Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,500
Jamani wanaJF, kuna rafiki yangu mmoja jana usiku kanieleza jambo nikaona niwaletee humu tujaribu kumsaidia. Huyu bwana ameniambia kuwa amejishangaa jana amekuta katika chupi yake kuna damu na inaonekana imevija toka ndani ya uume wake bila yeye kujua. amesema hali hiyo ilimstua sana na hajui sababu ni nini. Nimemuuliza kama ameshawahi kuugua ugonjwa wa zinaa akasema haijawahi kutokea kupata ugonjwa wowote. Nikamuuliza kama kakutana na msichana hivi karibuni akasema ana zaidi ya miezi miwili. Kwakweli nimeshindwa kujua nini kimempata huyu bwana nikaona kwakuwa JF ni Home of Great Thinkers, huenda kuna watu wenye taaluma ya afya wanaweza kusaidia kueleza kitaalamu hii inasababishwa na nini. Please hebu saidieni katika hili nini inaweza kuwa sababu.