Vodacom, huu ni wizi mpya mlioubuni? Nirudishieni 30000 yangu M-PESA

mfate42

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
3,770
4,260
Habari IPO namna hii,

Mimi ni mwenyekiti wa kikundi Fulani na watu huwa wanatuma pesa zao kwenye akaunt yangu kwa ajili ya kuwalipia M-Koba..

Laini nnayoitumia nliisajili kwa kitambulisho cha nida cha mke,. Nikaona isiwe kesi ,mke afute usajili ili nisajili kwa kitambulisho changu..na wakati huo akauntu ilikuwa na sh.30000..

Cha kushangaza Mara baada ya mke kufuta usajili na nikasajili kwa kitambulisho changu ile 30000 wakaifyeka, nikawapigia wakasema niende voda shop iliyo karibu yangu niwaeleze watanipa fomu nijaze nikafika walichonijibu wanasema nihesabu nimepoteza hiyo hela na nikiitaka basi niende mkoani kampuni ya voda naomba chonde chonde rudishen pesa hiyo haraka kabla sijawaburuza mahakamani
 
Cha kushangaza Mara baada ya mke kufuta usajili na nikasajili kwa kitambulisho changu ile 30000 wakaifyeka ,.nikawapigia wakasema niende voda shop iliyo karibu yangu niwaeleze watanipa fomu nijaze ..nikafika walichonijibu wanasema nihesabu nimepoteza hiyo hela..na nikiitaka basi niende mkoani ...kampuni ya voda naomba chonde chonde rudishen pesa hiyo haraka kabla sijawaburuza mahakamani
Imebaki kwenye account ya mkeo
 
Kosa ufanye wewe alafu ulaumu wengine...

Moja kutumia line ya mwingine ni kosa; kwahio ili wapate uhakika kwamba wewe sio mwizi unayefuta line na kujifanya ni yako (different owner) lazima kuwe na uhakiki na watu wa kufanya uhakiki wapo mikoani....

Sasa wakikupa Pesa, kumbe sio yako ni ya Mke wako kabla ya wewe kujifanya kubadilisha usajili itakuwaje...

Hizo ni security reasons ambazo zimesababishwa na wewe kwa kutumia line isiyo yako...
 
Back
Top Bottom