Msaada kutokomeza wezi?

Msaada kutokomeza wezi?

Huu wizi umerudi kwa kasi, last week walibeba nchi 70 kwangu nakurupuka kuuliza uliza na jirani yangu nae kapigwa usiku huo huo. Sijui wanatumia dawa gani washenzi hawa.
Nusu kaputi
 
Madirisha yote unganisha na Umeme
Pia jitahidi kufuga mbwa ili awe anakuamsha
Madirisha ukiunganisha na Umeme uwe na kumbukumbu maana wtoto wetu tunawajua walivyo
Pia pole sana

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
Very risk kuweka umeme unaweza dhuru watu usiolenga wadhirike.

Mbwa anawekewa sumu tu siku hizi na anakatika before haujaamshwa. Wewe unapigwa hewa ya kuchosha mwili inakulaza kabisa fofofo unaamka saa 6 hoi wanafagia kila kitu.
 
Huu wizi umerudi kwa kasi, last week walibeba nchi 70 kwangu nakurupuka kuuliza uliza na jirani yangu nae kapigwa usiku huo huo. Sijui wanatumia dawa gani washenzi hawa.
Inasemekana wanachanganya changanya wenyewe, wengine wanatumia klorofomu, ilimradi tu.

Ubaya ni kwamba, waki-overdose, unapitiliza!

Ila ndo wizi wa haya maTV umepamba moto, kijijini hapa wameshatembea TV mbili wiki iliyoisha!
 
CCTV camera hazisaidii sana maana wezi wanajiandaa na kuficha sura zao. Hata electric fence kuna namna watu wanapita bila kuzigusa.
Mbwa wanasaidia sana ingawa nao wanaweza kupigwa sumu dk 5 tu chali. Mie niliibiwa gari nina mbwa, camera, electric fence, ukuta kozi 11, geti la umeme na alarm ila wajinga walifanya yao na mbwa wote wanne walikufa kwa sumu.

Wezi wakipania hawakukosi
Pole Sana Mkuu Kama upo na Bastola muhimu na kuweka mlinzi hata Masai aisee pole sana
 
CCTV camera hazisaidii sana maana wezi wanajiandaa na kuficha sura zao. Hata electric fence kuna namna watu wanapita bila kuzigusa.
Mbwa wanasaidia sana ingawa nao wanaweza kupigwa sumu dk 5 tu chali. Mie niliibiwa gari nina mbwa, camera, electric fence, ukuta kozi 11, geti la umeme na alarm ila wajinga walifanya yao na mbwa wote wanne walikufa kwa sumu.

Wezi wakipania hawakukosi
Kunyanyinya. Hao majizi wamekula kisomo kisawa sawa wakaelemika.
 
Back
Top Bottom