Mrejesho: Nimefanya sana umalaya, sasa basi

Neemababy

Senior Member
Apr 1, 2016
118
166
Niliwahi kuleta thread yangu humu ndani nikielezea juu ya maisha yangu na vitu ambavyo nilivifanya katika maisha yangu kwa kuwa maisha yangu ya nyuma yaligubikwa na dhambi na vitendo vichafu=>Confession: Nimefanya sana umalaya, sasa basi

Namshukuru sana MUNGU kwa kweli nimepiga hatua kubwa sana katika maisha yangu; Ilinibidi kuhamia mkoa mwingine kabisa, na kuanza kazi sehemu nyingine ili niweze kuanza upya. Sasa hivi nimekuwa mtu mpya kabisa.

Nawashukuru sana watu wote humu ndani hasa wale ambao walinishauri na hata kunitumia PM za kunipa ushauri na kunipa moyo. Pia nawashukuru hata wale ambao walinitukana na kunikejeli.

Namshukuru sana pia kwa namna ya pekee mtaalamu wa Saikolojia ambae amenisaidia sana kufika hapa nilipo, na sasa hivi nasonga mbele, siangalii nyuma tena.

Ahsanteni sana na mbarikiwe sana na Mwenyezi MUNGU.

JamiiForums imenisaidia sana kwa kweli.

UPDATES ZAIDI (SEPT 2016)
Nazidi kuendelea vizuri sana kwa kweli, namshukuru Mungu kwa yote. Sasa hivi maisha yanaendelea vizuri tuu, nimesahau yote ya nyuma; Bado naendelea na sessions za counselling hadi sasa hivi, pia naendelea na kazi na kwa kiasi kikubwa sana nimeweza kuanza maisha mapya, maisha ya kuishi kwa kadri ya uwezo wangu na maisha ya kuwa na hofu ya Mungu. Naomba Mwenyezi Mungu muweza wa yote azidi kunipa nguvu na kunifanya niendelee kusimama.

Nawashukuru watu wote humu ndani kwa namna ya pekee (hata wale ambao walinikejeli na kunitusi); mmenifundisha jambo kubwa sana wapendwa.
 
Back
Top Bottom