Msaada: Vodacom ilichonifanyia ni uharamia

Shozylin

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
297
607
Mm ni mjasiliamali ninae toa huduma zakifedha kupitia simu za mkononi (wakala)

N Nina miliki laini mbili za uwakala till. Moja ninaitumia kwenye ofisi yangu na laini nyingine inatumika kwenye ofisi nyingine ambayo msimamizi wake ni kaka angu.

Tarehe 25/03/ 2024 saa 3:46 na saa 4 :41 usiku

Nilikatwa jumla ya fedha sh 1,233,000 wakadai ni wamekata kulipa madeni niliyo kopa kwenye wakala songesha na wezesha. Kimsingi mm kwenye laini yangu iliyopo ofisini kwangu sikua na deni lolote.

Ikabidi niwapigie kufahamu wakanambia kua hayo ni madeni ya till zako zingine yamehamishiwa kwako, nikampgia kaka kumuuliza Kama kweli alikopa akakiri kua kweli alikopa na ana deni la laki 994,000 nikafikili huwenda pengine wamekata kutokana na Hilo deni.

Jana tarehe 26 saa12 :03 nikatumiwa sms na Vodacom songesha kua kwakua nime feli kulipa deni la sh milion 7,772,062 hivyo nimefungiwa huduma ya kukopa. Nikachanganyikiwa milion 7 zimetoka wapi hizi?

Maana yake ukichukua 1,233,000 zilizo katwa + deni lililobaki kwa mujibu wa taarifa zao nakua na jumla ya deni la sh milion 9,005,062.

Nikapatwa na mshituko hizi fedha zimetoka wapi nikaenda kuonana na kaka kwenye ofisi namba 2 nikakagua ile till line juma ya madeni nikakuta songesha wanaidia laki 544, 000 na wezesha wanadai 450,000 jumla ya deni ni laki 994000 hizi ni pamoja na riba.

Nikastaajabu mbona deni la huku ni laki 9 halafu kwangu lina soma deni la milion 9.

Cha kustaajabisha nikua kwenye zile sms za makato ya kile kiasi Cha milion 1.2 wameelekeza kua deni limetoka till number flani ambayo ki msingi si yangu na na Mimi si mmiliki wa till hiyo na Haina usajili wangu.

Niliwapgia Vodacom kuwaelezea wakanipa majibu mepesi tu kua Hilo deni limetoka kwenye till zako zingine. Nikakataa kua kwneye till yangu namba 2 Nina deni la laki 9 na sio milion 9 tukapishana na mhudumu akakata simu bila msada.

Nimarudia tena kupiga simu nikaelekezwa niende Vodacom shop, nikaenda Vodacom shop nikakuta mhudumu wa pale hausiki na mawakala akanielekeza namba ya mhusika nikampgia simu nikamwelezea scenario nzima akasema acha akague madeni yangu atanirudia, hajarudi mpaka Sasa.

Hapa sjafungua office leo nimelala ndani Nina stress za kutosha, kumbe ndio maana wanaume tunakufa mapema, nimewaza mengi sanaa kuhusu haya maisha.

Wakuu inawezekana kuipeleka Vodacom mahakamani? Nianzie wapi kufanya hivyo?

Nawapelekeaje mahakamani wakati line yangu namba 2 tayari kaka Alisha ikopea laki 9 .? Naombeni msaada Kama hujaelewa tahadhali nitakuelewesha pia kwenye comment vodacom

Update.

Mpaka mda huu tayari voda wameondoa deni nililobambikiziwa la milion 7.7 na sina deni lolote mpaka Sasa nacho subiri ni wao kurejesha pesa waliyo chukua.
 
Hizo till number umesajili kwa jina lako? Au ndo zile mlikua mnanunua kwa dili? Ila sidhani kama ni busara au sheria kuhamisha deni kutoka till number hii kwenda nyingine
Mm ni mmiliki halali wa till number mbili ambayo moja naitumia Mimi na nyingine anaitumia kaka.

Zote nimesajili kwa documents zangu.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mimi hata niishiwe vipi; siwezi kukopa songesha ya aina yoyote ile kutoka voda! Na pia siwezi kamwe kuingia kwenye ule mtego wao wa voda bima!!

Voda siyo mtandao poa hata kidogo. Ni vile tu tupo huko, kwa sababu hatuna mahali pengine pa kukimbilia.
 
