Msaada: Nilifunga ndoa ya kidini, nahitaji cheti cha ndoa cha serikali

Msaada: Nilifunga ndoa ya kidini, nahitaji cheti cha ndoa cha serikali

Habari zenu wadau wenzangu.

Miaka michache iliyopita nilifunga ndoa ya kidini na nikapata cheti cha kidini(BAKWATA), kwa sasa nalazimika kupata cheti cha ndoa kutoka serikalini (kazini kinahitajika), naomba kujua utaratibu ukoje kwa mtu ambae tayari alishafunga ndoa na anahitaji cheti cha serikali na gharama zikoje?

Asanteni
Nimepata maelekezo mazuri, nashukuru kwa ushirikiano wenu.

CLOSED,
Mkuu nakusalimu.

Ulifanikisha vipi hili swala la kupata cheti cha serikali tofauti na kile cha bakwata.

Msaada wako unahitajika nimesoma comments naona kila mtu ana wazo lako tofauti.

Asante.
 
Wakuu msiwe wabishi cheti cha Bakwata kwa sasa hakitambuliwi serikalini.
Mimi ni mtumishi nina akili timamu msidhani hapa naandika kitu nisichokijua.
Kama mtu hujui namna ya kunielekeza ni vema ukatulia tu
Uko sahihi dini zingine hutoa vyeti vya ndoa vya kidini tu Kama wanavyotoa vyeti vya ubatizo kipaimara nk. Sio kazi kubwa nenda ofisi Ya RITA ile ofisi inayoshughulika kutoa vyeti mbalimbali utapewa fomu utajaza utasajili ndoa yako kiserikali au njia nyingine nenda kaandikishe hiyo ndoa bomani muifunge kiserikali
 
Back
Top Bottom