Vodacom wamefungia line yangu ikiwa na milioni 10 kwenye M-PESA

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Wakuu kwema?

Line yangu ya Vodacom inasoma mtandao vizuri lakini haifai kupiga namba yoyote, iwe ya kawaida au Mpesa au kununua vifurushi

Nilipoenda kwenye Vodashop nikidhani kuwa nilifungiwa sababu sikuhakiki namba vizuri

Lakini Vodashop walipoicheki wakasema niliihakiki vizuri na imetokea error tu yaani imefungwa kwa bahati mbaya na nisubiri kwa saa 24 itakuwa imefunguliwa, hiyo ilikuwa ni wiki iliyopita

Saa 24 zilipopita bado ikawa imefungiwa, nikaenda Vodacom makao makuu kuwaelezea

Makao makuu wakaniambia mbona line yako inaonekana imeshafunguliwa? Nikawaonyesha kwa kupiga simu pale kuwa haifai kupiga

Ndipo wakaniambia watashughulikia ndani ya saa 24 itakuwa tayari

Nikasubiri saa 24 zikapita bado ikawa haifai, nikawapigia huduma kwa wateja kupitia namba nyingine, huduma kwa wateja wakasema namba inaonyesha imeshafunguliwa nikate simu niijaribu tena, tukabishana pale maana nilijua haitaweza kupiga

Nikarudi tena makao makuu, wakaniambia wameishughulikia na ndani ya masaa 3 itakuwa tayari, masaa 3 yakipita ikawa haifai kupiga vilevile

Kesho yake nikarudi tena makao makuu nikawaeleza kuwa line haikufaa kupiga na sasa ninachotaka ni kupata hela zangu kwenye M Pesa hata kwa njia nyingine maana sina imani na mifumo yao tena (kumbuka siwezi kuingia M Pesa wala kufanya chochote)

Makao Makuu wakasema haiwezekani kupata hizo hela kwa njia nyingine, ni kupitia menu ya M Pesa tu,
Ila wakaniambia waliofunga line sio wao ni TCRA ila wanaipigania sana na kesho yake (leo) itakuwa tayari, jamaa akanipa na namba yake binafsi nimpigie kama haiatakuwa tayari

Sasa leo line haijawa tayari, na jamaa hapokei Simu

Wakuu hapa nafanyaje, maana hela zimekwama na sina uhakika kama nitazipata lini au ndio zitapotea moja kwa moja

CC Vodacom Tanzania

Soma Mrejesho: Mrejesho wa Vodacom wamefungia line yangu yenye milioni 10 M pesa
 
Back
Top Bottom