Marekebisho muhimu ya Katiba yetu

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Yafuatao ni maoni na mtazamo wangu binafsi juu ya uwepo wa haja kubwa ya Marekebisho ya haraka ya Katiba yetu ya JMT kulingana na mahitaji ya sasa. Marekebisho haya yafanyike haraka na mapema kabla ya Uchaguzi wa 2025 kwa sababu tunakoelekea kwa sasa hivi ni hatari zaidi kwa amani na Usalama wa nchi.

Nitaorodhesha hoja hizi kwa awamu kadri ya siku na uwezo unavyoniruhusu kuyaweka maoni yangu kwenye ukurasa mmoja.

1. HOJA YA UFISADI
Hakuna dawa ponya kuhakikisha Ufisadi unakwisha isipokuwa uwezekano wa njia za kinga kuzuia maambukizi na.kusambaa kwa rushwa zipo ikiwa ni pamoja uwepo wa sheria kali, viongozi mahili watendaji, nidhamu ya kazi, Uwajibikaji na Uzalendo na mwisho ni Utaratibu wa mara kwa mara wa Check and Balance.

Mambo haya yatawezekana kama hatua zifuatazo zitachukuliwa katika kufanya marekebisho ndani ya Katiba ya JMT haraka iwezekanavyo.

1) Kurudishwa ndani ya katiba miiko na maadili ya viongozi ambayo yatahusu zaidi kuzuia fursa na unufaikaji wa kiongozi katika biashara yoyote inayohusiana na madaraka yake. (Kickbacks).

Kutoa ama kupokea rushwa ikiwemo na Bakshish na takrima ya mali au fedha yenye malengo ya kushawishi achukue maamuzi ya upendeleo wa mikataba ama tenda za serikali kinyume cha sheria.

2) Kuondoshwa kwa Kinga ya viongozi wote katika ngazi zote aidha wakiwa madarakani ama baada ya madaraka.

Kuhakikisha kiongozi yeyote anayeparikana na hatia hataondolewa tu madarakani bali atashtakiwa na adhabu kali ya kifungo cha maisha itatolewa ikiwa ni pamoja na kupoteza (kufilisiwa) mali zote alizopata ama zitakazo julikana amerithisha, mke/wake zake, watoto wake, jamaa zake kulinga na Ushahidi uliopo.

3) Kuundwa kwa Baraza la Sanate lenye mamlaka ya kupitia mikataba yote ya Kitaifa kabla haijapelekwa kwa rais kusainiwa, jukumu la kuhoji matumizi ama kiongozi yeyote wa Serikali, Bunge, Mahakama, Mashirika na Taasisi zote za Umma na Kijamii kulingana na uzito wa tuhuma zozote za Ufisadi ama kuitia hasara serikali kutokana na matumizi mabaya ya wadhifa ama nyaraka za serikali kutokana na madai ama hoja za Bungeni. Baraza hili ni mbadala wa hoja ya Mh. Mbunge Kishimba alotaka kuundwa kwa wizara maalum.

Nishereheshe kusema kuwa;
a) Baadhi ya Wajumbe wa Baraza hili watakuwa viongozi wagombea Urais wa vyama vyote vya Upinzani pamoja idadi ndogo wajumbe kulingana na ushindi wa nafasi zao kama ilivyo sasa kwenye uteuzi wa wabunge wa viti maalum.

b) Litakuwa na wajumbe wengine 10 watateuliwa na rais kuingia baraza hili badala ya wateule wa rais kuingia bunge la JMT. Tayari rais ana Wabunge wengi wa kutosha ndani ya Bunge kutokana na ushindi wake.

c) Nafasi za Wabunge wa viti maalum zifanyiwe marekebisho kuwa na mbunge mmoja tu mwakilishi wa maslahi ya Jumuiya yake - vikundi vya wachache (minority). Muhimu tuzingatie kuwa Haki hupiganiwa kwa hoja sio idadi ya wawawakilishi.

d) Baraza hili litakuwa na mamlaka ya juu kabisa na huru kumuita na kumhoji kiongozi yeyote mubashara (live) baada ya kuwasiliana na kikosi cha kuzuia rushwa na vyombo vingine vya sheria nchini.

e) Maamuzi ya Baraza hili ndio ya mwisho na ndio lenye mamlaka ya kura ya turufu (veto) sheria ama maamuzi ya rais ikiwa yanakinzana na Kariba au haki ya Wananchi.

Kwa hiyo rais hata ondolewa wala kupunguziwi madaraka yake isipokuwa baraza hili litakuwa mamlaka ya kuhoji na hata kuwa na kura turufu maamuzi ya rais ambayo yanaweza kuathiri maslahi ya nchi kiuchumi, amani, haki na Usalama wa nchi.

4) Mahakama ya Wahujumu Uchumi kurasimishwa rasmi ndani ya Katiba kama kitengo au sehemu ya Mahakama kuu itakayo jihusisha na kesi zote za Ufisadi kwa muda isiozidi miezi sita.

Majaji watano watateuliwa na rais lakini watalazimika kupitishwa kwanza na Bunge pamoja na baraza la Senate kuhakiki sifa zao katika elimu ya sheria (Udadisi wa kisheria), hekima busara na Uzalendo wao kwa Taifa letu.

Nitaendelea sehemu ya pili ya maoni yangu inshaallah tukijaaliwa - Ramadhan Mubarak.
 
Yafuatao ni maoni na mtazamo wangu BINAFSI juu ya uwepo wa haja kubwa ya Marekebisho ya haraka ya Katiba yetu ya JMT kulingana na mahitaji ya sasa. Marekebisho haya yafanyike haraka na mapema kabla ya Uchaguzi wa 2025 kwa sababu tunakoelekea kwa sasa hivi ni hatari zaidi kwa amani na Usalama wa nchi.

Nitaendelea sehemu ya pili ya maoni yangu inshaallah tukijaaliwa - Ramadhan Mubarak.
Asante sana Mkuu Mkandara , tunafuatilia kwa makini sana na hoja kama hii pia niliwahi kushauri Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
P
 
Bila machafuko au mapinduzi usitegemee mabadiliko yoyote ya maana kwenye katiba yetu.
 
Back
Top Bottom