Nyaka-One
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 4,315
- 5,986
WanaJF hasa wajuzi wa sheria ya ndoa nina jambo naomba kupata ufafanuzi.
Majuzi niliona cheti cha ndoa cha mme na mke waliofunga ndoa ya kikristo miaka kadhaa iliyopita.
Kwenye cheti niliona kuna sehemu kimeandikwa ndoa imefungwa kwa madhehebu ya kikristo lakini ile sehemu ambapo cheti kinatakiwa kufafanua kama ndoa ni ya mke mmoja, wawili au zaidi hakuna sehemu mojawapo iliyofutwa kuonyesha kwamba moja kati ya hayo machaguo matatu ndiyo inayotakiwa kubaki.
Kutokana na hali hiyo swali langu linakuja hivi:
Je, kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania (iliyotungwa na serikali) inatoa mwanya kwa mwanandoa wa kiume aliyefunga ndoa ya kikristo na kupewa cheti cha ndoa (cha serikali) kuoa zaidi ya mke mmoja hasa pale inapotokea kwamba kwenye cheti hicho kwa bahati mbaya au makusudi hakuna sehemu yoyote iliyobainisha kwamba ndoa iliyofungwa na kutajwa kwenye hicho cheti ni ya mke mmoja au wengi?