GE2025 Mpina ahamia rasmi ACT Wazalendo, kumvaa Rais Samia Oktoba 29, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671
photo_2025-08-05_14-37-46.jpg

DAR. Mbunge wa zamani wa Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina ni mwanachama halali wa Chama cha ACT Wazalendo na tayari ameshakabidhiwa fomu ya kugombea urais wa chama hicho.

Taarifa za uhakika ndani ya ACT-Wazalendo zinasema, mwanasiasa huyo tayari amekabidhiwa kadi ya chama hicho cha upinzani na fomu ya urais jana Jumatatu, Agosti 4, 2025.

Hatua hiyo ni ukurasa mpya wa kisiasa, baada ya CCM kulikata jina lake kati ya watiania wa ubunge wa Kisesa, kwenye mchakato wa ndani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Taarifa za kujiunga na ACT Wazalendo zinakuja wakati chama hicho leo, Agosti 5, 2025 kinafanya vikao vya kamati ya uongozi, kamati kuu na halmashauri kuu, kuelelea Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho Jumatano, Agosti 6.

Saa 6 mchana wa leo Jumatatu, Mwananchi limemtafuta Mpina kwenye simu yake ya mkononi na baada ya mwandishi kujitambulisha na kumweleza uwepo wa taarifa za yeye kujiunga na ACT- Wazalendo ghafla simu ilikatika.

Chanzo cha uhakika kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa ACT Wazalendo, kimeithibitishia Mwananchi kuhusu kutua kwa Mpina ndani ya chama cha kamati ya uongozi na kwamba tayari ameshachukua fomu ya urais.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, huenda kada huyo mpya akatambulishwa katika kamati kuu au halmashauri kuu leo kabla ya mkutano mkuu kesho.

Kikao cha kamati kuu ya chama hicho kimeanza mchana huu, kikiwa kimechelewa kutokana na mvutano uliokuwepo kati ya aliyepangwa awali kuwa mgombea wa urais wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu na viongozi wengine.

Chanzo hicho kinaeleza, Dorothy alikuwa anashawishiwa kuachia urais kwa Mpina, au awe tayari kusimama naye ndani ya chama hicho, jambo ambalo haijafahamika limeamuliwaje.

“Bado alikuwa anashawishiwa akubali lakini amekataa kuachia urais na anasema waende kwenye kura za maoni lakini bila ushindani wa Mpina. Anasema akiwekewa Mpina kama mpinzani wake kwenye kura za maoni, atajiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya chama,” kimeeleza chanzo hicho.

Chanzo kingine kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa chama hicho, kimesema wajumbe wengi wanaonekana kuvutiwa na Mpina awe mgombea urais wa chama hicho, wakimwona turufu kwa upinzani.

Kutokana na hali hiyo, chanzo hicho kimesema kikao cha kamati kuu kinaendelea kuchelewa, lakini muafaka utapatikana, kwa sababu kinachoangaliwa ni masilahi ya chama so mtu binafsi.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma >> Pre GE2025 - 2025 CHADEMA kumsimamisha Luhanga Mpina?
 
Jicho la tofauti!

The state wameanza kutengeneza matishio ya KITI Cha urais ndani ya ccm kupitia Kanda pendwa!

Ogopa mgombea urais mwenye uwezo wa kuongea kisukuma hadharani akichukua fomu zamae hizie!

Ni hatari sana!

Tena kama watafanya coalition ya kisiasa kwamba ACT isimamishe mgombea urais Chadema isimamishe wagombea wengi ubunge halafu kina Lisu na heche wamsapoti mpina plus kina josephat Gwajima!!!

Wasukuma na wanyamwezinwapo Hadi Zanzibar!!

Hesabu kali!!

KAZI na utu tunasongambele!
 
Zitto kamleta Mpina, ili apate ruzuku iliyonona inayotolewa kulinga na idadi ya kura za Uraisi...

Kafanya alichofanya mbowe 2015....MPINA AMEKWISHA KISIASA!...MAANA AMEHARAMISHA MAGEUZI YA KWELI ALIYOKUWA AKIYAPAMBANIA AKIWA CCM...

ZITTO TARGET YAKE NI RUZUKU TU!... Na anajua mpina atapewa kura nyingi mno! Hasa kanda ya ziwa......ILA HAWEZI KUTANGAZWA NA TUME!
 
