SoC03 Mamlaka zitunge sheria ya kudhibiti mitandao ya simu kuuza taarifa za wateja wao

Stories of Change - 2023 Competition

Mabogo Jr

Member
Jan 27, 2018
33
44
Habari ya leo wana JF. Leo ningependa kuongelea maada tajwa hapo juu. Tafadhali fuatilia mkeka huu.

Kwa miaka kadhaa sasa imekuwa kama utaratibu wa kawaida kwa maelfu ya watumiaji wa mitandao ya mawasiliano nchini kupokea jumbe tofauti za matangazo ya biashara na huduma mbali mbali za makampuni ya michezo ya kubahatisha (bahati nasibu) zikinadi na kumshawishi mlengwa kujihusisha nazo. Jumbe hizi huja kwa kujirudia rudia karibu kila siku na imefika wakati inakuwa kero kwa watumiaji wengi wa mitandao ya mawasiliano kwani wamekuwa wahanga wa matangazo haya ambayo mara nyingi huja bila ridhaa yao kwani utakuta wengi wao hawajihusishi kabisa na biashara hizo na pengine hatahawa zihitaji.
IMG_20230624_102722.jpg
IMG_20230624_102549.jpg
Mbali kero hii ya jumbe nyingi za matangazo haya ya bahati nasibu, baadhi ya jumbe zimekuwa zinahusisha gharama za kila siku kwa (mlengwa) mteja wa mtandao husika, gharama mbayo hukatwa kutoka katika akiba ya muda wa maongezi (salio). Gharama hii hudaiwa kuwa malipo ya huduma inayo husiana na ujumbe husika, kwamaana nyingine jumbe hizi huonesha kama mlengwa amejisajili ili kupata huduma hiyo na kwamba atakuwa akilipia gharama za kila siku, jambo hili nalo mara nyingi hufanyika bila ridhaa na muhanga anakuwa huyo mteja wa mtandao husika wa mawasiliano na wengi wao hawana namna ya kujitoa kwani hawajui hata waliunganishwa vipi.​
IMG20230624102154.jpg
IMG_20230624_110957.jpg
IMG_20230624_111026.jpg

Ni kwa namna gani jumbe hizi huwafikia watumiaji wa mitandao ya simu bila wao kujisajili kwa huduma hizo?

Ikiwa nawe ni mmoja wa wahanga wa suala hili, si ajabu ukawa ukijiuliza swali hili kama ilivyo kwa watu wengine wengi wanao pitia adha hii. Kimsingi ukitazama wingi wa jumbe hizo utagundua kwamba zinatoka sehemu tofauti (watangazaji tofauti), hii inaleta picha ya kwamba makampuni yote haya yana uhuru wa kutumia taarifa za mteja kama namba za simu bila hiari ya mhusika (mwenye namba). Uhuru huu unaweza kuwa kiashiria kwamba wanapata taarifa hizi kutoka kwa makampuni yanayo toa huduma za mawasiliano ama kwa malipo au kwa kushiriki pamoja katika faida itokanayo na matangazo hayo. Jambo hili mbali na kuwa kero kubwa kwa watumiaji wa mitandao, pia ni udhirisho wa wazi kwamba taarifa binafsi za mtu zinaweza kusambazwa na kutumika kwa matumizi mengine hata zaidi ya hayo bila ridhaa ya mwenye taarifa, jambo ambalo si zuri sana kwani watu wengi huchagua huduma za mitandao hii kwaajili ya mawasiliano na huduma za kifedha tu. Hivyo suala hili la matumizi ya taarifa binafsi za watumiaji wa mitandao linaonesha namna gani uwepo wao (watumiaji wa mitandao) unatumika kunufaisha watu na makampuni mengine bila hiari yao na wala wao wenyewe kunufaika.


Nini kifanyike ili kudhibiti na kulinda taarifa binafsi za watumiaji wa mitandao ya mawasiliano
Tunayo mamlaka yenye dhamana ya usimamizi na udhibiti wa huduma za mawasiliano nchini (TCRA). Serikali kupitia mamlaka hii inaweza weka utaratibau sheria mahsusi kwajili ya kudhibiti na kulinda usalama wa taarifa binafsi za watumiaji wa huduma za mawasiliano. Maoni yafuatayo yanaweza tumika na mamlaka husika katika utekelezaji wa seraya ulinzi wa taarifa binafsi za watu.

Mamlaka ya mawasiliaono Itunge sheria au utaratibu utakao wadhibiti watoa huduma hizo nchini ili wawajibike katika kulinda taarifa za wateja wao. Taarifa kama namba ya simu ya mteja ni binafsi ya mteja na japokuwa atapokea jumbe za matangazo kupitia namba yake, basi matangazo hayo yawe yanahusiana na huduma za mtandao husika au ikiwa amejisajili mwenye kupata huduma za ziada kama hizo za michezo ya bahati nasibu (betting). Sheria hii iambatane na adhabu stahiki kwa kampuni ambayo itaendelea kuruhusu wateja wake kutumiwa jumbe za matangazo ambayo yanakuja bila idhini ya mteja husika, yani kwa huduma ambazo mteja hajajisajili na wala sio za kiserikali.

Mamlaka au Wizara inayohusika na mambo ya TEHAMA pamoja na ile inayo husika ya michezo ya bahati nasibu (betting) ziweke utaratibu wa kudhibiti matangazo ya biashara yale yanayo tumia mfumo wa jumbe fupi za mawasiliano (SMS) ambazo zimekuwa zikitumwa moja kwa moja kwa watu hata wasio jihusisha na michezo hiyo. Utaratibu huu uwekwe si kwa lengo la kudhibiti makampuni haya kujitangaza, bali ili yaweze kuzingatia na kujihusisha na watu ambao nao wanajihusha na huduma zao tu. Hii itasaidia katika kupunguza kero kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano pamoja na makato ambayo yamekuwa yakikatwa kutoka katika akaunti za watumiaji kwa kudaiwa ni malipo ya huduma fulani ambazo utakuta hawazijui.

Watoa huduma za mawasiliano waanzishe utaratibu wa kuwajulisha au kuwa elimisha wateja wao kuhusu huduma za ziada wanazo toa kupitia kipengele cha vigezo na masharti ili kila mtumiaji wa huduma hiyo awe na ufahamu juu ya haki alizonazo mtoa huduma wake juu ya taarifa zake binafsi. Elimu hii itolewe kwa wateja waliopo na iwe endelevu hata kwa wateja wanao ongezeka kwani kila siku watu hujisajili na kuanza kutumia huduma hizi. Elimu hii pia itamsaidia mtumiaji wa huduma za mawasiliano kujua haki zake za msingi na kwamba ikiwa ataunganishwa na huduma fulani asiyo ijua basi awe na uwezo au mahala pa kuripoti suala hilo sambamba na kuwa na uwezo au namna ya kujiondoa ikiwa hajapendezwa na huduma hiyo.​
 
Back
Top Bottom