Mpira ni nini? Kama ni pesa, mbona Marekani wanazo na hawajawahi kutwaa kombe la dunia? Kama ni vipaji, mbona vimejaa Afrika na hatufanyi maajabu?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu Jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Mpira ni nini? Kama ni pesa, mbona Marekani wanazo na hawajawahi kutwaa kombe la dunia? Kama ni vipaji, mbona vimeja sana Afrika na hatufanyi maajabu?

images (8).jpg


Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanaume ya Marekani imecheza fainali kadhaa za Kombe la Dunia.

Matokeo yao mazuri yalitokea wakati wa kuibuka kwao kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia la mwaka 1930, wakati Marekani ilipomaliza katika nafasi ya tatu.

Baada ya Kombe la Dunia la mwaka 1950, ambapo Marekani iliivuruga timu ya Uingereza katika mechi ya makundi kwa ushindi wa 1-0.

Marekani haikuwepo kwenye mashindano hayo mpaka mwaka 1990. Marekani ilishiriki kila Kombe la Dunia tangu mwaka 1990 hadi mwaka 2014, lakini hawakufuzu mashindano ya 2018 kwa mara ya kwanza tangu 1986 baada ya kupoteza kwa Trinidad na Tobago.

HAYA NDIO MAFANIKIO YA KANDANDA KWA NCHI ZA AFRIKA

(1) Cameroon (1990), Senegal (2002) na Ghana (2010) ndio timu pekee kutoka katika bara la Afrika kufika hatua ya robo fainali katika michuano ya kombe la dunia la FIFA.

(2) Cameroon imecheza mechi nyingi kama team ya Afrika katika historia ya kombe la dunia. Imecheza mechi 23.

images (9).jpg


(3) Nigeria ndio team iliyoshinda mechi nyingi katika kombe la dunia la FIFA kwa kushinda jumla ya mechi 6.

(4) Hao hao Nigeria (The Super Eagles) pia wanashikilia rekodi ya kushinda magoli mengi (Magoli 23) kwa timu za bara la Afrika.

(5) Mchezaji Abdul Rahman Fawzi ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka Afrika kushida katika mashindano haya ya kombe la dunia dhidi ya nchi ya Hungary mwaka 1934.

(6)Morocco ndio timu ya kwanza ya Afrika kupata "point" baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi na Bulgaria mwaka 1970.

(7) Tunisia ndio nchi ya kwanza ya Afrika kushinda mechi ya kombe la dunia baada ya kuwafunga Mexico 3-1 mwaka 1978.

(8) Morocco ndio timu ya kwanza kutoka Afrika kuvuka raundi ya kwanza na kufika raundi ya 16 bora mnamo mwaka 1978.

Mpira ni nini? Pesa au vipaji? Mbona umewashinda wote matajiri (U.S.A) pamoja na masikini (Afrika)?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Marekani mpira hauna influence kubwa kwa watu na wala hawaupendi that's why hawafanikiwi kule kuna michezo yao pendwa kama basket ball mieleka music

Afrika tunakosa uingozi bora na pesa kumbuka kuna timu nyingi za Afrika wanagoma kucheza katika kombe kisa hawajalipwa pesa mfano Nigeria 2014
 
Mpira ni utamaduni lazima uwe damuni na kuwa sehemu ya maisha hapo ndo utaona matokeo chanya......... Cricket ni sehemu ya maisha na utamaduni wa India, Pakistan, England, South Afrika na Zimbabwe kama ilivyo Basketball Marekani vivyo hivyo kama uchawi ulivyo sehemu ya maisha yetu kwa hiyo mkuu mpira sio hela kama unavyodhani angalia mchina anavyohustle kutengeneza huo utamaduni hadi ananunua wachezaji kwa bei za kutupwa
 
Mpira ni utamaduni lazima uwe damuni na kuwa sehemu ya maisha hapo ndo utaona matokeo chanya.........Cricket ni sehemu ya maisha na utamaduni wa India, Pakistan ,England ,South Africa na Zimbabwe kama ilivyo Basketball Marekani
Umejitahidi sana kufafanua mkuu...
 
Ukienda brazil watu wanapiga ball mpaka chooni we unazan watakuwa sawa na kina juma kaseja wachezaji ambao wanacheza mpira ili tu waendeshe maisha yao na mpira sio damu yao ukiiangalia brazil na mwaka 2002 pale korea au spain ya 2010 ndio utajua km wale jamaa walizaliwa na mpira toka tumbon watu wanapiga pasi kali kila ataeshika mpira ni kesi hakuna mzembe ata mmoja
 
Mpira ni zali tu ,unaweza ukawa na team yenye pesa,vipajj ,uongozi mzuri kisha ukafungwa na team ambayo wachezaji wake hata danadan hawawezi.Mifano ni mingi tu huko ulaya tunajionea kuanzia team za taifa mpka Club.
Mancity oyeeee
PSg oyeeeee
Madrid oyeee
Man u oyeee
 
Mpira ni zali tu ,unaweza ukawa na team yenye pesa,vipajj ,uongozi mzuri kisha ukafungwa na team ambayo wachezaji wake hata danadan hawawezi.
Hilo zali wamelikosa nchi za Afrika na Marekani pekee mkuu...
 
Mpira ni utamaduni ambao umejengwa moyoni,hauna uhusiano wowote na hela,nguvu za kiuchumi,ubabe wala udikteta
 
  • Thanks
Reactions: Auz
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom