papag
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 1,241
- 1,871
SHAHADA HESHIMA YAKE IONEKANE KATIKA KAZI
Adeladius Makwega – MBAGALA
Nilipokuwa nasoma Chuo Kikuu katika Shahada ya Sanaa ya Habari, nilifundishwa somo lililoitwa Cultural Anthropology. Mhadhiri wetu alikuwa Profesa Samwel Mshana, ambaye kwa sasa ni marehemu. Alikuwa mzee mwenye busara na uzoefu mkubwa. Mara nyingi Profesa Mshana alikuwa akituambia maneno haya:
"Nyinyi hapa mnasoma kwa bahati hii Shahada ya Sanaa ya Habari, lakini waandishi wengi wa habari hawajasoma kozi hii. Wapo wenye vyeti na diploma wachache, na wengine mnawaita makanjanja. Sasa nyinyi mnaosoma shahada hii, mjitahidi kwamba mkihitimu hapa, cheti chenu cha shahada kilingane na yale mliyonayo akilini mwenu katika kila mnachokifanya kama wanahabari. Unaweza kuwa na Shahada ya Sanaa ya Habari, lakini ukipimwa katika mizani ukaonekana una kiwango cha cheti au diploma tu. Hali hii ipo hata kwetu sisi wasomi; unaweza kuwa Daktari wa Falsafa au Profesa, lakini ukipimwa ukawa na uwezo unaolingana na mhitimu wa shahada ya kwanza. Hilo ni jambo la aibu kwa msomi. Wanangu, jitahidini, maana mwandishi wa habari ni kama mwalimu anayefundisha darasa kubwa lenye watu wa aina mbalimbali. Ukileta usomi wako ukakosolewa, usilalamike, kwa sababu jamii ina watu wenye ujuzi wa mambo mengi."
Maneno haya ya Profesa Mshana yameendelea kubaki akilini mwangu, hasa ninapoangalia namna ambavyo wasomi wetu wanavyopaswa kuwa.
Nimeyakumbuka leo si kwa bahati mbaya, bali kwa sababu ya hoja kadhaa zinazohusu Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), ambalo lilipata fursa ya kuongozwa na wasomi wawili katika kipindi cha mwaka 2007 hadi 2026.
Wengi hawafahamu historia hii vizuri. Mara baada ya kuunganishwa kwa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na Televisheni ya Taifa(TVT0 tarehe 1 Julai 2007 na kuundwa TBC, Bodi ya kwanza iliongozwa na Profesa Mwajabu Possi kutoka Chuo cha Habari, ambaye wakati huo alikuwa Makamu Mkuu wa chuo hicho.
Kwa maoni yangu, bodi hiyo haikufanya vizuri. Baadaye ilivunjwa na kuundwa bodi mpya, ambayo ilimjumuisha Dkt. Ayub Ryoba, naye pia akitokea katika chuo hicho kilichoongozwa na Profesa Mwajabu Possi. Hata hivyo, Dkt. Ryoba hakukaa muda mrefu kama mjumbe wa bodi, kwani baadaye aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC.
Wakati Profesa Mwajabu Possi akiwa Mwenyekiti wa Bodi, Mwanakwetu alikuwa Mwenyekiti wa Wafanyakazi. Binafsi nilimwambia Profesa Possi maneno haya:
"Mama, hali ni mbaya. Maisha ni magumu. Wewe ni Mwenyekiti wa Bodi, lakini uko mbali na taasisi. Jaribu kuwa karibu na watumishi. Isitoshe, mshauri Rais Jakaya Kikwete kwamba utaratibu wa kuwaleta viongozi waliostaafu kuongoza shirika hili si mzuri. Mtu akistaafu, apewe nafasi ya kupumzika. Mawazo mapya yanatakiwa kusaidia kulijenga shirika, na vijana wanaoanza kazi wasikatishwe tamaa."
Nilimwambia maneno hayo mbele ya Katibu Mkuu, Dkt. Elisante.
Wakati huo, Wizara ya Habari ilikuwa na Naibu Katibu Mkuu mwanamke aliyekuwa mnyenyekevu na mwenye uelewa mkubwa. (Msomaji wangu, simaanishi Siaba Mkinga; alikuwa mama mwingine mwema ambaye kwa sasa jina lake nimelisahau.)
Katika kikao cha ndani cha viongozi, nilimwambia tena Profesa Mwajabu Possi:
"Mama, leo umekuja kwa sababu Katibu Mkuu amekuja. Lakini ulipaswa kuwa unakuja mara kwa mara kutuangalia vijana wako tunaishije. Watumishi wa TBC wanaishije? Wanawake wanafanyakazi katika mazingira gani? Mahusiano kati ya utawala na watumishi yakoje?"
Baadaye, katika kikao cha wafanyakazi wote, Profesa Possi alisema:
"Nawaombeni mfanye kazi vizuri, lakini Makwega, usiwatenge wazee."
