Mrisho Mpoto, pumba tupu

Mrisho Mpoto, pumba tupu

Na wewe jifunze kusoma na kuelewa!!,
Nimesema sio utamaduni wetu, wapi nilipokanusha kuwa sio utamaduni wa kanisa katoliki?

Sasa kwanini ulisema si utamaduni wako? nani alikwaandikia hayo? nimesema "google Pengo" uone kavaa nini? huyo Pengo si Mtanzania? usitake kubisha mambo yaliyo wazi.
 
Sasa kwanini ulisema si utamaduni wako? nani alikwaandikia hayo? nimesema "google Pengo" uone kavaa nini? huyo Pengo si Mtanzania? usitake kubisha mambo yaliyo wazi.
Nilisema sio utamaduni wetu kwa sababu sio utamaduni wetu, na hata kama huyo Pengo ni mtanzania lakini majoho sio utamaduni wetu, Na hata hayo matambala uliyojifungasha kichwani ili uonekane macho tu sio utamaduni wetu, waachieni wazungu na waarabu.
 
Huyu jamaa kwakweli si mtu wakusema ni mhalisia wa yale anayoyasema me ninaurafiki na meneja mmoja wa hoteli fulani iliyopo maeneo ya ilala mara nyingi nyakati za jioni upendelea kwenda maeneo hayo kupiga story za hapa na pale ila kwakweli nimekuwa nikimshuhudia huyu jamaa akiingia na vibinti mara kadhaa tena katika hali isiyo na usalama wa afya yake. Kama huwa anapitaga huku asome na abadilike maana watanzania tunaimani nae kupitia nyimbo za…

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kwani Pengo akivaa nguo ndio unakuwa utamaduni wetu?

Wewe na kanzu wapi na wapi? zote wameleta wageni. Tembea na kigozi kinachoficha tupu kama unaupenda utamaduni wa babu na bibi zako.

Utamaduni wa mwenzio unaweza kuwa mzuri kuliko wako na ukautumia kuliko wako, huko ndio kustaarabika. Si unamuona Pengo anavyopendeza na kanzu.
 
Mkuu mashairi unayo sikia akiimba anaandikiwa!

Mkuu anaandikiwa na nani?.............................lakini yawezekana kabisa kwani kwa mashairi kama hayo halafu kujieleza sifuri naweza kukuamini!
 
Mkuu anaandikiwa na nani?.............................lakini yawezekana kabisa kwani kwa mashairi kama hayo halafu kujieleza sifuri naweza kukuamini!

wimbo wa kwanza kabisa mjomba mjomba aliandikiwa na Irene Sanga.......album yake ya kwanza yote "nikipata nauli" aliandikiwa na Mgunga mwa Mnyenyelwa.....waGoogle hao watu uwafahamu......cha kusikitisha Mpoto hakuwai kutoa credit wala kuwapa. asante awa watu,,alichowalipa ni dharau na kejeli....Wimbo wake mpya kaandika mwenyewe ndio maana ata ye mwenyewe hajui unahusu nini kafanya usanii wa kucheza na kiswahili kigumu kuchanganya wajinga.
 
Natazama TBC sasa hivi, huyu aitwae Mrisho Mpoto anahojiwa, jamani sijawahi kuona mtu anaongea mambo ya kijinga kama huyu kwenye TV.

Hivi ni nani huyu Mrisho Mpoto? Yaani anasema vijana wote Tanzania wanarudi kwenye utamaduni "kwa sababu yangu mimi".

Hivi huyu anajuwa maana ya utamaduni au anajisemea tu? Tanzania hii, ujisifu kuwa eti ni "ni kwa sababu yangu tu" vijana wanarudi kwenye utamaduni?

Pumba nyingine kibao, kichefuchefu.
Namuonaga havai viatu! Au ndiyo bangi zenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom