Unyanyasaji kwenye mtandao na jinsi ya kuukomesha

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553

1. Unyanyasaji wa kimtandao ni nini?​

Unyanyasi wa kimtandao ni uonevu unaotendeka kwa kutumia teknolojia za kidijitali. Mtu anaweza kufanyiwa kwenye mitandao ya kijamii, majukwaa ya kutuma ujumbe, majukwaa ya michezo ya kubahatisha na hata kwenye simu za mkononi.

Uonevu huu huwa na tabia ya kujirudia lengo likiwa ni kutisha, kukasirisha au kuwaaibisha wale wanaolengwa.

Mifano ya matendo ya uonevu wa mtandaoni ni pamoja na kueneza uwongo, kutuma picha au video za aibu za mtu fulani kwenye mitandao ya kijamii, kutuma ujumbe, picha au video za kuumiza, matusi au vitisho kupitia mifumo ya ujumbe, kuiga mtu mwingine na kutuma ujumbe mbaya kwa wengine kwa niaba yao au kupitia akaunti za kughushi.

Uonevu wa ana kwa ana na ule wa mtandao mara nyingi unaweza kutokea pamoja. Lakini uonevu mtandaoni huacha alama za kidijitali , na hizi kuweza kutumika kama rekodi muhimu ya kutoa ushahidi wa kusaidia kukomesha uonevu huo.

Kuna unyanyasaji wa kielekroniki unaofanywa dhidi ya watoto.

Khaled Abd El Wahab

Kuna unyanyasaji wa kielekroniki unaofanywa dhidi ya watoto.

2. Je, unawezaje kutofautisha mzaha na uonevu mtandaoni?​

Marafiki wote hutaniana wao kwa wao, lakini wakati mwingine ni vigumu kujua ikiwa mtu anafurahia utani huo au unamuumiza. Wakati mwingine mtu anaweza kukuumiza nafsi na kuishia kucheka kwakusema “natania tu,” au “usiichukulie kwa uzito sana.”

Lakini ikiwa unahisi kuumia au kufikiria wengine wanakucheka, basi mzaha huo umekwenda mbali sana na nivyema kumwambia anayefanya hivyo aache mara moja. Ikiwa ataendelea hata baada ya kumwomba, basi huu unaweza kuwa uonevu.

Na hali huwa mbaya zaidi inapofanyika mtandaoni kwasababu watu wengi wanaona wakiwemo wageni.
Chakuzingatia ni ikiwa huna furaha kuhusu jambo hilo, hupaswi kukaa kimya. Na ikiwa unajisikia vibaya ni vyema kupata msaada.

Kukomesha uonegvu wa mtandao sio tu kuwataja wakorofi, bali pia ni kutambua kwamba kila mtu anastahili heshima mtandaoni na katika maisha halisi.

3. Yapi ni madhara ya uonevu mtandaoni?​

Madhara yanaweza kudumu kwa muda mrefu na kuathiri mtu kwa njia nyingi:-
Kiakili - kujisikia hasira, aibu, mjinga, hofu au hasira
Kihisia - kujisikia aibu au kupoteza hari ya kufanya mambo unayopenda
Kimwili - uchovu (kukosa usingizi), au kupata dalili kama vile maumivu ya tumbo na maumivu ya kichwa.

Hisia ya kuchekwa au kunyanyaswa na wengine, inaweza kuzuia watu kuzungumza au kujaribu kushughulikia tatizo linalowakabiili. Katika hali mbaya zaidi, uonevu wa mtandao unaweza hata kusababisha watu kujiua.
Uonevu mbali na kuleta athari nyingi lakini aliyefanyiwa vitendo hivyo anaweza kushinda hisia mbaya
na kurejesha imani na afya yake.

Nchini Ufaransa, hatari ya utoro ni mara tatu zaidi kati ya waathiriwa wa unyanyasaji wa mtandao.

Photo by Anthony Tran on Unsplash

Nchini Ufaransa, hatari ya utoro ni mara tatu zaidi kati ya waathiriwa wa unyanyasaji wa mtandao.

4. Nizungumze na nani iwapo nimefanyiwa uonevu mtandaoni?​

Ni muhimu sana kutoa ripoti iwapo umefanyiwa uonevu mtandaoni.

Hatua ya kwanza ni kutafuta msaada kutoka kwa mtu unayemuamini kama vile wazazi wako, rafiki yako, mwanafamilia au mtu mzima mwingine unayemuamini.

Ikiwa ni shuleni unaweza kuwasiliana na mshauri, mkufunzi wa michezo au mwalimu unayempenda, na unaweza kufanya hivi kwa njia ya mtandao au ana kwa ana.

Na ikiwa huna raha kuzungumza na mtu unayemjua, tafuta simu ya usaidizi katika nchi yako ili kuzungumza na mshauri wa kitaalamu.

Ikiwa uonevu unafanyika kwenye mtandao wa kijamii, zingatia kumzuia mnyanyasaji na kuripoti rasmi tabia zao kwenye mtandao huo. Makampuni ya mitandao ya kijamii yana wajibu wa kuwaweka watumiaji wao salama.

5. Kusanya ushahidi wa uonevu​

Ili kukomesha uonevu ukome, inahitaji kutambuliwa na kuripotiwa.

Kusanya na hifadhi ushahidi, iwe ni ujumbe mfupi au picha za simu , upige picha “ screenshot” ili kuonesha kile ambacho kimekuwa kikiendelea.

