Mpira ni nini? Kama ni pesa, mbona Marekani wanazo na hawajawahi kutwaa kombe la dunia? Kama ni vipaji, mbona vimejaa Afrika na hatufanyi maajabu?

Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Mpira ni nini? Kama ni pesa, mbona Marekani wanazo na hawajawahi kutwaa kombe la dunia? Kama ni vipaji, mbona vimeja sana Afrika na hatufanyi maajabu?

View attachment 1645695

Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanaume ya Marekani imecheza fainali kadhaa za Kombe la Dunia.

Matokeo yao mazuri yalitokea wakati wa kuibuka kwao kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia la mwaka 1930, wakati Marekani ilipomaliza katika nafasi ya tatu.

Baada ya Kombe la Dunia la mwaka 1950, ambapo Marekani iliivuruga timu ya Uingereza katika mechi ya makundi kwa ushindi wa 1-0.

Marekani haikuwepo kwenye mashindano hayo mpaka mwaka 1990. Marekani ilishiriki kila Kombe la Dunia tangu mwaka 1990 hadi mwaka 2014, lakini hawakufuzu mashindano ya 2018 kwa mara ya kwanza tangu 1986 baada ya kupoteza kwa Trinidad na Tobago.

HAYA NDIO MAFANIKIO YA KANDANDA KWA NCHI ZA AFRIKA

(1) Cameroon (1990), Senegal (2002) na Ghana (2010) ndio timu pekee kutoka katika bara la Afrika kufika hatua ya robo fainali katika michuano ya kombe la dunia la FIFA.

(2) Cameroon imecheza mechi nyingi kama team ya Afrika katika historia ya kombe la dunia. Imecheza mechi 23.

View attachment 1645697

(3) Nigeria ndio team iliyoshinda mechi nyingi katika kombe la dunia la FIFA kwa kushinda jumla ya mechi 6.

(4) Hao hao Nigeria (The Super Eagles) pia wanashikilia rekodi ya kushinda magoli mengi (Magoli 23) kwa timu za bara la afrika.

(5) Mchezaji Abdul Rahman Fawzi ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka Afrika kushida katika mashindano haya ya kombe la dunia dhidi ya nchi ya Hungary mwaka 1934.

(6)Morocco ndio timu ya kwanza ya Afrika kupata "point" baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi na Bulgaria mwaka 1970.

(7) Tunisia ndio nchi ya kwanza ya Afrika kushinda mechi ya kombe la dunia baada ya kuwafunga Mexico 3-1 mwaka 1978.

(8) Morocco ndio timu ya kwanza kutoka Afrika kuvuka raundi ya kwanza na kufika raundi ya 16 bora mnamo mwaka 1978.

Je, mpira ni pesa au kipaji? Mbona umewashinda wote matajiri (U.S.A) pamoja na masikini (Afrika)?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Marekani tuna mpira wetu American Football.

Hiyo soccer kwa kiasi kikubwa wanacheza wanawake na wahamiaji huku.

The United States women's national soccer team represents the United States in international women's soccer. The team is the most successful in international women's soccer, winning four Women's World Cup titles, four Olympic gold medals, and eight CONCACAF Gold Cups.
 
Marekani tuna mpira wetu American Football.
Huo mnaouita mpira wenu ni kwa sababu mmeuweza ila huu wa soccer la wanaume sio wenu kwa sababu umewashinda. Mambo ya sungura "sizitaki mbichi hizi".

Kama soccer sio kipaumbele cha USA, why do they maintain men's national team?...
 
USA hawapendi mpira, nafatiliaga sana comment zao kwenye page ya espn, ikipostiwa habari ya mpira wanaponda sana, wanaita 'boring sport' na ni mchezo wa maskini
Kwa hiyo hao wachache wa huko ESPN ndio unachukulia kuwa wamarekani wote hawapendi soccer?
 
Hiyo soccer kwa kiasi kikubwa wanacheza wanawake na wahamiaji huku.
Kitendo cha kuwa na timu ya taifa ya soccer ya wanaume ni kwamba wanatamani kupata mafanikio hayo ila mchezo umewakataa ndio maana wanalialia na kutoa justifications za kitoto eti "sio kipaumbele chao"...
 
Siyo priority, ni kama badminton.

Hivi ndivyo Wamarekani wengi wanavyoikejeli soccer.

Hii ni kutoka movie "Coming To America", walikuwa wanaangalia basketball.

Halafu wamarekani mpira wa miguu wanaita 'soccer' ni kama jina la kejeli, mchezo wao ule wa kijinga unaofanana na Rugby ndo wanauita football 'American Football', yaani wale watu ni kama wanaishi kwenye dunia yao. Kuna siku niliona Will Smith amepost kwenye page yake jinsi alivyokutana na Neymar na akamtag, chini kwenye comment section kulijaa maswali 'who is that?', wengi wakawa wanashangaa mtu gani huyu mbona ana followers wengi sana halafu hawamjui
 
The United States women's national soccer team represents the United States in international women's soccer. The team is the most successful in international women's soccer, winning four Women's World Cup titles, four Olympic gold medals, and eight CONCACAF Gold Cups.
This thread is all about men's soccer bro.
 