Hoja iliyozuka ilikuwa kwamba Makwega anawachukia wazee.
Nikajibu:
"Hapana. Mimi mwenyewe nitakuwa mzee siku moja. Ninayosema ni kwa nia ya kujenga taasisi."
Hatimaye, Bodi ya Profesa Mwajabu Possi ilivunjwa na kuundwa bodi mpya iliyomjumuisha Dkt. Ayub Ryoba. Baadaye, kama nilivyosema awali, Dkt. Ryoba akateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC.
Matumaini yalikuwa makubwa, lakini kwa mtazamo wangu, mambo yaliyofuata yalikuwa tofauti na matarajio.
Msomaji wangu, leo naomba nikushirikishe maoni ya baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Dkt. Ayub Ryoba akiwa TBC katika ngazi ya menejimenti.
Kwa sababu za kulinda utambulisho wao, nitawapa majina ya kubuni.
Sauti ya Kwanza – "Kayamba"
"Dkt. Ryoba aliaminiwa sana, lakini alipokuwa TBC alikuwa kituko. Fikiria tunaingia kwenye kikao cha menejimenti, barua inawekwa kwenye projekta, halafu tunaanza kujadili namna ya kuiandika. Hivi kweli menejimenti ya shirika la umma inapaswa kujadili namna ya kuandika barua?
Uandishi wa barua tulifundishwa tangu shule ya msingi. Vikao vya menejimenti vilipaswa kujadili namna ya kuboresha vipindi, kutambua udhaifu wa shirika, kuboresha matangazo na kutafuta njia za kuongeza mapato.
Tulimweleza hilo. Nakumbuka mzee mmoja alimwambia, 'Wenzako akina Tido Mhando hawakuwa wanaendesha vikao kwa namna hii. Tunapoteza muda. Walikuwa wanajadili mambo ya msingi ya uendeshaji wa shirika.' Maneno hayo yalimkasirisha sana.
Makwega, nina hakika wewe ulikuwa mkali katika kutetea haki za wafanyakazi. Naam, ninaamini kama ungekuwa kwenye vikao vya Dkt. Ryoba alipokuwa Mkurugenzi Mkuu usingekubali hali hiyo."
Hiyo ndiyo sauti ya kwanza, niliyoipa jina la Kayamba.
Sauti ya Pili – "Marimba"
"Mimi, huyu jamaa aliagiza nihamishiwe katika taasisi nyingine. Nikapewa barua na nikaondoka. Baadaye walishindwa kupata mtu wa kufanya kazi niliyokuwa nafanya. Kilichofuata kilinishangaza.
Dkt. Ryoba akaanza kuandika barua mara kwa mara kwenda katika taasisi niliyokuwa nimehamishiwa, akiniomba nirudi kufanya vipindi TBC kwa muda huku nikilipwa posho nzuri.
Baadaye suala hilo likafuatiliwa. Wakaulizwa, 'Mbona mliridhia mtumishi huyu ahamishiwe taasisi nyingine, halafu leo mnamrudisha kwa barua na kumpa posho, huku mkieleza kuwa yeye ndiye mtaalamu wa kazi hiyo? Kama alikuwa mtaalamu muhimu kiasi hicho, kwa nini mliruhusu ahamishwe?'
Dkt. Ryoba hakuwa na majibu. Hatimaye wakaacha kuniita. Kwa upande wangu niliona hilo lilikuwa sahihi, kwa sababu kama nilikuwa mtaalamu mnayenihitaji, haikuwa na mantiki kunihamisha halafu mnitumie kwa utaratibu wa posho. Hapo ndipo nilipoona udhaifu wake mkubwa; alishindwa kutambua kuwa kinachotuunganisha kazini ni kazi, si urafiki."
Hii ndiyo sauti ya pili, ambayo nimeipa jina la Marimba.
Sauti ya Tatu – "Ngoma"
Mdau mwingine alisema yafuatayo:
"Dkt. Ryoba kwa sasa anauambia umma mambo mengi ambayo si sahihi. Pia, vyombo vya habari vinavyomhoji mara nyingi haviandai maswali ya kina. Anaongea kana kwamba bado ndiye kiongozi wa TBC, ilhali rekodi yake akiwa Mkurugenzi Mkuu si ya kujivunia.
Hawezi kudai kwamba mafanikio makubwa ni kuhamisha matangazo kutoka analojia kwenda dijitali. Huo ulikuwa mwelekeo wa dunia nzima; haukuwa jambo ambalo lingeepukika. Hoja ya msingi ni: aliboresha nini katika vipindi vya TBC?
