Nahitaji kusoma uhasibu, nina cheti cha Kidato cha Nne cha Sita na degree nyingine isiyohusiana na masuala ya kifedha

micind

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
342
867
Habari zenu,

Nahitaji kusoma hii fani ya uhasibu, nina cheti cha kidato cha nne cha sita na degree nyingine haihusiani kabisa n maswala ya kifedha.

Nimejaribu kutafuta taarifa kidogo nimekutana na ACCA, NBAA na wale wenye degree za accountancy kutoka kwenye vyuo vikuu vya hapa nyumbani.

Sasa swali langu nauliza je nahitaji kusoma Tena degree ya uhasibu Kisha niendelee huko mbele kwenye CPA na kwingine?

Nikisoma courses za ACCA tu na baadae nikafanya CPA(T) inatosha Mimi kua muhasibu au ni lazima niwe na degree ya uhasibu kwanza?

Naombeni msaada wenu kwa maswali yangu na pia kama Kuna suggestion zingine nipo tayari kuzipokea kwasababu hapa JF Kuna utajiri wa maaarifa.

Asanteni.
 
Kama hutaki kusoma Bachelor degree ya Accounting au Finance, itabidi uanze na ATEC1 chini ya NBAA hadi ufike CPA.
 
Kama hutaki kusoma Bachelor degree ya Accounting au Finance, itabidi uanze na ATEC1 chini ya NBAA hadi ufike CPA.
Siku hizi hakuna ATEC1. Kuna CPA level I mpaka VI. Kama umesoma digrii nyingine. Nenda vyuo kama Uhasibu kurasini au CBE au uliza pale pale NBAA wapi wanafundisha masomo ya jioni.

Ukiwapata utaanza kusoma CPA level 1. Utaendendelea hivyo mpaka CPA levei VI. Hapa utakuwa umekamilisha CPA yako.

Waliosoma digrii ya uhasibu wanaanza moja kwa moja na level V.

Ujue kuwa hizo level ni kama mchakamchaka wa kusoma digrii tu.
 
Mi siwez aisee
Mimi mahesabu yangu yanapokuja kuvurugika ni pale kwenye kipato unakuta dogo janja tu anasumbua mtaani na hajasoma wala nini kina joni kisomo wanasugua kuamka saa kumi na moja kutoka saa kumi na moja sio mchezo
 
😂😂😂kutoboa maisha siyo Elimu mkuu...watu na degree zao wapo wanapaa na mikokoteni uyole hapa...waliowaacha la saba wanaenda kuchukua mizigo Dubai
 
Siku hizi hakuna ATEC1. Kuna CPA level I mpaka VI. Kama umesoma digrii nyingine. Nenda vyuo kama Uhasibu kurasini au CBE au uliza pale pale NBAA wapi wanafundisha masomo ya jioni. Ukiwapata utaanza kusoma CPA level 1. Utaendendelea hivyo mpaka CPA levei VI. Hapa utakuwa umekamilisha CPA yako.
Waliosoma digrii ya uhasibu wanaanza moja kwa moja na level V.
Ujue kuwa hizo level ni kama mchakamchaka wa kusoma digrii tu.
Okay Asante mkuu nimekuelewa
 
Kama hutaki kusoma Bachelor degree ya Accounting au Finance, itabidi uanze na ATEC1 chini ya NBAA hadi ufike CPA.
Okay asante, sio kwamba sitaki kusoma degree ya accounting au finance, naweza kusoma Kama ikiwa ndio option nzuri zaidi, ndio maana nimeomba mawazo ya wadau wa hii sekta mkuu, yote yanawezekana
 
Siku hizi hakuna ATEC1. Kuna CPA level I mpaka VI. Kama umesoma digrii nyingine. Nenda vyuo kama Uhasibu kurasini au CBE au uliza pale pale NBAA wapi wanafundisha masomo ya jioni.

Ukiwapata utaanza kusoma CPA level 1. Utaendendelea hivyo mpaka CPA levei VI. Hapa utakuwa umekamilisha CPA yako.

Waliosoma digrii ya uhasibu wanaanza moja kwa moja na level V.

Ujue kuwa hizo level ni kama mchakamchaka wa kusoma digrii tu.
Vipi ukiwa na Bachelor degree ya Tax, si unaweza kuanza na CPA level V pia?!

Maana ninachokijua Uhasibu na Kodi ni ndugu wasiofanana ila wanatoka shina moja...
 
Kama una degree nyingine tofaui na ya uhasibu basi utaanza Foundation level, hapo utafanya mitihani ya masomo sita.

Ukitoboa hapo utaendelea na

Intermediate level, hapo napo utafanya mitihani ya masomo sita.

Ukitoboa hapo utaendelea tena kwenye

Final level ambapo utafanya masomo manne.

Ukiwa vizuri haswa, ndani ya mwaka mmoja na nusu tu ushaikamata CPA yako mkononi.

Kila la kheri.
 
Back
Top Bottom