Msaada hichi kidonda sehemu ya siri nitumie dawa gani?

Decoration

Member
Oct 27, 2018
63
88
Mficha maradhi kifo humuumbua nimeweka na picha

Kilianza miezi 3 iliyopita kama kipele tu sasa hivi ndo kama unavyokiona

Hakiponi kabisa nilijitahidi kukanda na maji moto na chumvi lakini wapi

Kinakaa kinavimbia utadhan usaha kumbe kinavimbia damu tu

Nakosa hata raha ya kuwaza kushiriki tendo la ndoa
Kinakua kinavimbia damu tu kila mara na inakua hivyo bila kupona nisaidieni nitumie dawa gani kikauke na kipone?Nilikua natumia hair removal kushave nywele nimeacha kwa maana ilikua ikinichubua huko mpaka sasa nahofia kufanya hivyo maana ninahofia kitachubuka zaidi
Screenshot_20210821-041903.png



Mrejesho:Nilichelewa kuja kutoa mrejesho humu ndani kuhusu kidonda changu Lakini baada ya kutoka hapa niliuchukua ushauri nikaenda hospital ambapo kwa bahati mbaya niliambiwa Bima yangu haijawa activated hivyo nikakosa huduma..

Halaf hichi kidonda hakikuwa na association yoyote au uhusiano na history yangu ya kuugua kabisa maana kuna watu walikua wanafukua thread zangu sijawah kuugua magonjwa ya zinaa kabisa maishani mwangu na wala sio mtu wa kujiachia sana, ni muangalifu sana nina mpenzi mmoja tu mwaka wa 8 huu

Nikamcheki dr mmoja nguli mwenye hospital yake kupitia watsaap nikamuelezea akanambia niende matibabu yake ni elfu 75 kwa kuanzia..Nikaona ngoja nisubiri kwanza

Nilishauriwa niende duka la dawa pia lakini wakati nikiwa kwenye kuwaza nichague chaguo lipi maana kilikua kimevimbia damu, nikasoma kitabu kimoja hivi ambacho nilikua nacho cha anti bacteria and anti viral herbals ambacho nilikua nimekinunua nikawa nimekipuuza tu muda mrefu kujisomea ndo nikakuta kwamba aloevera na kitunguu swaumu kwa pamoja vinakausha vidonda na ni antiviral na antibacterial pia...

Nikatafuta aloevera maana nimepanda nyumbani, nikaikata ule utomvu wake nikaukamua nikakoroga pamoja na kitunguu swaumu kilichosagwa nikapaka then nikapafunga na bandeji ili hiyo dawa isitoke nikafanya hivyo kwa kuweka aloevera na kitunguu swaumu asubuhi na jioni

You can't believe kidonda kimekauka ndani ya siku 2 tu
Baada ya kukauka nikawa naendelea kupaka kama siku 7 hivi kimepona kabisa uvimbe umekwisha yaani ukiambiwa nilikuaga na kidonda kikubwa hapo mahali huwezi amini panavyoonekana utadhani hapajawahi kuwa na uvimbe na kidonda..
 
Mimi naona kama ni kipele kilichotokana na unyoaji mbaya wa nywele za chini. Hapo utakuta unywele umejiviringa ndani humo kwenye ngozi basi ni shida tuupu. Ila hiyo dawa uliyomshauri itamsaidia.
Ni mchubuko tu huo wa kawaida.. Sema kwa nature ya ngozi ya sehem za siri huwa inakuwa na layer ya mafuta ndo maana kidonda kinachelewa kupona.

Pia anahisi kina usaha, kiuhalisa hakuna usaha ila ni ngozi ya ndani nyeupe ambayo ni layer ya fat(mafuta)

Cha msingi ahakikishe anapunguza mazingira ya unyevu nyevu sehem hizo na kuepuka kuvaa nguo za kubana
 
Hapo tatizo limesababishwa na kutokunyoa na kujifanyia usafi.
1. Nyoa nywele zote huko chini
2. Jioshe vizuri na hakikisha unakuwa mkavu
3. Pakaa antibacterial ambayo utaipata pharmacy
4. Hakikisha hauvai nguo za kubana


Ukifanya hayo siku 3 ni nyingi utakuwa umepona na uje kutupa mrejesho
 
Mficha maradhi kifo humuumbua nimeweka na picha

Kilianza miezi 3 iliyopita kama kipele tu sasa hivi ndo kama unavyokiona

Hakiponi kabisa nilijitahidi kukanda na maji moto na chumvi lakini wapi

Kinakaa kinavimbia utadhan usaha kumbe kinavimbia damu tu

Nakosa hata raha ya kuwaza kushiriki tendo la ndoa
Kinakua kinavimbia damu tu kila mara na inakua hivyo bila kupona nisaidieni nitumie dawa gani kikauke na kipone?Nilikua natumia hair removal kushave nywele huko mpaka sasa nahofia kufanya hivyo maana ninahofia kitachubuka zaidi

Samahanini kwa hizi picha
View attachment 1900225View attachment 1900226View attachment 1900227View attachment 1900228View attachment 1900231View attachment 1900229View attachment 1900230
Kuna dawa ya kupaka inaitwa DEZOR inauzwa elfu 15 nadhani, ni nzuri,ungekunywa na vidonge vya antbiotics au sindano zile za p,serf
 
Back
Top Bottom