Mpinzani wa JK apeta TUCTA

hawa wabunge ni wawakilishi wa kundi la wafanyakazi walio wanachama wa CCM.inanipa shida kidogo ikiwa na Chadema nao watakuwa na wawakilishi wa wafanyakazi katika wabunge wao wa kuteuliwa! Ningependa wabunge wa kuteuliwa kupitia chama cha wafanyakazi wasiwe affiliated na chama chochote ili wawe independent!

Ni sahihi kwa TUCTA kuwakataa hao wabunge wa CCM maana hawajatokana na mchakato ndani ya TUCTA bali na mchakato nadani ya CCM.

Comments nyingi ni sahihi, lakini am interested na hii kuhusu uwepo wa waziri na riz1 to facilitate anti Mgaya vote,

my consern is how we associate the son of president in our Tz politics as well as business sector.

i think he should use his position as well as his carrier to initiate maendeleo ya jamii by having an organisation, this is the best way to use a president son position as opposed to the kind of lifestyle people always associate him with kama kwenye ilivyoonekana kwenye hiyo comment na nyinginezo ambazo kila siku tunakutana nazo

CANT MAKE HEAD OR TAIL OF WHAT YOU ARE SAYING MR "intellectual" CAN YOU REWRITE YOUR THREAD IN SWAHILI OR SOME OTHER LANGUAGE YOU FEEL COMFOTABLE WITH.

tuko pamoja Mgaya tunakuaminia sasa anza kazi ilikuondoa hizi kero hasa za viongozi wa serikali yetu inayotufanya wafanya kazi kama hatuna akili huku wao wakijilimbikizia madaraka ,mali , etc

Mpinzani wa JK apeta TUCTA
• Wabunge wa CCM watimuliwa

na Grace Macha

ALIYEKUWA Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA), Nicholaus Mgaya, amechaguliwa kwa kura nyingi kuwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, huku akiahidi kufanya maamuzi magumu katika kudai haki za wafanyakazi, ikiwemo kuendesha migomo.

Mgaya ambaye taarifa za awali zinaonyesha kuwa zilitumika nguvu kubwa kujaribu kumzuia asiibuke mshindi ndiye kiongozi pekee aliyeshambuliwa vikali na Rais Jakaya Kikwete baada ya chama hicho kutishia kuhamasisha wafanyakazi wasimpigie kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Akizungumza na walioitwa wazee wa jiji la Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Kikwete aliyeambatana na wakuu wote wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini, alimshambulia vikali Mgaya kiasi cha kufikia kutoa kauli ya kutozitaka kura za wafanyakazi.
Katika uchaguzi huo wa aina yake, Mgaya alipata kura 324 akiwaacha mbali wagombea wenzake James Mnyeti aliyepata 24 na Honoratha Chitanda aliyeambulia kura 28.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uchaguzi huo, Mgaya alisema kazi yao kubwa ni kujadiliana na serikali kutatua madai ya msingi ya wafanyakazi, lakini kama njia hiyo itashindikana, atahamasisha na kusimamia migongo nchi nzima hadi kieleweke.
Alisema atahakikisha anasimamia kikamilifu kutafuta ufumbuzi wa kero za wafanyakazi, hususan kupunguza kiwango kikubwa cha kodi inayotozwa kwenye mishahara ya wafanyakazi ambayo pia ni midogo kwani haiendani na hali halisi ya maisha.
Alisema kuwa watashughulikia tatizo la mafao madogo yanayotolewa na mifuko ya jamii kwa wafanyakazi wanaostaafu hali inayowafanya waishi maisha ya mateso baada ya kumaliza utumishi.
Aidha katibu huyo alisema watapigania mabadiliko ya Katiba ili iweze kuwanufaisha zaidi wafanyakazi.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha wajumbe kutoka vyama 13 vya wafanyakazi hapa nchini, Omary Juma alifanikiwa kutetea nafasi yake ya urais wa shirikisho hilo katika uchaguzi huo uliokuwa na kila aina ya ushindani ambao ulilazimika kwisha usiku wa manane.
Nafasi ya makamu wa rais wa shirikisho hilo ilichukuliwa na Nortburga Masikini aliyepata kura 180 akimwangusha Dk. Diwani Mrutu aliyepata kura 126.
Nafasi ya naibu katibu mkuu ilichukuliwa na Ezron Kaaya aliyepata kura 212 akiwaacha kwa mbali Salma Chande aliyepata kura 84 na Mchafu Chakomu kura 39 na James Kalanje alifanikiwa kutetea nafasi yake ya uweka hazina kwa kupata kura 243.
Waliochaguliwa kuwa wadhamini wa Tucta na kura zao kwenye mabano ni Charles Mngodo (76 ) , Rehema Mlongelakweli (84), Cecilia Mpamila( 84) na Clement Mswanyama (71).
Nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya wanawake imekwenda kwa Asia Kapori na katibu wake ni Zainabu Matavale.
Wabunge wa CCM watimuliwa
Katika hatua nyingine wabunge wawili wa viti maalum (CCM), Zainab Kawawa na Angellah Kairuki, wamezuiwa kuhudhuria mkutano mkuu wa shirikisho hilo kwa vile hawatambuliwi.
Mgaya alisema TUCTA haiwatambui wabunge hao wa viti maalum walioingia bungeni kwa mgongo wa uwakilishi wa shirikisho hilo kwani hawakutoka ndani ya shirikisho hilo.

