Mpaka Vazi la Spika wanashonea uingereza!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpaka Vazi la Spika wanashonea uingereza!!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Rubabi, Oct 31, 2007.

 1. R

  Rubabi Senior Member

  #1
  Oct 31, 2007
  Joined: Nov 30, 2006
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpaka Vazi la Spika wanashonea uingereza!! Utumwa wa mawazo huu, washonaji wa kitanzania hawapo, na hizo pes zote hizo?

  Wakati huo huo, Bw. Sitta, aliwafahamisha wabunge kuwa jana alikuwa amevaa joho jipya lililofumwa na nyuzi za dhahabu.

  ``Kwa wale ambao hawajagundua, Spika leo amevalia joho jipya. Lile la zamani lilikuwa limechakaa,`` alisema Spika.

  Alisema vazi hilo ambalo huchakaa baada ya miaka 12 hadi 15, limeshonwa na mafundi maalum mjini London, nchini Uingereza.
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2007
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  hii ni bongo na ukishangaa watakuambia kuwa hata suti zao wanatengenezea new york
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2007
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hahaha, mbona unashangaa mambo madogo! ulitegemea suti ya spiker iliyotariziwa kwa dhahabu ikashonwe kariakoo au magomeni??!!

  si la kushangaa kwa utawala wa sasa au wa miongo miwili tatu ijayo!
   
 4. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,213
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280

  Bado tuna utumwa wa kiakili, kuwa kitu bora lazima kitoke nje ya nchi. Mbaya sana ni kuwa waanzilishi wa upofu huu ni wakubwa wetu!
   
 5. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  nasajesti hata vyupi vyao vishoneshwe india bana, huko si ndio kuna chip leba !
   
 6. N

  Ngao Member

  #6
  Oct 31, 2007
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyie mnafanya mzaha na kuwasusuika wakubwa tu! Nyie mnavaa vya wapi? Acheni hizo! Najua wabongo wengi tuna tabia ya kugeuza kila kitu siasa (si hasa!) Tunachokitetea tunakinyanyapaa inapokuja katika yale tuyafanyayo binafsi. Sifa tu jamvini, lakini najua wengi wa hawa wasemaji ni washabiki wa 'vya nje'. Wangapi tukirudi bongo tunatafuta mavazi ya kitanzania kama yale watengenezayo Afrika Sana pale Sinza?
  Hawa jamaa wameshonea hilo joho 'kwa mama' kwa sababu hawajui pengine pa kushone. Hawajui kuwa majoho ya spika, naibu wake na makarani wa bunge la Afrika Mashariki yalisanifiwa (hata kama hayakushonwa) na hao jamaa wa Afrika Sana!
  Lakini msisahau pia kwamba kuna suala la maslahi ya kipesa (ufisadi!) kwa yule anayeagiza na anayeagizwa mizigo kama hiyo! Uliza bei yake sasa hilo joho! Mhm, kalagabaho!
   
 7. R

  Rubabi Senior Member

  #7
  Nov 1, 2007
  Joined: Nov 30, 2006
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngao, watu binafsi sawa wanaweza wakachukua vitu nje lakini hata vazi la bungeni mpaka washonee ulaya? Huu ni mfano halisi unaoonyesha mawazo tegemezi ya hawa watu.Wabunge wanatakiwa waonyeshe mfano kwanza kwamba wanathamani nchi yao...huu ni mfano mdogo tu unaoonyesha kuwa kweli Tanzania hali ni mbaya, yaani tusitegemee hawa jamaa kama watafanya kitu cha maana.
   
 8. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #8
  Nov 1, 2007
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Wana JF natumaini kwa maneno sasa sisi ni zaidi ya Mafundi. Namaanisha sisi Wadanganyika. Tumetoka kwenye kupiga soga za uso kwa uso, tukahamishia maneno kwenye simu kisha mitandao kama hii JF. Na hapa tukajiona tumepiga hatua na tuko tofauti na wapiga soga wa mtaani. Labda twafikiri kwa kufanya hivi ndo twaitwa wana maendeleo.

  Hivi haya masuala ya Fikra Mgando sisi ndo wa kwanza kuyasikia au kuyaona? Na je tuna utofauti gani na waliotutangulia kuyaona au kuyasikia?

  Lililowazi kwa maneno tu huitaji mtu mwenye uwezo wa kuandika kwenye JF hata wauza kahawa na wacheza bao wasiojua A au Be pale Buguruni wanajua haya na wanayasema sana tena kwa naksi safi sana za Kiswahili.

  Mabadiliko ni mchakato. Lazima yaanzie kwa mtu kwenda kwa watu. Nataka kuleta pendekezo la jinsi ya kupunguza na kisha kuondoa fikra hii. Wazo langu likiunga mkono hata na watu wachache watakaosoma wa thread hii na wakatenda. Mwanzo wa mabadiliko utakuwa umebisha hodi.

  Nashauri tuanzishe siku katika wiki au mwezi ambayo itaitwa "Imetengenezwa Tanzania" yaani Made in Tanzania Day. Siku hii labda J5 au Alhamisi tutakuwa tunavaa mavazi yalitengenezwa nchini, kula chakula cha asili na kununua mali zenye asili ya Tanzania. Kwa tendo hili tutarejesha moyo wa uzalendo, tutajenga uchumi na kukuza taifa. Ebu fikiria kwa mfano mimi nanyi tukaanzisha au kuendeleza kwa tuliokwisha anza, na kisha "Mtalii wa Ikulu" akaunga mkono kama alivyofanya kwa kale kaugonjwa ketu. Akatangaza siku ya kutokula burgers Ikulu hata aje Bush. Tukio hili laweza kutulejesha kwenye kuthamini na kuongeza thamani katika mali na asili zetu.
   
 9. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #9

 10. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mnashangaa nini? Kwani hapa si ilianzisha thread ya kwanini serikali inunue funiture kutoka nnje na wakati kuna funiture hapa nyumbani kujenga soko na ajira za ndani hasa kwa vijana wa VETA na Keko Magurumbasi? Ndio hivyo Tanzania yetu inakwenda kwa mwendo huo.
   
 11. P

  PAGAN JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2017
  Joined: Aug 19, 2014
  Messages: 6,048
  Likes Received: 6,580
  Trophy Points: 280

  We jamaa pumba sana.
   
Loading...