
Wakuu msiwe wabishi cheti cha Bakwata kwa sasa hakitambuliwi serikalini.
Mimi ni mtumishi nina akili timamu msidhani hapa naandika kitu nisichokijua.
Kama mtu hujui namna ya kunielekeza ni vema ukatulia tu
Taratibu brother kama kweli unahitaji msaada, hili sio suala la kubishana maana ni suala la kisheria. Kikanuni ndoa hata ingefungwa popote ili mradi tu ni ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania cheti 'SHAHADA YA NDOA' au marriage certificate, kinachotambulika kiutendaji ni kile kinachotolewa na serikali ya JMT na hii ni moja kati ya HATI MAALUM za kiserikali yenye serial and registration number kama ilivyo kwa vyeti vya kuzaliwa au vya vifo, sasa wasajili wa ndoa kupitia taasisi za kidini ziwe za kiislamu, kikrsto nk yaani mashekh, maimamu, wachungaji nk kwanza ni lazima wao wenyewe waidhinishwe na serikali na kupewa kibali 'PERMIT' ya kusajili na kufunga ndoa kwa niaba ya serikali kupitia taasisi za dini zao. Hivyo basi zingatia kuwa vyeti vinavyotolewa na taasisi za kidini havina nguvu yoyote ya kasheria na havitambuliki nje ya spheres za dini zao.
USHAURI.
Kwa kuwa ni BAKWATA nenda ktk ofisi ya imam au Sheikh aliyesajili na kufunga ndoa yako, hata kama hayupo leo lakini kumbukumbu zinapaswa kuwepo kwani wakati wa kusajili ndoa kuna fomu ya kusudio inayopaswa kujazwa baina ya wanandoa watarajiwa na msajili yaani Sheikh, na fomu hii ya kusudio la kufunga ndoa nakala yake hubaki ofisini kwa msajli na original hupelekwa serikalini, ukiipata fomu ya usajili unaweza kuandikiwa shahada ama na BAKWATA wenyewe au hata serikali maana hii ni sehemu ya haki yako ya kisheria kama Raia. Zoezi lote hili gharama yake hutegemeana na mazingira ila shahada ya ndoa haizidi Tshs 20,000=.
 
Back
Top Bottom