mh mgaya ajiandae kama mwenzake wa tra..

tuko pamoja Mgaya tunakuaminia sasa anza kazi ilikuondoa hizi kero hasa za viongozi wa serikali yetu inayotufanya wafanya kazi kama hatuna akili huku wao wakijilimbikizia madaraka ,mali , etc
sema uko pamoja na mgaya..mvunjaji amni mwenzako.

Mpinzani wa JK alikuwa Slaa akapigwa chini mbaya kabisa...hadi leo anaweweseka na huyu lini kagombea urais wa URT?

Hoja zingine matope kweli..

kwa mapenzi ya mhe. J.K kwani anagawa madaraka kama pipi hajali una uwezo ngani, unakubalika au laa, ni moja ya dhalili ya vongozi wavivu kufikiri na kufanya maamuzi sahihi!

Unafahamu vizuri juu ya hao wawakilishi wanavyopatikana?.Mjengoni wanaingia kupitia vyama vyao vya siasa sio TUCTA.
si kweli ni kwa vile CCM wamelazimisha iwe hivyo ila inapaswa wawe wametoka vyama vya wafanyakazi

Vasco da Gamba wakati anawahutubia "wazee wa magamba" Dar kwenye hotuba maarufu ya "Changanya na za mbayuwayu", wenye akili tulijua anamjenga na kumuongezea umaarufu Mgaya bila yeye mwenyewe kujijua, kwani alikuwa ana jazba amechanganya na za masaburi. Alikuwa anachemka akitoa mlolongo wa upupu wa hesabu kama hakusoma vile!

Kwenye nchi zenye demokrasia ya ukweli, mtu kama Mgaya anaweza kugombea upresida na akachukua kiti, ila hapa kwetu zengwe na tunguli mtindo mmoja.

Huyo Honoratha Chitanda aliyeambulia kura 28 ni nduguye na Mary Chitanda wa Arusha muasisi wa mauaji ya kihistoria?

Kinachofuata ni kuitisha mgomo ili hao wawakilishi feki wa tucta bungeni watolewe.viva tucta.

Ustaadh omar ayub jumaa kuendelea kuwa rais wa tucta naona kama ni ''a big blow'' kwa wafanyakazi wa nchi hii.

Mwanzoni aliaminiwa sana na wafanyakazi wengi alionekana ni kiongozi imara lakini sasa anaonekana amekuwa soft mno kwenye masuala ya kuishinikiza serikali hadi mwaka jana kaimu katibu mkuu mgaya kuonekana kama ndiye kiongozi mkuu wa tucta.

Ustaadh omar ayub jumaa kuendelea kuwa rais wa tucta naona kama ni ''a big blow'' kwa wafanyakazi wa nchi hii.

Mwanzoni aliaminiwa sana na wafanyakazi wengi alionekana ni kiongozi imara lakini sasa anaonekana amekuwa soft mno kwenye masuala ya kuishinikiza serikali hadi mwaka jana kaimu katibu mkuu mgaya kuonekana kama ndiye kiongozi mkuu wa tucta.

Hakuna Rais katika historia ya Tanzania "aliyeboresha maslahi ya wafanyakazi kama JK" none

Na ni busara za mzee Juma..zimefanya kazi..

Kama kuna madiwani wanaingia kwenye vikao harafu hawana sehemu wanayowwakilisha unashangaa hili la wabunge wa kupewa baada ya kuuvua utu wao mmm!! haya ndiyo maajabu ya jfirauni bana.

viti maalum kawaida ni chakula ya wakubwa au kuna mtoto wa mkubwa anabambia

Back
Top Bottom