Mrisho Gambo: Agizo la Rais kwa TRA kutofungia Biashara liingie kwenye Sheria ya Fedha

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118

Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo amehoji sababu za Serikali kutoingiza kwenye Muswada wa Sheria ya Fedha maelekezo ya Rais Samia kwa Mamlaka ya Mapato (TRA) ya kutofungia Biashara kwa kigezo cha madeni ya nyuma licha ya Waziri wa Fedha kutaja jambo hilo kama pendekezo kwenye Bajeti Kuu.

Gambo amesema suala hilo linapaswa kuingizwa kwenye Sheria ili kuepusha kuwaingiza TRA kwenye mtihani wa kuendelea kufunga biashara kwasababu suala hilo haliko Kisheria bali maelekezo ya tu Viongozi.

Aidha, ameongeza kuwa TRA watakapoacha kufunga biashara waache pia kufungia akaunti za Wafanyabiashara pamoja na kuchukua Vifaa vyao zikiwemo Kompyuta kwa maelezo ya kwenda kufanya uchunguzi wa masuala ya Kikodi.
 

Attachments

  • 2023-06-21 14-53-11.mp4
    25.8 MB
Back
Top Bottom