Anadai CHADEMA walikataa kushirikiana na TBC. Ninachokifahamu ni kwamba CHADEMA walilalamikia namna TBC ilivyokuwa ikirusha mikutano yao ya moja kwa moja. Mara nyingi, hoja nzito zilipoanza kutolewa, kamera zilihamishiwa kwa watangazaji waliokuwa studio badala ya kuendelea kuonyesha kilichokuwa kinaendelea kwenye mkutano. Kitaaluma, unapokuwa unarusha matangazo ya moja kwa moja, jukumu lako ni kuonyesha kinachoendelea, si kukatiza maudhui kwa mazungumzo ya studio."
"Pia amekuwa akitoa mfano wa Marekani bila kuueleza kwa usahihi mfumo wake wa vyombo vya habari. Hoja zake kuhusu Marekani zina mapungufu makubwa."
"Anadai kwamba akiwa TBC hakuwahi kupokea maelekezo kutoka mahali popote, lakini baadaye anakiri kwamba alipigiwa simu zenye maelekezo. Kauli hizo zinapingana."
Huyu mdau nimempa jina la Ngoma.
Kwa hakika, maoni ya Kayamba, Marimba na Ngoma yanatoa taswira ya namna baadhi ya watumishi walivyoitazama menejimenti ya wakati huo.
Msomaji wangu, baada ya kuyasoma maoni haya, nakusihi uyakumbuke tena yale maneno ya mhadhiri wangu wa Chuo Kikuu, Profesa Samwel Mshana:
"Nyinyi hapa mnasoma kwa bahati hii Shahada ya Sanaa ya Habari, lakini waandishi wengi wa habari hawajasoma kozi hii. Wapo wenye vyeti na diploma wachache, na wengine mnawaita makanjanja. Sasa nyinyi mnaosoma shahada hii, mjitahidi kwamba mkihitimu hapa, cheti chenu kilingane na maarifa mliyonayo na namna mnavyotekeleza taaluma yenu. Hata sisi wasomi tunaweza kuwa na vyeo vikubwa vya kitaaluma, lakini tukapimwa tukakutwa uwezo wetu haulingani na hadhi tuliyonayo. Hilo ni jambo la aibu kwa msomi. Mwandishi wa habari ni kama mwalimu anayefundisha jamii yenye watu wa aina mbalimbali. Ukikosoa au ukakosolewa kwa hoja, usilalamike, kwa sababu jamii ina watu wenye uelewa wa mambo mengi."
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Maoni ya Kayamba, Marimba na Ngoma yanaweza kutofautiana na mitazamo kadhaa, lakini yana ujumbe mmoja muhimu: kiongozi hupimwa zaidi na namna anavyoendesha taasisi kuliko namna anavyoizungumzia baada ya kuondoka madarakani. Kutoka kwa Kayamba, funzo ni kwamba menejimenti inapaswa kujadili masuala ya kimkakati yanayoboresha taasisi, kama vile ubora wa vipindi, ubunifu, mapato na maendeleo ya shirika, badala ya kutumia muda mwingi kwenye mambo ya msingi ambayo yanaweza kushughulikiwa katika ngazi nyingine za kiutendaji.
Kutoka kwa Marimba, funzo ni kwamba kiongozi anatakiwa kuthamini na kuwatunza wataalamu wake. Uamuzi wa kumhamisha mtumishi unapaswa kuwa wa kitaasisi na wenye sababu za msingi. Ikiwa baadaye taasisi inamlazimika kumtegemea tena mtumishi huyo kwa sababu ndiye mwenye ujuzi unaohitajika, ni ishara kwamba maamuzi ya awali hayakufanywa kwa umakini wa kutosha. Uongozi bora hujenga watu badala ya kuwatenga.
Kutoka kwa Ngoma, funzo ni kwamba msomi na kiongozi wa zamani anapozungumza hadharani kuhusu taasisi aliyoiongoza, anapaswa kuzingatia ukweli, ushahidi na usahihi wa kitaaluma. Kauli zinazotolewa mbele ya umma zinapaswa kuwa thabiti, zisizojipinga na zenye lengo la kujenga taasisi pamoja na taaluma ya habari.
Kwa ujumla, maoni haya matatu yanatoa somo kwamba uongozi mzuri hujengwa kwa kusikiliza watu, kuthamini wataalamu, kufanya maamuzi yenye mantiki, kutumia muda kwenye masuala ya kimkakati na kukubali kukosolewa kwa hoja. Hayo ndiyo yanayojenga heshima ya kudumu kwa kiongozi na kuacha urithi wenye manufaa kwa taasisi na taifa.
Kwako Dkt. Ayub Ryoba ninakwambia waziwazi haikuitendea haki taaluma yetu ulipokuwa pale TBC.
Mwanakwetu upo?Kumbuka:
“Shahada Heshima Yake Ionekane Katika Kazi.”
Nakutakia Siku njema.
Barua pepe:
makwadeladius@gmail.com
Simu: 0717 649 257