Mitandao ya mawasiliano ya simu mnapopunguza dakika vifurushi vyenu toeni taarifa pia

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,726
2,082
Salaam humu.

Kuna jamaa amekuja kwangu nimuungie kifurushi kwenye mtandao mmoja pendwa nikajifanya kama mjuaji sana na madoido yangu nikamuungia akaondoka zake.

Baada ya dakika tano karudi analalamika nimemuungia kifurushi siyo chenyewe kuja kuangalia kweli dakika zimepungua nikatoa macho nikasema ngoja nijaribu kuona nikarudia kama naunga ngoma iko palepale nikasema hapa nimeumbuka kumbe kampuni imeshafanya yake wameshaminya dakika kimyakimya.

Ikabidi nimueleweshe kuwa jamaa wamepunguza dakika za kifurushi huwezi kupata kama mwanzo nikamwambia naona makampuni ya simu nao wameamua kufidia gharama za kupanda sukari maana sasa hivi kila kitu kinapanda bei.

Kinachoboa haya makampuni ni hizi meseji zao za matangazo yao kila siku na kila dakika meseji zinajirudia hizo hizo tu kila siku lkn hizi za muhimu za kupunguza vifurushi hawatumi wanauchuna kimya sijui wanaogopa nini.

Kwa nini wasiseme tu jamani waungwana tumepunguza dakika za baadhi ya vifurushi vyetu tunafidia na sisi bei ya kupanda sukari na mafuta ya kula na mafuta ya magari yetu.

 Sisi mbona
tutawaelewa tu.

Haya kazi kwenu watanganyika bado kitu gani kingine muhimu hakijapanda bei ...🙁
.
 
Mimi nasikitika jinsi wanavyokata muda wa maongezi bila sababu na wanakata pesa nyingi mnoo! Voda wamenikata elfu 5 nzimaa sijui kwanini tigo wamekata elfu 1 huduma ya kuongea na mhudumu wameondoa najibiwa na computer pre-recorded msg baasi!

Kama kuna anayeweza kunielekeza wanakoshitakiwa hawa wenye mitandao naomba msaada tafadhali.
 
Tafuta wanasheria mjaribu kuangalia.Wanafanya vitu kienyeji sana.
 
Back
Top Bottom