Kuna uwezekano nyaraka zako zilitumika kutengeneza line zingine zaidi ya hizo mbili halali.
Hao ma freelancer huwa wanadublicate line na kuziuza.
Km ni hivyo hapo imekuka kwako mkuu
 
Mm ni mjasiliamali ninae toa huduma zakifedha kupitia simu za mkononi (wakala)

N Nina miliki laini mbili za uwakala till. Moja ninaitumia kwenye ofisi yangu na laini nyingine inatumika kwenye ofisi nyingine ambayo msimamizi wake ni kaka angu.

Tarehe 25/03/ 2024 saa 3:46 na saa 4 :41 usiku

Nilikatwa jumla ya fedha sh 1,233,000 wakadai ni wamekata kulipa madeni niliyo kopa kwenye wakala songesha na wezesha. Kimsingi mm kwenye laini yangu iliyopo ofisini kwangu sikua na deni lolote.

Ikabidi niwapigie kufahamu wakanambia kua hayo ni madeni ya till zako zingine yamehamishiwa kwako, nikampgia kaka kumuuliza Kama kweli alikopa akakiri kua kweli alikopa na ana deni la laki 994,000 nikafikili huwenda pengine wamekata kutokana na Hilo deni.

Jana tarehe 26 saa12 :03 nikatumiwa sms na Vodacom songesha kua kwakua nime feli kulipa deni la sh milion 7,772,062 hivyo nimefungiwa huduma ya kukopa. Nikachanganyikiwa milion 7 zimetoka wapi hizi?

Maana yake ukichukua 1,233,000 zilizo katwa + deni lililobaki kwa mujibu wa taarifa zao nakua na jumla ya deni la sh milion 9,005,062.

Nikapatwa na mshituko hizi fedha zimetoka wapi nikaenda kuonana na kaka kwenye ofisi namba 2 nikakagua ile till line juma ya madeni nikakuta songesha wanaidia laki 544, 000 na wezesha wanadai 450,000 jumla ya deni ni laki 994000 hizi ni pamoja na riba.

Nikastaajabu mbona deni la huku ni laki 9 halafu kwangu lina soma deni la milion 9.

Cha kustaajabisha nikua kwenye zile sms za makato ya kile kiasi Cha milion 1.2 wameelekeza kua deni limetoka till number flani ambayo ki msingi si yangu na na Mimi si mmiliki wa till hiyo na Haina usajili wangu.

Niliwapgia Vodacom kuwaelezea wakanipa majibu mepesi tu kua Hilo deni limetoka kwenye till zako zingine. Nikakataa kua kwneye till yangu namba 2 Nina deni la laki 9 na sio milion 9 tukapishana na mhudumu akakata simu bila msada.

Nimarudia tena kupiga simu nikaelekezwa niende Vodacom shop, nikaenda Vodacom shop nikakuta mhudumu wa pale hausiki na mawakala akanielekeza namba ya mhusika nikampgia simu nikamwelezea scenario nzima akasema acha akague madeni yangu atanirudia, hajarudi mpaka Sasa.

Hapa sjafungua office leo nimelala ndani Nina stress za kutosha, kumbe ndio maana wanaume tunakufa mapema, nimewaza mengi sanaa kuhusu haya maisha.

Wakuu inawezekana kuipeleka Vodacom mahakamani? Nianzie wapi kufanya hivyo?

Nawapelekeaje mahakamani wakati line yangu namba 2 tayari kaka Alisha ikopea laki 9 .? Naombeni msaada Kama hujaelewa tahadhali nitakuelewesha pia kwenye comment vodacom
mpaka sasa hivi hujaenda voda makao makuu

andaa mwanasheria wako
 
Pole sana mkuu .
Mimi niliweka akiba Mgodi siku niitoe nifurahi na marafiki ikagoma nikapiga simu sikupata msaada ikabidi niwatishie kumbana wakala wao , hela zangu zikatoka ndani ya saa moja
Toka hapo siweki hela mpesa mimi nsogopa sana
 
Kuna uwezekano nyaraka zako zilitumika kutengeneza line zingine zaidi ya hizo mbili halali.
Hao ma freelancer huwa wanadublicate line na kuziuza.
Km ni hivyo hapo imekuka kwako mkuu
Mkuu haipo hivyo. Hakuna lain ya voda yoyote iliyo sajiliwa kwa namba yangu ya nida nisiyo ifahamu.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom