Mrejesho wa Vodacom wamefungia line yangu yenye milioni 10 M pesa

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Wakuu habari, juzi nilileta uzi kuhusu line yangu kufungiwa

Kabla ya yote kwanza niwajibu waliokuwa wakilaumu au kushangaa mtu kuweka milioni 10 kwenye M pesa wakisema benki ndio salama

Benki unaweza kuweka na hela zako zikipotea vilevile, kama mnakumbuka kuna benki kama 3 zilifungwa kipindi cha Magufuli kutokana na benki hizo kufilisika na waliokuwa na fedha humo kuzipata ikawa ni mtihani,

So ishu inategemea umeweka hela benki gani au mtandao gani, kama benki haina afya au mtandao hauna afya hela inapotea

Nirudi kwenye mrejesho, kuna jamaa alinipa namba ya dada anayefanya kazi TCRA makao makuu, akanionyesha ushirikiano vizuri na kunipa namba ya mkuu wa kitengo kinachohusika na malalamiko ya wateja

Baada ya kuwasiliana na mkuu huyo wa kitengo akaniambia nirudi Vodacom na kama line yangu haitafunguliwa siku hiyo basi nimpigie nikiwa hapohapo

Nikaenda Vodacom asubuhi wakaniambia leo lazima niondoke na line yangu ikiwa inafanya kazi maana usumbufu ulikuwa umezidi

Nikasubiri mpaka saa tisa, najaribu kupiga bado haikubali. Jamaa akaniambia nichomoe line kwenye simu niwape wakaondoka nayo, siku zote hizo line nilikuwa sijawapa ile line bali nawatajia namba tu

Jamaa kurudi akaniambia lin iliyokuwa kwenye simu yangu wameiangalia na wameona haikuwa ile niliyowatajia na line hiyo inaonyesha niliifunga tarehe 12 mwezi wa pili,

Aisee nilishikwa na hisia tatu tofauti kwa wakati mmoja mshangao , furaha na kukosa pozi

Ni kweli kuwa tarehe 12 nilienda Vodacom na kufuta line moja ya Vodacom niliokuwa naitumia kwenye device ya intaneti,
Lakini kumbe ile line niliyoifuta niliichanganya na line iliyokuwa na hela sababu zote zinafanana muonekano

Sababu niliiweka kwenye simu na ikawa inasoma mnara vizuri, nikaona ipo sawa hadi nilipojaribu kupiga simu zikawa haziendi

nikamwaambia a renew ile line iliyokuwa na hela sababu nilikuwa sina uhakika na nilipoiweka

Jamaa akawa ananiuliza ilikuwaje nikachanganya line na kuwahangaisha kiasi kile, nikawapa pole ambayo hata hakuitikia.
Nikahakiki salio na kuchukua line yangu na kuondoka

Nimewajibika kuleta huu mrejesho sababu nilichangia kwa kiasi flani watu kukosa imani na Vodacom kwa sababu yangu

Pia soma: Vodacom wamefungia line yangu ikiwa na milioni 10 kwenye M-PESA
 
Asante na hongera kwa kuonesha hekima kubwa na kukubali pale ulipokosea
 
Kosa la mteja. Bado anadunda tu kitaa. Ingekua kua upande w voda munge imba pambio ni wezi ni wezi hayo makampuni. Pia waziri nape anashirikia nayo
Ndio maana kwa weledi wake akaamua kuleta mrejesho na hata hao voda wanastahili lawama kwakuwa hawakuchukua hatua stahiki tangu siku ya kwanza huku wakimwongopea kwamba aliyefungia line yake ni TCRA
 
Wakuu habari, juzi nilileta uzi kuhusu line yangu kufungiwa

Kabla ya yote kwanza niwajibu waliokuwa wakilaumu au kushangaa mtu kuweka milioni 10 kwenye M pesa wakisema benki ndio salama

Benki unaweza kuweka na hela zako zikipotea vilevile, kama mnakumbuka kuna benki kama 3 zilifungwa kipindi cha Magufuli kutokana na benki hizo kufilisika na waliokuwa na fedha humo kuzipata ikawa ni mtihani,

