Msaada jinsi ya kublock hizi meseji za bahati nasibu za haya makampuni ya mawasiliano ya simu

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,733
2,083
Habarini wanajamvi.

Sijui humu ndani kama kuna mtu amewahi kushinda ama kupata hiyo bahati ya kushinda hela au magari wanayotangaza.Na sijui dhamira yao ni nini.Zimekuwa 'too much' Nani kawaambia kuwa si tunataka hizo bahati nasibu zao.

Hebu tusaidiane jinsi ya kuwablock hawa watu.Vitu vingine havina msingi kabisa ni kujaza simu tu.Yaani wanatufanya kama watoto hivi mtu upewe mamilioni au gari la bure hivi hivi tu.

Haiingii akilini hata kidogo.Waache hiyo tabia watafute namna nyingine ya watu kushiriki hizo bahati nasibu zao.
 
Block namba moja moja,wakituma tu ujumbe nenda setting ya sms kwa Android Mara nyingi ipo kwenye Dot's tatu zilizopo upande wa kulia juu ya screen yako
 
Airtel jana wamenitesa sana, wenitumia meseji kama 100 hivi za bahati nasibu. Halafu zote wanatumia na ya Airtel money, hivyo unaweza kuhisi umepokea pesa..
 
Habarini wanajamvi.
Sijui humu ndani kama kuna mtu amewahi kushinda ama kupata hiyo bahati ya kushinda hela au magari wanayotangaza.Na sijui dhamira yao ni nini.Zimekuwa 'too much' Nani kawaambia kuwa si tunataka hizo bahati nasibu zao.
Hebu tusaidiane jinsi ya kuwablock hawa watu.Vitu vingine havina msingi kabisa ni kujaza simu tu.Yaani wanatufanya kama watoto hivi mtu upewe mamilioni au gari la bure hivi hivi tu.
Haiingii akilini hata kidogo.Waache hiyo tabia watafute namna nyingine ya watu kushiriki hizo bahati nasibu zao.
Mkuu wapigie simu tu na uwaondoe katika mailing list yao.
Mimi nimefanya hivyo kwa vodacom na Tusuamapene yao. Sasa sipati tena.
 
Kama unatumia smartphone simple tu.
Nenda kwenye notifications juu slide kioo chini kisha bonyeza sms au notification unayoipenda kwa sekunde kama tano then changua option ya kublock
 
Habarini wanajamvi.
Sijui humu ndani kama kuna mtu amewahi kushinda ama kupata hiyo bahati ya kushinda hela au magari wanayotangaza.Na sijui dhamira yao ni nini.Zimekuwa 'too much' Nani kawaambia kuwa si tunataka hizo bahati nasibu zao.
Hebu tusaidiane jinsi ya kuwablock hawa watu.Vitu vingine havina msingi kabisa ni kujaza simu tu.Yaani wanatufanya kama watoto hivi mtu upewe mamilioni au gari la bure hivi hivi tu.
Haiingii akilini hata kidogo.Waache hiyo tabia watafute namna nyingine ya watu kushiriki hizo bahati nasibu zao.
Jamaa wamezidi aisee
 
Waweke option ya kuchagua kushiriki au kutoshiriki.Na sio kuvurumisha tu mameseji yanaingia kama kuna kitu cha msingi kumbe hamna.
 
Niliwapigia halotel wakanambia siyo kila meseji ya kuzuiwa nyingine nivumilie tu maana akizuia huenda nisiweze hata kupata hiduma ya sms... nikanywea!

Voda niliwapigia wakatoa

Tigo nilipiga wakaondoa japo bado matoleo mapya ya sms kila siku

TTCL hawanaga naona hizoishu japo matapeli wengi wana TTCL

Zantel nilipiga wakatoa (tena hawa walitoa kwelikweli maana hakuingii meseji yoyote ya kipuuzi- hata utapeli Zantel inaonekana wako vizuri kudhibiti siyo kama hawa wengine kila siku utapeli)

Suluhisho la pili ni kuwapigia simu huduma kwa wateja (maana kublock kwa wengine ni vigumu kidogo)
 
Inachezwaje hiyo.
Ukifanya muamala wowote wa Airtel money unaingizwa moja Kwa moja kwenye bahati nasibu Yao ambayo Kila siku mahindi mmoja anapata 1m.

Huwezi jua unaweza shinda na wewe.

Anyway Mimi ni mshiriki mmoja wapo ambaye nipo kwenye uchezeshaji wa hiyo bahati nasibu
View attachment 2273473inachezwaje tupe mwanga kidogo.
 
Mie voda jamani, line yao sijaaweka vocha ina zaidi ya mwaka sasa ila kila wakati wananitumia sms ya kifurushi changu kuisha sasa sijui kifurushi gani
 
Back
Top Bottom