Kushamiri kwa online App za mikopo

sitagliptin

JF-Expert Member
Mar 10, 2023
1,080
2,308
Habari wanandugu na wageni na wenyeji wa JamiiForums hakika Mungu aendelee kumbariki mwashishi wa hii kitu

Nivumiliwe tu sio mtaalamu wa kuandika sana ila najua sana kusoma waliachoandika waandisho manguli
baada ya pukurukushani za wiki nzima angalau nchi imechangamka na mengi kuanzia michezoni mpaka kwenye siasa Niende kwenye mada moja kwa moja bila kupoteza muda wako, kama kichwa kinavyojieleza.

Hivi karibuni kumezuka matangazo ya mtandaoni na hata mitaani ya huduma za mikopo kwa riba nafuu mfano kuna pesa x kuna wale wa cash x nk ukingia YouTube, Instagram, Facebook na hata mtandao wa X

Binafsi mwanzo nilikuwa nahisi pengine ni matapeli ko sikuwahi jishughurisha nao hataa ila majuzi baada ya kuona vijana kadhaa mtaani kwangu wakiinadi kwa bashasha pesa x ikabidi niwaze sana je kuna ukweli (Samahani makampuni nayo yataja siyataji kama sehemu ya matangazo au kuyatangaza)

Buana buana ikabid nijaribu moja wapo nikaipakua na kujaza kama wanavyohitaji ikiwa ni pamoja na kitambulisho cha uraia, kweli dakika chache nikakamilisha na kuomba mkopo nikapewa 25000 cash kupitia mpesa

Baada ya hapo nikaanza kupata adds nyingi za kuhusiana na mikopo na hapo ndipo nikanza kujiuliza haya ambayo yamefanya nije hapa kuandika kwa kuuliza kwanza nataman kujua haya nakampuni ni ya nchi gani na je bank kuu wanataarifa za kutosha kuhusu uwepo wake? Pili hawa wamiliki pesa hizi ni halali kweli au

Mawazo yangu binafs yamenipeleka kuwaza huenda wamiliki wakubwa ni viongozi wetu wakubwa ma hapa tunahitaji Bank Kuu BOT ichunguze kwa umakini uwepo wake na uhalali wake sambamba na kujua wamiliki wake halisi isijekuwa kuna utakatishaji wa fedha za umma iwe tz, kenya au popote kwa sababu jamaa wanatoa hela kama njugu afu bila wasiwasi

Pia polis wangalie nao kwa upande wao usalama wa watu wake ambao watashindwa kurejesha manake tunakopeshwa na mtu ambaye hatumuoni tumaelekea mwaka wa uchaguzi isijekuwa pesa chafu ndio zinaandaliwa njia yake. Bank kuu, Polisi Tanzania.

Asante msinitukane sana uandishi wangu hata mi mwenyewe haunivutii kabisa ila najikaza tu
 
Hujakamilisha story yako vizuri... baada ya kupata huo mkopo wa 25,000 marejesho yamekuwaje? Unatakiwa kurudisha shs ngapi kwa muda gani nk?
 
Tumia tu akili yako kuchuja serikali haisaidii kila kitu.

DECI watu walilizwa..

Q-Net watu walilizwa.

Juzi wamekuja wa kununua nyoka ,kenge kwa 600k tukawatahadharisha watu haikuchukua muda wakalizwa tena.

Na ponzi scheme nyingi na mikopo ya utapeli kibao.

Scam is everywhere..jiridhishe vizuri

Kumbuka "CHEAP IS EXPENSIVE"
 
Hujakamilisha story yako vizuri... baada ya kupata huo mkopo wa 25,000 marejesho yamekuwaje? Unatakiwa kurudisha shs ngapi kwa muda gani nk?
Hapo unapata 23,400/- bado makato ya kutolea. Marejesho ni 37,000/- baada ya siku 8. Ikifika siku ya 7 wanaanza kukupigia simu.
 
Habari wanandugu na wageni na wenyeji wa Jamii forum hakika Mungu aendelee kumbariki mwashishi wa hii kitu

nivumiliwe tu sio mtaalamu wa kuandika sana ila najua sana kusoma waliachoandika waandisho manguli

tunaishi afu tunaishia
Dhamana ya huo mkopo ni hiyo smart phone Yako na wala sio kitambulisho chako kama unavyodhani, katika masharti uliyokubali ni pamoja na kuweka dhamana ya simu Yako hiyo IMEI number za simu wamechekua ulishindwa kulipa wanazima simu hiyo mpaka utakapolipa
 
Hii mikopo unapigiwa simu kuwa kuna mtu kakuweka kama mdhamini ambacho hawakuconfirm na mimi wakati hizo details zinajazwa yaani ni uhuni uhuni.

Nadhani ni biashara nzuri lakini inahitaji usimamizi mkubwa lasivyo money laundaring haitatuacha
 
Dhamana ya huo mkopo ni hiyo smart phone Yako na wala sio kitambulisho chako kama unavyodhani, katika masharti uliyokubali ni pamoja na kuweka dhamana ya simu Yako hiyo IMEI number za simu wamechekua ulishindwa kulipa wanazima simu hiyo mpaka utakapolipa
Sio kweli
 
Habari wanandugu na wageni na wenyeji wa Jamii forum hakika Mungu aendelee kumbariki mwashishi wa hii kitu

nivumiliwe tu sio mtaalamu wa kuandika sana ila najua sana kusoma waliachoandika waandisho manguli

simba uongozi haufai

tunaishi afu tunaishia
Crypto currency
 
Dhamana ya huo mkopo ni hiyo smart phone Yako na wala sio kitambulisho chako kama unavyodhani, katika masharti uliyokubali ni pamoja na kuweka dhamana ya simu Yako hiyo IMEI number za simu wamechekua ulishindwa kulipa wanazima simu hiyo mpaka utakapolipa
Toka Lini wakafanya Hivyo Buana acha kutishia watu hawana huo ubavu
 
Back
Top Bottom