Msaada - Gari yangu inakula sana mafuta

Msaada - Gari yangu inakula sana mafuta

Acha hizo. Hiyo ni kawaida. Mi mwenyewe nasukuma zote mannual na automatic na nikiingia auto kushoto breki kulia mafuta. It plays so well. Haya mambo ua hamisha hamisha mi siyawezi

OK mkuu, huo ni utaratibu wako na maadamu umekwisha zoea unaweza kuendelea. Lakini kitu kinanishangaza kama unaendesha manual lakini ukija kwenye Auto unalifanya hilo la kukanyaga brake kwa mguu wa kushoto??? Hebu nikuulize kwanini ile taratibu ya Manual transimission ambako kuna pedal 3 ile ya kushoto ikiwa ni ya clutch, katikati brake na kulia ni mafuta (accelerator), ambapo mguu wa kushoto ndo unatumika kwa clutch, usiitumie hapa kwenye Auto kuliko na pedal 2 na ukajikuta mguu wako wa kushoto una-rest mahali pake ambapo wamekuwekea (kuna foot rest imewekwa hapo) na mguu wako wa kulia ukafanya zile kazi ambazo hua unafanya kwenye gari ya manual??? yaani kukanyaga mafuta na brake???

Ikumbukwe kwamba ukiwa umekanyaga brake huhitaji ku-accelerate nikiwa na maana unatakiwa kuachia mafuta na ndio maana taratibu inakutaka uondoe mguu wa kulia kwenye accelerator ili uutumie kukanyaga brake kwa sababu hapo kwenye mafuta hautakiwi kwa wakati huo.You cant apply brakes while accelerating.

Pamoja na yote tunayojaribu kubadilishana, mwisho wa siku ni uamuzi wako kutumia utaratibu unaoona unakufaa.
 
mbona nilisikia gari ambazo hazili sana mafuta moja wapo ni spacio. mbona mnanichanganya? au kuna spacio ambae haikuli sana mafuta na kunayo inayokula sana. naomba mnieleweshe
 
Back
Top Bottom