Mpinzani wa JK apeta TUCTA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpinzani wa JK apeta TUCTA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilemi, Sep 17, 2011.

 1. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ninesoma kwenye gazeti la Tanzania daima Mpinzani wa JK apeta TUCTA, kuwa wabunge wa viti maalum CCM wametimuliwa kwenye kukao cha tukta kwa kuwa wao sio wanachama! Wadau, uwezekano huo upo kumteua mtu kuwa mwakilishi wa kikundi asichokijua? Au uteuzi wa wabunge viti maalum wakiwa kama wawakilishi wa jumuia huzingatia vigezo gani?
   
 2. i

  issenye JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 282"]
  [TR]
  [TD] Mpinzani wa JK apeta TUCTA
  • Wabunge wa CCM watimuliwa


  na Grace Macha


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE="width: 712"]
  [TR]
  [TD] ALIYEKUWA Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA), Nicholaus Mgaya, amechaguliwa kwa kura nyingi kuwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, huku akiahidi kufanya maamuzi magumu katika kudai haki za wafanyakazi, ikiwemo kuendesha migomo.

  Mgaya ambaye taarifa za awali zinaonyesha kuwa zilitumika nguvu kubwa kujaribu kumzuia asiibuke mshindi ndiye kiongozi pekee aliyeshambuliwa vikali na Rais Jakaya Kikwete baada ya chama hicho kutishia kuhamasisha wafanyakazi wasimpigie kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
  Akizungumza na walioitwa wazee wa jiji la Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Kikwete aliyeambatana na wakuu wote wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini, alimshambulia vikali Mgaya kiasi cha kufikia kutoa kauli ya kutozitaka kura za wafanyakazi.
  Katika uchaguzi huo wa aina yake, Mgaya alipata kura 324 akiwaacha mbali wagombea wenzake James Mnyeti aliyepata 24 na Honoratha Chitanda aliyeambulia kura 28.
  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uchaguzi huo, Mgaya alisema kazi yao kubwa ni kujadiliana na serikali kutatua madai ya msingi ya wafanyakazi, lakini kama njia hiyo itashindikana, atahamasisha na kusimamia migongo nchi nzima hadi kieleweke.
  Alisema atahakikisha anasimamia kikamilifu kutafuta ufumbuzi wa kero za wafanyakazi, hususan kupunguza kiwango kikubwa cha kodi inayotozwa kwenye mishahara ya wafanyakazi ambayo pia ni midogo kwani haiendani na hali halisi ya maisha.
  Alisema kuwa watashughulikia tatizo la mafao madogo yanayotolewa na mifuko ya jamii kwa wafanyakazi wanaostaafu hali inayowafanya waishi maisha ya mateso baada ya kumaliza utumishi.
  Aidha katibu huyo alisema watapigania mabadiliko ya Katiba ili iweze kuwanufaisha zaidi wafanyakazi.
  Katika uchaguzi huo ulioshirikisha wajumbe kutoka vyama 13 vya wafanyakazi hapa nchini, Omary Juma alifanikiwa kutetea nafasi yake ya urais wa shirikisho hilo katika uchaguzi huo uliokuwa na kila aina ya ushindani ambao ulilazimika kwisha usiku wa manane.
  Nafasi ya makamu wa rais wa shirikisho hilo ilichukuliwa na Nortburga Masikini aliyepata kura 180 akimwangusha Dk. Diwani Mrutu aliyepata kura 126.
  Nafasi ya naibu katibu mkuu ilichukuliwa na Ezron Kaaya aliyepata kura 212 akiwaacha kwa mbali Salma Chande aliyepata kura 84 na Mchafu Chakomu kura 39 na James Kalanje alifanikiwa kutetea nafasi yake ya uweka hazina kwa kupata kura 243.
  Waliochaguliwa kuwa wadhamini wa Tucta na kura zao kwenye mabano ni Charles Mngodo (76 ) , Rehema Mlongelakweli (84), Cecilia Mpamila( 84) na Clement Mswanyama (71).
  Nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya wanawake imekwenda kwa Asia Kapori na katibu wake ni Zainabu Matavale.
  Wabunge wa CCM watimuliwa
  Katika hatua nyingine wabunge wawili wa viti maalum (CCM), Zainab Kawawa na Angellah Kairuki, wamezuiwa kuhudhuria mkutano mkuu wa shirikisho hilo kwa vile hawatambuliwi.
  Mgaya alisema TUCTA haiwatambui wabunge hao wa viti maalum walioingia bungeni kwa mgongo wa uwakilishi wa shirikisho hilo kwani hawakutoka ndani ya shirikisho hilo.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Walipania kumwangusha Mgaya, waziri alikuja pia Riziwani na viongozi wengine toka serikalini walitaka asipite lakini walishindwa.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Huleeee Mgaya wewe ni AK47 kwenye uchaguzi wa 2015 ila chunga uhai wako maana wanaweza kukukolimba!
  Alafu huwa nachoka wabunge wawakilishi wa wafanyakazi hawatambuliwi na TUCTA apo CCM ndo mwaniachaga hoi kwa kuforce Kinga
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Hatutegemei maneno tena. Sasa kazi tu!!!!
   