This thread is all about men's soccer bro.
Mimi nakueleza na kukufafanulia kwamba US soccer ni mchezo wa wahamiaji na wanawake.

Wamarekani wanaume wengi wanacheza American Football na Basketball.

Hawana interest na Soccer.

Sasa kuwauliza kwa nini hawafanyi vizuri katika mchezo ambao hawana interest nao ni kuwaonea.

Marekani walimleta mpaka Pele acheze soccer New York ili aongeze interest, akashindwa kuongeza interest ya watu.

Sasa kama watu hawaupendi mchezo wenu, usiwalazimishe waupende.

Wao wana michezo yao.

Wamarekani wanaume waongeleshe habari za Basketball, American Football na Baseball.

Ukiwaongelesha soccer hapo hapo utasikia "Where are you from?".

Wanajua tayari wewe immigrant.
 
Mpira ni Kipaji na Adabu ambavyo mchezaji huanza kuandaliwa tangu akiwa mdogo. Mtoa mada nikuulize pia na wewe pengine tutakutana katikati.

Nchi za Kiafrika sana zimewekeza katika Fani zipi za Michezo!?
 
Mimi nakueleza na kukufafanulia kwamba US soccer ni mchezo wa wahamiaji na wanawake.

Wamarekani wanaume wengi wanacheza American Football na Basketball.

Hawana interest na Soccer.

Sasa kuwauliza kwa nini hawafanyi vizuri katika mchezo ambao hawana interest nao ni kuwaonea.
Mkuu, nimehoji kuhusiana na soka kwa sababu ndio mchezo number moja duniani. Kwa hiyo hata kama Marekani hawaupendi hiyo haiondoi ukweli kwa kandanda ndio mchezo wenye mashabiki wote kuzidi hizo baseball na american football...
 
Namba moja duniani lakini si namba moja Marekani.

Sasa unalazimisha mtu awe mahiri katika mchezo asioupenda?

Unavyokwenda unaweza kuingia shughuli ya Waislamu Msikitini halafu ukawauliza kwa nini pilau lao halina nyama ya kitimoto.

Kwa sababu nyama ya kitimoto inapendwa sana duniani.

Marekani ni nchi tofauti. Wanapenda kuwa tofauti. Wana kitu wanakiita "American Exceptionalism".Wamekataa kutumia metric system mpaka leo. Si lazima wafuate mfumo unaofuatwa na dunia yote.

Dunia yote karibu wanatumia kilometers na meters, Marekani wanatumia miles na inches.

Wamarekani walitaka kupingana na wakoloni wao Waingereza.

Wakoloni wao Waingereza wanakunywa chai, Wamarekani wamekataa kunywa chai, wanakunywa kahawa.

Wakoloni wao Waingereza wanaendesha gari kushoto, Wamarekani wanaendesha kulia.

Wakoloni wao Waingereza tai zao stripes zake zinaenda upande mmoja, tai za Wamarekani stripes zinaenda upande tofauti.

Wakoloni wao Waingereza wanapenda Soccer, Wamarekani wanapenda American Football na Basketball.

Sasa usipoelewa haya mambo kihistoria unaweza kuhoji kama Wamarekani hawawezi Soccer, kumbe wenzako wamekataa mchezo wa Wakoloni wao, wameanzisha michezo yao tofauti.

Wewe usiyeweza kuanzisha michezo yako na kuifanya ipendwe na watu wako, endelea tu kuwa koloni la Muingereza kiutamaduni.
 
Wewe pia ni lazima uelewe kwamba wao ndio wenye pesa nyingi hapa duniani...
Elewa kuwa kuna kiwango cha pesa mkifikia mnakuwa mnauwezo wa kufanya chochote, nini ambacho marekani ana uwezo wa kufanya kwenye soka ambacho uk hawezi fanya kisa kazidiwa pesa?
 
Mimi nakueleza na kukufafanulia kwamba US soccer ni mchezo wa wahamiaji na wanawake.

Wamarekani wanaume wengi wanacheza American Football na Basketball.

Hawana interest na Soccer.

Sasa kuwauliza kwa nini hawafanyi vizuri katika mchezo ambao hawana interest nao ni kuwaonea.

Marekani walimleta mpaka Pele acheze soccer New York ili aongeze interest, akashindwa kuongeza interest ya watu.

Sasa kama watu hawaupendi mchezo wenu, usiwalazimishe waupende.

Wao wana michezo yao.

Wamarekani wanaume waongeleshe habari za Basketball, American Football na Baseball.

Ukiwaongelesha soccer hapo hapo utasikia "Where are you from?".

Wanajua tayari wewe immigrant.
Walimpeleka mpaka Ngasa ili anogeshe mambo kwa kukipiga na Man u, lakini wapi
 
Back
Top Bottom