Mpira ni nini? Kama ni pesa, mbona Marekani wanazo na hawajawahi kutwaa kombe la dunia? Kama ni vipaji, mbona vimejaa Afrika na hatufanyi maajabu?

Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu Jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Mpira ni nini? Kama ni pesa, mbona Marekani wanazo na hawajawahi kutwaa kombe la dunia? Kama ni vipaji, mbona vimeja sana Afrika na hatufanyi maajabu?

View attachment 1645695

Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanaume ya Marekani imecheza fainali kadhaa za Kombe la Dunia.

Matokeo yao mazuri yalitokea wakati wa kuibuka kwao kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia la mwaka 1930, wakati Marekani ilipomaliza katika nafasi ya tatu.

Baada ya Kombe la Dunia la mwaka 1950, ambapo Marekani iliivuruga timu ya Uingereza katika mechi ya makundi kwa ushindi wa 1-0.

Marekani haikuwepo kwenye mashindano hayo mpaka mwaka 1990. Marekani ilishiriki kila Kombe la Dunia tangu mwaka 1990 hadi mwaka 2014, lakini hawakufuzu mashindano ya 2018 kwa mara ya kwanza tangu 1986 baada ya kupoteza kwa Trinidad na Tobago.

HAYA NDIO MAFANIKIO YA KANDANDA KWA NCHI ZA AFRIKA

(1) Cameroon (1990), Senegal (2002) na Ghana (2010) ndio timu pekee kutoka katika bara la Afrika kufika hatua ya robo fainali katika michuano ya kombe la dunia la FIFA.

(2) Cameroon imecheza mechi nyingi kama team ya Afrika katika historia ya kombe la dunia. Imecheza mechi 23.

View attachment 1645697

(3) Nigeria ndio team iliyoshinda mechi nyingi katika kombe la dunia la FIFA kwa kushinda jumla ya mechi 6.

(4) Hao hao Nigeria (The Super Eagles) pia wanashikilia rekodi ya kushinda magoli mengi (Magoli 23) kwa timu za bara la Afrika.

(5) Mchezaji Abdul Rahman Fawzi ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka Afrika kushida katika mashindano haya ya kombe la dunia dhidi ya nchi ya Hungary mwaka 1934.

(6)Morocco ndio timu ya kwanza ya Afrika kupata "point" baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi na Bulgaria mwaka 1970.

(7) Tunisia ndio nchi ya kwanza ya Afrika kushinda mechi ya kombe la dunia baada ya kuwafunga Mexico 3-1 mwaka 1978.

(8) Morocco ndio timu ya kwanza kutoka Afrika kuvuka raundi ya kwanza na kufika raundi ya 16 bora mnamo mwaka 1978.

Mpira ni nini? Pesa au vipaji? Mbona umewashinda wote matajiri (U.S.A) pamoja na masikini (Afrika)?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
soccer is all about ability + chance
 
Back
Top Bottom