Hypersonic
JF-Expert Member
- Apr 14, 2012
- 612
- 1,131
Kama nilivoahidi kuwa leo Jumatatu tarehe 26/02/2024 naanza mchakato wa kuwashitaki hawa watu.
Nimeanzia TCRA ambako nimepeleka malalamiko yangu, Majibu ya TCRA ni kwamba wao hawahusiki kwa sababu hasimamii watu bali wabasimamia makampuni ya mawasiliano. Hii kidogo imeshitua hivo ikabidi niende polisi, Majibu ya polisi ni kwamba nikamshauri mkopaji alipe kwanza alafu yeye ndo afungue mashitaka.
Nimeamua kubadilisha kesi na nimefungua kesi ya kutukwana na kudhalilishwa kwa njia mtandao kwa wale niliofanikiwa kuwarekodi.
Ahadi ya polisi ni kwamba wanatrack namba wakishawapata wahusika watawakamata na baada ya hapo ndo tutaendelea mbele.
Ugumu wa kesi ni kuthibitisha pasipo shaka kuwa kweli ile sauti ni ya mhusika pindi akiwa mahakamani.
Ni nini cha kufanya:- Bado sijakamata tamaa narudisha mpira kwa kipa kwa maana ya kushirikiana na wanasheria ili nishitaki ama TCRA au Kampuni ya mtandao husika kwa kushindwa kulinda faragha yangu nikiwa kama mteja ambaye wanawajibu wa kulinda taarifa zangu.

TCRA mmeamua kuuza utu wetu kwa wahuni? {APP za mikopo mtandaoni.}
Ndugu wanajamvi, Asalaam Aleikhum. Kama kichwa cha habari kilivo hapo juu nimejikuta na kuwa mhanga wa hawa matepeli wa APP za mitandaoni. Iko hivi kuna mtu ambaye ninafahamiana naye ama ni mtu wangu wa karibu ktk familia, kwa utashi wake binfasi alikopa kwa hawa jamaa, alikopa lini na kiasi...
www.jamiiforums.com