Ili uonevu ukome, inahitaji kutambuliwa na kuripoti ni muhimu. Inaweza pia kusaidia kuonyesha mnyanyasaji kwamba tabia yake haikubaliki.

Ikiwa uko katika hatari na unahitaji jambo hilo kutatuliwa kwa dharura basi unapaswa kuwasiliana na polisi au huduma za dharura katika nchi yako.

Programu ya Facebook inaoneshwa kwenye simu mahiri.

Unsplash/Solen Feyissa

Programu ya Facebook inaoneshwa kwenye simu mahiri.

6. Jinsi ya kumsaidia rafiki aliye onewa mtandaoni​

Mtu yeyote anaweza kuwasilisha taarifa za unyanyasaji wa mtandaoni. Ukiona mtu anatendewa vitendo viovu na unamfahamu jaribu kutoa usaidizi.

Ni muhimu kumsikiliza rafiki yako au mtu huyo kwanini anaogopa kwenda kutoa taarifa na kuonewa mtandaoni. Unaweza kumuuliza Je, wanajisikiaje?

Unaweza kumsaidia kwa kumjulisha kwamba si lazima aripoti chochote rasmi, lakini ni muhimu kuzungumza na mtu ambaye anaweza kusaidia.

Zingatia;-​

Rafiki yako anaweza kuwa na hisia dhaifu. Kuwa mkarimu kwake , msaidie kufikira anachowezqa kusema. Jitolee kwenda nae ikiwa ataamua kwenda kutoa malalamiko rasmi. Muhimu zaidi, mkumbushe kuwa uko kwa ajili yake na unataka kumsaidia.

Ikiwa rafiki yako bado hataki kuripoti tukio hilo, basi umuunge mkono kutafuta mtu mzima anayemwamini ambaye anaweza kumsaidia kukabiliana na hali hiyo. Kumbuka kwamba katika hali fulani matokeo ya unyanyasaji mtandaoni yanaweza kutishia maisha.

Kutofanya chochote kunaweza kumfanya mtu ahisi kwamba kila mtu yuko kinyume naye au kwamba hakuna anayejali. Maneno yako yanaweza kuleta mabadiliko.

Serikali na makampuni ya intaneti wameshindwa kuzuia chuki mtandaoni

Unsplash/Priscilla du Preez

Serikali na makampuni ya intaneti wameshindwa kuzuia chuki mtandaoni

7. Je, kuna adhabu ya uonevu mtandaoni?​

Shule nyingi huchukulia uonevu kwa uzito na watachukua hatua dhidi ya aliyeanya uonevu. Ikiwa unadhulumiwa mtandaoni na wanafunzi wengine, ripoti kwa shule yako.

Watu ambao ni waathirika wa aina yoyote ya unyanyasaji, ikiwa ni pamoja na uonevu na uonevu mtandaoni, wana haki ya kupata haki na kuwajibishwa mkosaji.

Sheria dhidi ya unyanyasaji, haswa juu ya uonevu wa mtandaoni, ni mpya na bado hazipo kila mahali. Hii ndiyo sababu nchi nyingi hutegemea sheria zingine zinazofaa, kama vile dhidi ya unyanyasaji, kuadhibu wanyanyasaji wa mtandao.

Katika baadhi ya nchi zenye sheria hizi, waathiriwa wa unyanyasaji wa mtandaoni wanaweza kutafuta ulinzi, kuzuia mawasiliano kutoka kwa mtu maalum na kuzuia matumizi ya vifaa vya kielektroniki vinavyotumiwa na mtu huyo kwa uonevu wa mtandaoni, kwa muda au kwa kudumu.

Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa adhabu si mara zote njia bora zaidi ya kubadili tabia ya waonevu. Mara nyingi ni bora kuzingatia kurekebisha madhara na kurekebisha uhusiano.

Social media can fuel the spread of COVID-19 misinformation.

Unsplash/Ruth Burrows

Social media can fuel the spread of COVID-19 misinformation.

8. Nyenzo za mtandaoni za kuzuia unyanyasaji na Uonevu kwa watoto au vijana​

Kila mtandao wa kijamii hutoa zana tofauti zinazokuruhusu kuweka vikwazo kuhusu nani anayeweza kutoa maoni au kutazama machapisho yako au anayeweza kuunganishwa kama rafiki, na kuripoti visa vya uchokozi.

Nyezo nyingi kati ya hizo zinahusisha hatua rahisi za kuzuia, kunyamazisha au kuripoti unyanyasaji wa mtandaoni.

Kampuni za mitandao ya kijamii pia hutoa elimu na mwongozo kwa watoto, wazazi na walimu kujifunza kuhusu hatari na njia za kukaa salama mtandaoni.

Kumbuka ya kwanza ya ulinzi dhidi ya uonevu mtandaoni inaweza kuwa wewe mwenyewe. Fikiria kuhusu mahali ambapo unyanyasaji wa mtandaoni hutokea katika jumuiya yako na njia unazoweza kusaidia kwa kupaza sauti yako, kuwataja waonevu, kuwasiliana na watu wazima unaowaamini au kwa kutoa ufahamu kuhusu suala hilo.

Kama umeshawahi kufanyiwa uonevu mtandaoni haupo pekeyako , tazama video hii ya vijana waliofanyowa uonevu ambao wanaeleza namna uya kukabiliana na hali hiyo.

Chanzo: Umoja wa Mataifa
 
Back
Top Bottom