MREJESHO; Wa Kaka yangu aliyechanganyikiwa

MREJESHO; Wa Kaka yangu aliyechanganyikiwa

Hapo ndiyo nachanganyikiwa kabisa yaani
Unachanganyikiwa nini? Hii kama hujatunga basi mmepata mganga wa mchongo ...sio kwamba watu hawako wa kuwasaidia ila wakat mwingine uongo uongo mwingi wa humu na usanii utapeli ndio hufanya watu wapite kushoto huku wakisoma.kimya kimya ..Kuna vitu hapo hata havi make sense...eti mwezi wa 6 na 12...wamewaacha muda wote huo
 
Sasa km kukataa ungekataa pale pale kwamba mimi haya mambo siyataki na siyaamini sipo tayari kuyafanya, kuliko kukubari kisha baadae unakataa wakati kule ulishatia saini yako kwamba umekubari huoni km unajitafutia matatizo zaidi?
Nilikuwa nimechanganyikiwa nilishndwa kukataa
 
Unachanganyikiwa nini? Hii kama hujatunga basi mmepata mganga wa mchongo ...sio kwamba watu hawako wa kuwasaidia ila wakat mwingine uongo uongo mwingi wa humu na usanii utapeli ndio hufanya watu wapite kushoto huku wakisoma.kimya kimya ..Kuna vitu hapo hata havi make sense...eti mwezi wa 6 na 12...wamewaacha muda wote huo
Mimi mwenyewe hayo maelezo yamenichanganya mkuu siwezi kutunga haya mambo nimeambiwa mimi jana
 
Wewe utakua una matatizo yako binafsi na hausaidiki sikia hayo makolokolo uliyopewa na huyo mganga yatie kiberiti kisha kaa sikilizia upepo yaan fanya km hujaona kitu vile na usikae unafikiria sijui kaka yangu vile kaka yangu hivi siku sio nyingi utatuletea story ya mama yako na yeye tayari wadudu washamuingia, msijishirikishe kwenye vitu msivyovifahamu kwa kina mwisho wake hua ni majuto tu
Asante mkuu, sitaenda kuoga hiyo dawa kabisa
 
Sasa ushakubari ndio ufanye ulichoambiwa

Nitakupa kisa kimoja, kuna Mzee mmoja alikua anataka Cheo ofisi moja kubwa tu akaenda kwa Sir Ngoma akaomba afanyiwe mambo kweeli akampa vidawa dawa Mzee akaenda kufanya aalivyoambiwa ndani ya muda mambo yakaenda safi akapanda Cheo ghafla, sasa Mzee tamaa ikamuingia akawa anataka Cheo cha juu zaidi yaan hakutosheka na kile Cheo alichopanda akaenda tena Sir Ngoma akaomba afanyiwe utaratibu apande Cheo cha juu zaidi, ukweli Sir Ngoma hakukataa ila aalimwambia ili afikie hicho Cheo kuna sharti gumu inabidi alitekeleze, Mzee bila kujua alipoulizwa yupo tayari akasema yeye anataka Cheo cha Juu zaidi yupo tayari kwa sharti lolote basi Bwana Sir Ngoma akampa Sharti gumu, Mzee akaondoka kwenda kumsimulia mkewe mkewe akalifikiria lile sharti ila sababu na yeye alikua anataka mumewe awe na Cheo cha juu akakubari, shida ikaja kwenye kulitekeleza hilo sharti, hapo ndipo walipoisha wote yaan kizazi chake chote kuanzia yeye mkewe na watoto wake wote ninapoongea sasa wote ni marehemu na hio siri alikuja kuisema mkewe kabla hajafa maana yeye mkewe ndie aliekua wa mwisho kufa
Duh! Mbona hii ni hatari sana aisee, ila mimi sijakabidhiwa chochote wala sijaoga hayo maji ya madawa kabisa
 
Huyo mganga atawapiga hela na kuwagombanisha ukooo na ndugu zenu mpaka mchoke wenyewe.

Utasikia shangazi yake kamroga, ama mama mkubwa ndie kamroga, ama ndugu fulani kamroga

Note : huyo mganga hatawaomba hela cash atawapiga hela kupitia vifaa na dawa, atawaelekeza maduka ya kununua dawa ambayo kuna matapeli wenzake.
Inaonyesha na wewe muhanga, iliwahi kukutokea?
 
Back
Top Bottom