Msaada: Nilifunga ndoa ya kidini, nahitaji cheti cha ndoa cha serikali

Msaada: Nilifunga ndoa ya kidini, nahitaji cheti cha ndoa cha serikali

Habari zenu wadau wenzangu.

Miaka michache iliyopita nilifunga ndoa ya kidini na nikapata cheti cha kidini(BAKWATA), kwa sasa nalazimika kupata cheti cha ndoa kutoka serikalini (kazini kinahitajika), naomba kujua utaratibu ukoje kwa mtu ambae tayari alishafunga ndoa na anahitaji cheti cha serikali na gharama zikoje?

Asanteni.
Utakuwa ulipewa cheti fake...Maana cheti cha Ndoa kinatolewa na serikali kinapitia tu Kanisani ama Msikitini...
 
Mkuu, nimesoma Comments zote na kutambua kuwa kuna uwalakini katika ufungishaji wa ndoa yenu.

Moja, kwa utambuzi na uhalali wa ndoa lazima cheti kitolewe na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia sehemu uliyofungisha. Misikiti na makanisa ni Mawakala tu wa Serikali katika kukamilisha zoezi hilo.

Lakini huenda wengine hatuna mwanga nao. Sasa tunaomba utuambie kama BAKWATA wana vyeti vingine vya ndoa tofauti na hivyo vinavyotolewa na Serikali. Je, cheti hicho kinatolewa na nani? Je, kinafananaje?

Hii itatusaidia na pia kuondoa sintofahamu baina ya watu hapa wanaokuwa mwanga, ambao kimsingi wapo sahihi kabisa.
 
Cheti cha ndoa ni cha serikali, dini ni wakala tu wa kufungisha ndoa, kumbuka ndoa inayokubalika kwa mujibu wa sheria za ndoa ni mke mmoja, hivyo basi kwa waislamu mke wa kwanza tu ndiyo utapewa cheti cha ndoa cha serikali. Kumbuka kuwa mawakala wote wa kufungisha ndoa vyeti wanavyo, makanisani, misikitini na pia bomani.
Hapana wadau BAKWATA nasikia wana vyeti vyao. Kuna zile ndoa za waislam unamuona binti asbh, mchana mntangaza uchumba jioni ndoa. Hapo shehe hatoi cheti cha serikali wana vyeti vyao vya kudanganyia.
 
Mkuu, nimesoma Comments zote na kutambua kuwa kuna uwalakini katika ufungishaji wa ndoa yenu.

Moja, kwa utambuzi na uhalali wa ndoa lazima cheti kitolewe na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia sehemu ulipopafungisha. Misikiti na makanisa ni Mawakala tu wa Serikali katika kukamilisha zoezi hilo.

Lakini huenda wengine hatuna mwanga nao. Sasa tunaimba utuambie kama BAKWATA wana vyeti vingine vya ndoa tofauti na hizo zinazotolewa na Serikali. Je, cheti hicho kinatolewa na nani?

Hii itatusaidia na pia kuondoa sintofahamu baina ya watu hapa wanaokuwa mwanga, ambao kimsingi wapo sahihi kabisa.
Kuna vyeti vya Bakwata kama Bakwata, na kuna vyeti vya serikali
Waliooa wanajua hili, uliza mashekhe watakwambia.
Kuna mashekhe pia wanakua na vyeti vya Bakwata na serikali ila ni wachache sana pia ni vigumu kuwajua maana katika kata nzima vyeti vya serikali unaweza kukuta kapewa shekhe mmoja tu.

Kuna watu wana comment utoto hapa, sio kila jambo utalijua hata encyclopedia haijui kila kitu.
 
Wakuu msiwe wabishi cheti cha Bakwata kwa sasa hakitambuliwi serikalini.Mimi ni mtumishi nina akili timamu msidhani hapa naandika kitu nisichokijua.
Kama mtu hujui namna ya kunielekeza ni vema ukatulia tu
Kwa uzoefu wetu cheti cha ndoa cha dini au serikali ni kile kile cha jamhuri ya Tanzania. Ila tu kuna sehemu inaonyesha kuwa ni ndoa ya kikristu, ya kiislamu au ya kiserikali. Watu hawajaelewa imekuaje umepewa cheti tofauti na wengine? Tueleweshe mkuu hatujaelewa!
Mi nashauri ungeenda ofisi ya wilaya wanapofungisha ndoa..watasolve tatizo lako!
 
Mkuu, nimesoma Comments zote na kutambua kuwa kuna uwalakini katika ufungishaji wa ndoa yenu.

Moja, kwa utambuzi na uhalali wa ndoa lazima cheti kitolewe na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia sehemu uliyofungisha. Misikiti na makanisa ni Mawakala tu wa Serikali katika kukamilisha zoezi hilo.

Lakini huenda wengine hatuna mwanga nao. Sasa tunaomba utuambie kama BAKWATA wana vyeti vingine vya ndoa tofauti na hivyo vinavyotolewa na Serikali. Je, cheti hicho kinatolewa na nani? Je, kinafananaje?

Hii itatusaidia na pia kuondoa sintofahamu baina ya watu hapa wanaokuwa mwanga, ambao kimsingi wapo sahihi kabisa.
Kama alivyosema mtoa mada nimegundua watu wengi mnacoment bila uelewa. MTU kashakwambia alipew cheti kisichotambuliwa hivi shida hapo nini nini kinawafanya msielewe?