 6. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wapiga kura wa vyama vya wafanyakazi wamezitendea haki kura zao na wafanyakazi wanaowawakilisha. Sasa kazi ifanyike kwani tumekupatia panga na silaha ya kazi
   
 7. C

  Chacky Member

  #7
  Sep 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hongera ndugu Mgaya. Usibweteke na wala usimkamie mtu, simamia sheria na kanuni za shirikisho unaloliongoza. Ila hili la wabunge wanaodai kuwakilisha TUCTA na wakati hawatambuliki, tafadhali naomba ulifuatilie.
   
 8. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Watanzania hupenda kula 1. Viatu 2. Pamoja. Tuma 1 au 2 kwenda 15015 bure!
   
 9. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama hali ndiyo hiyo basi ujue mabadiliko yameshaiva Tanzania. Kilichobaki ni kupakuliwa tu. Ninadhani CCM bado wanaota ndoto kuwa muda wa mabadiliko haujafika kumbe wao ndio wanaoota ndoto.
   
 10. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Mgaya namkubali huwa haogopi safi sana
   
 11. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  sasa kama shirikisho haliwatambui, waliingiaje mjengoni?
   
 12. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Big Up Mgaya sasa kazi kwenda mbele kutetea maslahi ya wafanyakazi hasa wa serikali ndio malipo kiduchu komaa hadi kieleweke sie tutakuunga mkono
   
 13. j

  joejou Member

  #13
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Hiyo inawezekana Bongo. Madiwani wasio na chama wanashiriki vikao Arusha na posho kama kawa.
  <hbr />
  <br />
   
 14. i

  intellectual39 Member

  #14
  Sep 17, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Comments nyingi ni sahihi, lakini am interested na hii kuhusu uwepo wa waziri na riz1 to facilitate anti Mgaya vote,
  my consern is how we associate the son of president in our Tz politics as well as business sector.
  i think he should use his position as well as his carrier to initiate maendeleo ya jamii by having an organisation, this is the best way to use a president son position as opposed to the kind of lifestyle people always associate him with kama kwenye ilivyoonekana kwenye hiyo comment na nyinginezo ambazo kila siku tunakutana nazo
   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Dawa ya moto ni moto tu, dawa ya fitina ni fitina vile vile, tehe tehe tehe tehe.
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wafanyakazi wametumia kura zao,hawakufanya makosa,sijui kwanini hii inaonesha kuwa hata mwaka2010 hawakufanya makosa ndio maana hata Mr Msoga alipungukiwa kura,it means hakuwapa kweli,,,,,,,,,,VIVA MGAYA,NAKUPONGEZA
   
 17. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,982
  Likes Received: 20,377
  Trophy Points: 280
  Kuhudhuria kwa mtoto wa rais na waziri lazima kunaenda mbali zaidi ya kutaka Mgaya asichaguliwe, na huu ndo ukweli, wabunge walioingia kupitia vyama vya wafanyakazi hawatambuliwi na TUCTA, hivi wafanyakazi wa ccm hawatambuliwi na shirikisho hili!!
   
 18. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Jibu ni taratibu huwa zinapindishwa kukidhi matakwa ya watu...(we regulate our procedures to suit personalities)
   
 19. lutamyo

  lutamyo JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Kama kuna madiwani wanaingia kwenye vikao harafu hawana sehemu wanayowwakilisha unashangaa hili la wabunge wa kupewa baada ya kuuvua utu wao mmm!! haya ndiyo maajabu ya jfirauni bana.
   
 20. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mgaya ahanze na ili la hawa wabunge hii ni kashifa
   
Loading...