View attachment 3432229

DAR. Mbunge wa zamani wa Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina ni mwanachama halali wa Chama cha ACT Wazalendo na tayari ameshakabidhiwa fomu ya kugombea urais wa chama hicho.

Taarifa za uhakika ndani ya ACT-Wazalendo zinasema, mwanasiasa huyo tayari amekabidhiwa kadi ya chama hicho cha upinzani na fomu ya urais jana Jumatatu, Agosti 4, 2025.

Hatua hiyo ni ukurasa mpya wa kisiasa, baada ya CCM kulikata jina lake kati ya watiania wa ubunge wa Kisesa, kwenye mchakato wa ndani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Taarifa za kujiunga na ACT Wazalendo zinakuja wakati chama hicho leo, Agosti 5, 2025 kinafanya vikao vya kamati ya uongozi, kamati kuu na halmashauri kuu, kuelelea Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho Jumatano, Agosti 6.

Saa 6 mchana wa leo Jumatatu, Mwananchi limemtafuta Mpina kwenye simu yake ya mkononi na baada ya mwandishi kujitambulisha na kumweleza uwepo wa taarifa za yeye kujiunga na ACT- Wazalendo ghafla simu ilikatika.

Chanzo cha uhakika kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa ACT Wazalendo, kimeithibitishia Mwananchi kuhusu kutua kwa Mpina ndani ya chama cha kamati ya uongozi na kwamba tayari ameshachukua fomu ya urais.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, huenda kada huyo mpya akatambulishwa katika kamati kuu au halmashauri kuu leo kabla ya mkutano mkuu kesho.

Kikao cha kamati kuu ya chama hicho kimeanza mchana huu, kikiwa kimechelewa kutokana na mvutano uliokuwepo kati ya aliyepangwa awali kuwa mgombea wa urais wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu na viongozi wengine.

Chanzo hicho kinaeleza, Dorothy alikuwa anashawishiwa kuachia urais kwa Mpina, au awe tayari kusimama naye ndani ya chama hicho, jambo ambalo haijafahamika limeamuliwaje.

“Bado alikuwa anashawishiwa akubali lakini amekataa kuachia urais na anasema waende kwenye kura za maoni lakini bila ushindani wa Mpina. Anasema akiwekewa Mpina kama mpinzani wake kwenye kura za maoni, atajiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya chama,” kimeeleza chanzo hicho.

Chanzo kingine kutoka miongoni mwa viongozi wa kitaifa wa chama hicho, kimesema wajumbe wengi wanaonekana kuvutiwa na Mpina awe mgombea urais wa chama hicho, wakimwona turufu kwa upinzani.

Kutokana na hali hiyo, chanzo hicho kimesema kikao cha kamati kuu kinaendelea kuchelewa, lakini muafaka utapatikana, kwa sababu kinachoangaliwa ni masilahi ya chama so mtu binafsi.

Chanzo: Mwananchi
Sidhani kama ni urahis, labda ubunge, urahis ni wrong move and too soon kwa sasa
 
Mpina --- Membe tunawatakia kila la kheri act, lakini yeye mpina anayajua wanachofanya ccm, kugombea kwake sio kujifurahisha?
 
Kosa kubwa hili linajirudia kama lilivyotokea kwa chadema enzi za Lowasa. Yaani Mpina anafika leo na kupewa ugombea urais kwa tiketi ya ACT
Kama ACT wakimsimamisha Mpina kugombea Urais ACT itavuna kura nyingi za Urais kutoka huku Kanda ya Ziwa kwa sababu hatutaki hata kusikia jina la Samia , labda INEC wazifinye tu lakini Samia huku hana chake kabisa na yeye mwenyewe anajua hilo kwani siyo siri hatuna ishu naye.
 
Kama ACT wakimsimamisha Mpina kugombea Urais ACT itavuna kura nyingi za Urais kutoka huku Kanda ya Ziwa kwa sababu hatutaki hata kusikia jina la Samia , labda INEC wazifinye tu lakini Samia huku hana chake kabisa na yeye mwenyewe anajua hilo kwani siyo siri huyo Mzanzibari tuna ishu naye.
Kila kura moja ya huko Kanda ya ziwa itazidishwa mara milioni 1. Usije kushangaa majumuishi ya kura za rais Samia yakaonesha kuwa kavuna mamilioni mengi zaidi toka huko.

Chezea tume-mfukoni wewe!
 
Back
Top Bottom