Ni kweli kuna Wabunge wa Ikulu?

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,494
37,787
Ibara ya 66 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inataja Aina za Wabunge, ikiwemo wa kuchaguliwa, viti maalum na wa kuteuliwa na Rais.

Jana Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala akimwongelea Bashiru Ally Kakurwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais, alitueleza kwamba Mbunge Huyo Kwa vile ameteuliwa na Ikulu basi anapaswa kuitetea na kuisemea Ikulu.

Swali langu kwake na Kwa wanaomuunga mkono,

Je, katika nchi hii kuna Jimbo la Ikulu? Yaani Ikulu ya Tanzania Kwa mujibu wa Kigwangala na wenzake ina wawakilishi ndani ya Bunge?

Je, na wao wanapeleka hoja bungeni kuiombea Ikulu, maji, barabara, Majengo, au fedha zaidi za maendeleo?

Nchi hii kuna vitu wengine hatuvifahamu vizuri na mojawapo ni hili la Ikulu kuwa na Mwakilishi bungeni.

Tafadhali Mh Kigwangala na wengine mnaoelewa zaidi nisaidieni Mimi Mbumbumbu wa Katiba.
 
Ni kweli, mbunge ni mwakilishi wa waliomchagua. Kama umeteuliwa kutoka Ikulu inabidi uiwakilishe ikulu, kama umeteuliwa kwa chama kwa wale wanawake wa viti maalum inabidi ukiwakilishe chama chako.
Katiba mpya itamke ubunge ni wa kuchagaliwa na wananchi katika jimbo tu.
 
Jana Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala akimwongelea Bashiru Ally Kakurwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais, alitueleza kwamba Mbunge Huyo Kwa vile ameteuliwa na Ikulu basi anapaswa kuitetea na kuisemea Ikulu.
Kuitetea Ikulu kwa mambo yepi!!
 
Ni kweli, mbunge ni mwakilishi wa waliomchagua. Kama umeteuliwa kutoka Ikulu inabidi uiwakilishe ikulu, kama umeteuliwa kwa chama kwa wale wanawake wa viti maalum inabidi ukiwakilishe chama chako.
Katiba mpya itamke ubunge ni wa kuchagaliwa na wananchi katika jimbo tu.
Kwa hiyo Halima na KUNDI lake WANAMWAKILISHA MAGUFULI?
 
Back
Top Bottom