Msaada: Naomba kukopeshwa hela nimpeleke mtoto shule

Msaada: Naomba kukopeshwa hela nimpeleke mtoto shule

Wente matatizo ya namna hii wapo wengi kipindi hiki. Sasa kwa mfano ikipatikana iyo laki 7 yakumpeleka shule mwaka huu vip miaka itakayofata?
 
>>>>Pole mama..... Msaada ninaoweza ni kukupatia shule ambayo wanaweza kumpokea na kukuvumilia hadi mwezi wa tatu ama wa nne..


>>>>Kama ukikubali huo msaada niPM tuone tunafanyaje.........
 
Picha inaonesha mtoto ni wa kike... Alafu jina anaitwa Alex m. Mwasile? Huyo mtoto ni mJapana au?

Tuseme labda hiyo account ni ya kwako... wewe ni mme au mmke? Sijakuelewa?
Nilivyomuelewa mimi, A/C ya shule ndo ina jina hilo.
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] lkn co yakucheka
 
Kashindwa kusoma form2 shule ya kata, kwani amefukuzwa?

Na y unaema ni mwaka huu umrguwa mgumu, kabla ulilipaje?

Nauliza sababu sijakuelewa.
 
Utapeli ni kipaji. Sasa huyu sio tapeli Bali anajifunza utapeli lakini kachemka Mapema kabisa. Pole sana Miss Alex. Hii ndio Jf so next ukija jipange sawasawa. Yaani post ya kwanza tu hapa unaomba msaada.
 
Hapa kuna mengi sana nimjifunza kupitia Uzi wa mwana JF mwenzetu.....na nikiwa mdau wa elimu nina hakika ya haya:

1. Kuna uwezekano mkubwa kuwa huyu mzazi ana mtoto anayetakiwa kuingia kidato cha Tatu, (nimesoma jinsi anavyo-sound)

2. Hana uwezo wa kumlipia ada kwa mihula iliyobaki ya kidato cha Tatu na cha NNE

3. Ana uwezo wa kawaida tu wa kumlisha, kumvisha mwanaye, anapenda amwendeleze zaidi kielimu maana yeye hakufanikiwa sana kielimu (ingawa naona alionyesha juhudi kwa kusoma secretarial course) na naona hataki mwanaye aishie njiani.

4. Kuna udhaifu mkubwa sana katika idara ukaguzi wa shule zetu, mfano, shule tajwa hapo inawapa wazazi account ya mmliki wa shule, badala ya account iliyosajiliwa ya taasisi.

5. Udhaifu mwingine ni pale ambapo shule inasomeka kuwa INA usajili wa kidato cha tano na cha sita lakini mkuu wa shule kumbe anapokea watoto hadi wa o level (au shule haija-update taarifa zake ?)

6. Nimejifunza pia wadau wengi hapa wana nia ya dhati ya kumsaidia mzazi lakini wameingiwa na woga baada ya "makosa, mapungufu" katika Maelezo ya mzazi, mfano jina Alex, ambalo sio la mtoto Bali la mmliki wa shule, imeonekana picha ni ya binti lakini jina la account ni Alex, kumbe Alex ni mmliki wa shule.

Cha kumsaidia mzazi, kwanza asikate tamaa, (nimehisi anakatishwa tamaa na wanaohisi ni tapeli) siku hizi hatuaminiani hasa huku mtandaoni. Pili apate nyaraka kutoka shuleni ikiwamo acc ya shule sio ya mkuu wa shule, barua au joining instruction yenye mihuri ya shule, barua ya kiongozi wa mtaa au kijiji yenye muhuri ikimtambulisha mtoto na mzazi.

Asante, haya ni maoni tu kutoka kwangu, hasa nikilinganisha na wazazi wengine wanavyohangaika katika haya maeneo ninayoishi.
 
January imeanza sasa,bado wa kodi za nyumba nao kujitokeza.ila yote kwa yote kuna uwezekano Jf ikatumika kusaidia matapeli
 
Ukiona mtu ambaye humfahamu anataka kukukopa pesa ambazo hata huko mitaani anaweza kuzipata, uwe na shaka. Ama kawaliza watu kwa mikopo au ni tapeli.
 
Huyu huyu Mwasile muuza gas hapa kwetu MAUKI dark city? Jamani huu si wizi huu? Kwanza mama hapa Morogoro uko mtaa gain? Hebu tulioko Morogoro atutajie mtaa tukamwone na atupe vielelezo vya mtoto kama ameshindwa kuviweka hapa! Matapeli wamekuwa wengi mno!
 
Picha inaonesha mtoto ni wa kike... Alafu jina anaitwa Alex m. Mwasile? Huyo mtoto ni mJapana au?

Tuseme labda hiyo account ni ya kwako... wewe ni mme au mmke? Sijakuelewa?
[emoji15] [emoji15] ...ujapani tena..[emoji15] [emoji15] ...!!!!!....
 
Back
Top Bottom