Mkuu nimesema sio mimi ila nimeshuhudia watu zaidi ya watatu wakitumia staili hiyo mmoja wapo mke wangu, na mimi nikawauliza kama wewe, walichoniambia kwa upande fulani kina mantiki. "Mmoja alisema aliamua kutumia staili hiyo kutokana na yeye mguu wake wa kushoto ndiyo wenye nguvu zaidi ya kulia, sawa na mikono ya watu wengine hutofautiana nguvu na hata matumizi, wengine hutumia hata mkono wa kushoto kuandika au kula chakula. So huwezi kumlazimisha mtu anayetumia mkono wa kushoto kutumia wa kulia."
Mwingine alisema, "kuna jamaa yake mmoja aliwahi kugonga mti akiwa anapaki gari ofisini, jamaa alihamisha mguu bila kuangalia vizuri akidhani anakanyaga brake kumbe thleluthi ya mguu wake bado ilikuwa juu ya pedal ya mafuta, ile anatua mguu kwenye pedal akidhani ni brake alishuhudia gari ikiruka na kuvaa mti". Jamaa kasema toka siku hiyo ni heri atumie yote awe na uhakika kwamba akiinua mguu kutoka kwenye pedal ya mafuta anajua kuna back up ya mguu wa kulia kwa ajili ya ku-brake incase ikitokea amekosea na gari kuondoka ghafla.
NB: Mke wangu anaendesha auto transmission na anatumia miguu yote miwili wa kushoto brake na kulia mafuta hasa akifika kwenye tight jam ili kujilinda na kugonga gari ya mbele kwa miaka takribani kumi sasa na hajagonga hata bata wa mtu.
Tuwe wa kweli ni kweli vyuoni tunafundishwa namna hata ya kuweka mkono kwenye usukani, je niwangapi kati yetu barabarani tuna-implement hiyo? Tunashudia kila siku watu wanaendesha magari wakitumia mkono mmoja, wengine wanatuma msg au kuchat kabisa.