Mrejesho: Nimefanya sana umalaya, sasa basi

Niliwahi kuleta thread yangu humu ndani nikielezea juu ya maisha yangu na vitu ambavyo nilivifanya katika maisha yangu kwa kuwa maisha yangu ya nyuma yaligubikwa na dhambi na vitendo vichafu=>Confession: Nimefanya sana umalaya, sasa basi

Namshukuru sana MUNGU kwa kweli nimepiga hatua kubwa sana katika maisha yangu; Ilinibidi kuhamia mkoa mwingine kabisa, na kuanza kazi sehemu nyingine ili niweze kuanza upya. Sasa hivi nimekuwa mtu mpya kabisa.

Nawashukuru sana watu wote humu ndani hasa wale ambao walinishauri na hata kunitumia PM za kunipa ushauri na kunipa moyo. Pia nawashukuru hata wale ambao walinitukana na kunikejeli.

Namshukuru sana pia kwa namna ya pekee mtaalamu wa Saikolojia ambae amenisaidia sana kufika hapa nilipo, na sasa hivi nasonga mbele, siangalii nyuma tena.

Ahsanteni sana na mbarikiwe sana na Mwenyezi MUNGU.

JF imenisaidia sana kwa kweli.
Hongera lakini kumbuka kusali sana sana kulingana na imani ulonayo,shetani hua anatafuta sana wale walomdhalilisha kwa kumrudia MUNGU awaangushe upya
 
Ahsante sana mtu wa Mungu. Ubarikiwe sana.
 
Nawewe unataka kuwa malaya mstaafu?
Kustaafu kuna retirement package ujue, inakuwa package nzuri zaidi kama ndani ya mwezi umalaya unafutika na kusahaulika na ninapata kazi mpya, mitaa mpya kila kitu kipya. Mi mwenyewe ningetemana na ishu zangu chafu chafu like yesterday
 
Naomba usome thread yangu ya kwanza mpendwa, ili uelewe vizuri context ya huu uzi.
Hakuna haja ya kuwa harsh; kwako its just a story, lakini kwangu ni reality. Ubarikiwe sana.
 
Nipe number yako ya simu ili nikumbee mm mchngaji.....
 
Sio upo ktk mchakato na upembuzi yakinifu wa kuanzisha kanisa lako?
 
Hahaha yaani kwa mwezi mmoja toka ufanye maamuzi 'magumu' hadi leo umeshahama mkoa, ukapata kazi, na kushukuru Mungu? Kweli maisha ya sasa zaidi ya bongo movies
Niliwahi kuleta thread yangu humu ndani nikielezea juu ya maisha yangu na vitu ambavyo nilivifanya katika maisha yangu kwa kuwa maisha yangu ya nyuma yaligubikwa na dhambi na vitendo vichafu=>Confession: Nimefanya sana umalaya, sasa basi

Namshukuru sana MUNGU kwa kweli nimepiga hatua kubwa sana katika maisha yangu; Ilinibidi kuhamia mkoa mwingine kabisa, na kuanza kazi sehemu nyingine ili niweze kuanza upya. Sasa hivi nimekuwa mtu mpya kabisa.

Nawashukuru sana watu wote humu ndani hasa wale ambao walinishauri na hata kunitumia PM za kunipa ushauri na kunipa moyo. Pia nawashukuru hata wale ambao walinitukana na kunikejeli.

Namshukuru sana pia kwa namna ya pekee mtaalamu wa Saikolojia ambae amenisaidia sana kufika hapa nilipo, na sasa hivi nasonga mbele, siangalii nyuma tena.

Ahsanteni sana na mbarikiwe sana na Mwenyezi MUNGU.

JF imenisaidia sana kwa kweli.
 
Hongera sana. Na ss wafanya nini.
Mwezi mmoja kurecover trauma za umalaya kipsychologia ni ngumu. Ila pia kwa sala yawezekana.
Endelea kidogo kututhreadisha, kama unania ya kutoa shule ili wengine tukufuate.
 
Kuna watu Dunia hii tuiishiyo mambo yao ni chap chap, umekuja hapa na uzi tarehe 2/4/2016 leo mambo yashakunyookea yanaenda bam bam. Itabidi utupe siri ya urembo ili na sisi tujibadili chap chap.
Watu hawafanani Angry Bird
Wengine inawachukua wiki tu kubadilika
 
Utukufu kwa Bwana!
Kata minyororo yote ya shetani sasa.
 
Back
Top Bottom