Jf vichwa ngumu mpo wengi
Kama ungeleewa uzi wangu basi usingeandika hayo, alafu nipo serious nahitaji msaada sasa kama hili jambo hulijui just relax uendelee kusoma comments za wenzetu.
 
Cheti ulichopewa na bakwata ndio hicho peleka huko kazini maana hicho ndio cheti cha ndoa kilichoidhinishwa na serikali, kama ww ni muislam utapewa na shekh alieidhinishwa na bakwata na kama ww ni mkristo utapewa padri aliekifungisha ndoa huko kanisani na kama ulifungia bomani yaana kwenye office ya mkuu wa wilaya/mkoa au kwa kada utapewa cheti nacho ni cha serikali. Basi usihangaike kutafuta cheti wakati unacho
Cheti cha Bakwata kazini wanataka cha serikali, cha Bakwata wanapokea ila hakina nguvu katika mambo kama uhamisho na maslahi ya mtumishi.

Kama kuna yeyote alipeleka cha Bakwata wakamwambia kinatosha basi ajiandae kutafuta cheti cha serikali watamsumbua baadae
 
Kama alivyosema mtoa mada nimegundua watu wengi mnacoment bila uelewa. MTU kashakwambia alipew cheti kisichotambuliwa hivi shida hapo nini nini kinawafanya msielewe?

Jf vichwa ngumu mpo wengi
Alipewa na nani cheti kisichotambuliwa? BAKWATA hawatoi cheti kisichotambuliwa.
 
Pole sana mkuu; vyeti vya ndoa vya serikali huwa wanapewa mashehe, au wachungaji, au mapadre au maaskofu rasmi ambao wana vibali rasmi vya kufungisha ndoa. Kwa wakristo si kila anayeitwa mchungaji anakuwa na uwezo wa kufungisha ndoa bali mwenye kibali tu. Kwa waislamu unaweza kufungishwa ndoa na shehe yeyote unayependa akufungishe ila wengi wao wanakuwa hawana mamlaka kiserekali kufungisha ndoa hivyo atakupa cheti cha Bakwata tu kwa sababu dini inaruhusu hivyo.
Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kuuomba uongozi wa Bakwata ulio karibu na unapoishi ukusaidie kupata cheti cha serikali. Au nenda Bomani watakuelekeza jinsi ya kukipata.
 
Wakuu msiwe wabishi cheti cha Bakwata kwa sasa hakitambuliwi serikalini.Mimi ni mtumishi nina akili timamu msidhani hapa naandika kitu nisichokijua.
Kama mtu hujui namna ya kunielekeza ni vema ukatulia tu
Labda hiyo siku uliooa walikupa fake, mimi pia nimefunga ndoa hiyo na nimepewa cheti na bakwata chenye muhuli wa serekali ya Kijiji pia. Hakuna cheti cha ndoa kisichoitambua uwepo wa serekali.
 
Hapana wadau BAKWATA nasikia wana vyeti vyao. Kuna zile ndoa za waislam unamuona binti asbh, mchana mntangaza uchumba jioni ndoa. Hapo shehe hatoi cheti cha serikali wana vyeti vyao vya kudanganyia.
Kama alipewa cheti cha kudanganyia hapo sawa.
 
Wakuu msiwe wabishi cheti cha Bakwata kwa sasa hakitambuliwi serikalini.Mimi ni mtumishi nina akili timamu msidhani hapa naandika kitu nisichokijua.
Kama mtu hujui namna ya kunielekeza ni vema ukatulia tu
Inawezekana siko sahihi kwa mujibu wa ndoa yako uliyofunga, lakini ukweli ni kwamba kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 si kila MTU ana mamlaka ya kufungisha hadi pale atakapokuwa na leseni ya kufungisha ndoa ambayo inatolewa na msajili mkuu wa ndoa. Inawezekana aliyekufuñgisha ndoa hana leseni hiyo hivyo kutokuwa na kitabu cha vyeti vya ndoa ambacho kinaambatana na hiyo leseni.
 
Labda hiyo siku uliooa walikupa fake, mimi pia nimefunga ndoa hiyo na nimepewa cheti na bakwata chenye muhuli wa serekali ya Kijiji pia. Hakuna cheti cha ndoa kisichoitambua uwepo wa serekali.
Kama wewe ni mtumishi wa serikali jiandae kutafuta cheti cha serikali.
Hicho cha Bakwata ninacho na kina kila mihuri unayotaja wewe.
Kama hutanielewa time will tell
 
Tatizo la binadamu ni kutaka kuonekana anajua kila jambo
Endelea na kazi utafute ugali wa familia, hili nililouliza wewe hulijui ndio maana unajibu kujifurahisha
Baana e usituchoshe hapa.maswali unayoulizwa hutaki kujibu umebaki ooh mnajifanya mnajua.kama hutaki tukusaidie funga mjadala nenda huko RITA wakakusikilize.
 
Baana e usituchoshe hapa.maswali unayoulizwa hutaki kujibu umebaki ooh mnajifanya mnajua.kama hutaki tukusaidie funga mjadala nenda huko RITA wakakusikilize.
Hakuna unachojua katika hili, unajichosha mwenyewe kutaka kucomment kila jambo hata usilolijua
 
Back
Top Bottom