So ishu inategemea umeweka hela benki gani au mtandao gani, kama benki haina afya au mtandao hauna afya hela inapotea

Nirudi kwenye mrejesho, kuna jamaa alinipa namba ya dada anayefanya kazi TCRA makao makuu, akanionyesha ushirikiano vizuri na kunipa namba ya mkuu wa kitengo kinachohusika na malalamiko ya wateja

Baada ya kuwasiliana na mkuu huyo wa kitengo akaniambia nirudi Vodacom na kama line yangu haitafunguliwa siku hiyo basi nimpigie nikiwa hapohapo

Nikaenda Vodacom asubuhi wakaniambia leo lazima niondoke na line yangu ikiwa inafanya kazi maana usumbufu ulikuwa umezidi

Nikasubiri mpaka saa tisa, najaribu kupiga bado haikubali. Jamaa akaniambia nichomoe line kwenye simu niwape wakaondoka nayo, siku zote hizo line nilikuwa sijawapa ile line bali nawatajia namba tu

Jamaa kurudi akaniambia lin iliyokuwa kwenye simu yangu wameiangalia na wameona haikuwa ile niliyowatajia na line hiyo inaonyesha niliifunga tarehe 12 mwezi wa pili,

Aisee nilishikwa na hisia tatu tofauti kwa wakati mmoja mshangao , furaha na kukosa pozi

Ni kweli kuwa tarehe 12 nilienda Vodacom na kufuta line moja ya Vodacom niliokuwa naitumia kwenye device ya intaneti,
Lakini kumbe ile line niliyoifuta niliichanganya na line iliyokuwa na hela sababu zote zinafanana muonekano

Sababu niliiweka kwenye simu na ikawa inasoma mnara vizuri, nikaona ipo sawa hadi nilipojaribu kupiga simu zikawa haziendi

nikamwaambia a renew ile line iliyokuwa na hela sababu nilikuwa sina uhakika na nilipoiweka

Jamaa akawa ananiuliza ilikuwaje nikachanganya line na kuwahangaisha kiasi kile, nikawapa pole ambayo hata hakuitikia.
Nikahakiki salio na kuchukua line yangu na kuondoka

Nimewajibika kuleta huu mrejesho sababu nilichangia kwa kiasi flani watu kukosa imani na Vodacom kwa sababu yangu

Pia soma: Vodacom wamefungia line yangu ikiwa na milioni 10 kwenye M-PESA

Kwa hiyo usumbufu wote huu ni upumbavu wako?
 
Acha kudanganya mkuu au unafikiri JF wote wanapenda hizo fix zako.. laini ukishaifuta usajili huwezi kuirenew tena.

Alafu swali lingine unalokwepa ni kwa vipi laini yako iwe na access ya kuhifadhi hadi milioni 10 wakati ni laini ya kawaida na sio ya biashara
 
Hata asingeleta mrejesho aisee, kawasema watu vibaya kweli.
Sikuwasema hata vibaya, kasome uzi wangu wa mwanzo tena
Nilikuwa naelezea mtiririko wa nilivyokuwa naenda ofisi zao na nilichokuwa naambiwa na Vodacom

Sikusema kuwa wanataka kuiba hela au ni makusudi japo kuna wachangiaji wengi walisema hivyo

Kuleta mrejesho ni kuwaondoa Vodacom kwenye tuhuma hizo na kujibebesha lawama
 
Acha kudanganya mkuu au unafikiri JF wote wanapenda hizo fix zako.. laini ukishaifuta usajili huwezi kuirenew tena.

Alafu swali lingine unalokwepa ni kwa vipi laini yako iwe na access ya kuhifadhi hadi milioni 10 wakati ni laini ya kawaida na sio ya biashara
Line iliyokuwa renewed sio niliyoifuta, soma tena

Line za kawaida zinafaa hadi milioni 10, zamani ilikuwa milioni 5, za biashara hadi milioni 50
 
Back
Top Bottom