Moyo wangu unaungua, Akili inaharibika, Mwili unakonda, Mapenzi yanatesa sana

Mbona wewe hujaelezea upande wako ? Wewe ulikua kama malaika hukuwahi kumkosea hata mara moja ndani ya kipindi chote icho? Wanawake mnapenda sana kutafuta huruma mda mwingine
 
Salaam waungwana wote,
Kwa kweli katika kitu najuta maishani ni kumpenda huyu mtu, nimekua nae kwa miaka 7 sasa, niseme tu nilimkuta hana kitu kabisa sikujali kitu nilijali mapenzi, tukaanza mapenzi na yalikua moto moto, alikua anafanya kazi sehemu kwa mshahara mdogo sana, wakati huo mie nipo chuo,

Nikaanza mizinga home jumlisha na mshahara wake tukaanza kununua vitu vya ndani, ndani ya miezi kadhaa chumba kilijaa, nikamshawishi tuhame ile nyumba na kuhamia eneo lingine tukapata chumba self na sebule,

Kufupisha story, nilivyomaliza chuo, tukafunga ndoa na kuanza rasmi maisha ya mke na mume, upendo ulikua mkubwa sana, mimi nikiwa nimejiajiri na yeye alikua bado na ajira yake ile ambayo hakua anaifurahia,

Nakumbuka siku moja, kaka yangu akanambia kuna ajira zimetoka ila ni mkoa X nimjulishe mume wangu ili amfanyie mpango , nikamjulisha alivyorudi jioni akampigia shemeji yake, kwa kweli ilikua shangwe maana mshahara ulikua mnono na marupu rupu tele, baada ya kufurahi, mwenzangu akabadilika ghafla, kumuuliza kisa akasema ataniacha peke yangu na hajazoea kua mbali na mimi, tulihuzunika lakini nilimpa moyo kua aende akatafute, kikubwa akumbuke familia aliyoiacha ambayo ni mimi (hatukua na mtoto) akaniahidi vitu vingi vya kunitia moyo na kunifariji...

Siku ya safari ikawadia, ilikua ni siku ngumu sana kwetu, tulilia sana hatimae akaondoka, nikaanza maisha rasmi ya upweke,

Ndani ya miezi sita akanitumia pesa ninunue kiwanja tuanze ujenzi chap, nilifurahi sana na tukaanza ujenzi wa nyumba yetu hadi ikaisha, alirudi baada ya mwaka mmoja, kipindi chote hicho hatukuwahi kukwaruzana, tulishirikiana kwa kila jambo, kurudi kwake ilikua ni likizo ya miezi miwili, akanunua tena kiwanja kingine akajenga foundation, kiufupi maisha yalikua mazuri, siku anaondoka tukaondoka wote nikapaone anapoishi, nilikaa kwa wiki 2 ila nikagundua anapata pesa nyingi sana na wala hatagemei mshahara, nikamuuliza akasema anapiga madili, nikamuonya awe makini asije akaishia jela na jasho lote likapotea akanijia juu na kudai Wanawake ndio tulivyo, tunapenda kuwaza negative muda wote ndio maana hua hatushirikishwi, basi nikamtaka radhi na maisha yakaendelea,

Nilivyorudi, akabadilika sana, akawa busy, anaweza asipokee simu hata wiki anadai busy, ila whatsapp anaonekana na kupost, akawa bata kwa sana, kampan ya kutosha, akanunua na gari ya kutembelea, nilikua naumia sana na mabadiliko yake siku moja nikaenda ghafla mkoa X, nilivyofika nyumba anayoishi nikamtumia msg kua nipo nje kama anaweza mtuma mtu aniletee funguo, akapiga video call akashtuka kuona ni kweli, akaja mbio mbio na lawama kibao kwann nimekuja ghafla, kufungua ndani nikakuta kusafi na nguo za mwanamke zimepangwa vema, kumuuliza akadai kuna mfanyakazi mwenzie aliomba hifadhi yeye alimpisha akaenda kulala hotel, sikutaka malumbano nikazitoa na kuziweka kwenye mfuko, nikamwambia atampatia akimuona, nilikaa pale nikagundua ana wanawake wanne na wote hufika pale kwake, akawastopisha eti mke wake amekuja, niweke wazi sikushiriki nae tendo nilimwambia hadi tupime magonjwa ya zinaa ikiwemo HIV akagoma, basi tuliishi kama marafiki tu hadi siku alipochoka tukaenda kupima wote tukawa poa, mimi nikaondoka, ila Moyo wangu alikua ameshaurarua sana, nikajikuta namchukia hata zile dua njema nilizokua namuombea mume wangu nikaacha, nikaamua kufocus na biashara yangu, nikawa simtafuti kama zamani hadi siku mwenyewe anikumbuke,

Mwaka jana akarudi likizo ya miezi mitatu, kumbe kasimamishwa kazi asiseme, mara akauza bajaji, mara piki piki kumbe anaenda kwa waganga mie khabari sina,

Mwaka huu ndio napata kujua na hasa baada ya miezi mitatu kuisha mtu haondoki, kumbana ndio anasema ukweli wote, wanajadiliwa wakikutwa na hatia wafukuzwe kazi ama washtakiwe, nikamwambia asiwaze amuombe tu Mungu amvushe ila aachane na Waganga wanammalizia pesa, nashukuru alinielewa, ila sasa akaanza kua mlevi yaan analewa hadi analala huko huko Bar, nikajaribu kuwashirikisha familia yake ikawa kazi bure, na mie kuja kushtuka ni mjamzito, kwa kweli ilitupasa tufurahi maana ni ujauzito wetu wa kwanza lakini kwa yanayoendelea tuliishiwa furaha kabisa,

Ujauzito ulikua unaniendesha sana ikanibidi niende kwa wazazi wangu, mwenzangu akauza kiwanja kile alichoanza kujenga foundation, nakumbuka alikuja kuniona na kunipa hizo taarifa, alikaa kwa siku 3 ujauzito ukiwa na miezi miwili tu, siku anaondoka akanipa laki 6 na kuahidi angerejea tena baada ya mwezi,

Mwezi ukapita na mawasiliano yalikua yakusua sua sana, siku moja akaniandikia waraka kua tuachane anahisi amefeli maisha na hawezi kunipa maisha aliyoniahidi na ujio wa mtoto ndio umemchanganya zaidi, anaona hawezi kua baba bora kwa hiyo nipambane mwenyewe, nilivyopata huo ujumbe ilikua mwezi wa tano, niliumia sana, nikampigia sana simu hakupokea, nikawashirikisha wazazi wetu wote, wa upande wangu hapokei simu, kwa mama ake anapokea na kumwambia yupo busy atakuja kuniona,

Mwezi wa saba familia yangu ikanambia niishi tu home, nimwambie anipe talaka nijiandae kwa kujifungua na maisha mengine, nikimwambia anipe talaka hajibu,

Kwa sasa najitahidi kuizoea hii hali ila nashindwa hasa nikiwaza kulea mtoto peke yangu, najiuliza nini kimempata hata kufikia kunifanyia hayo, natamani niondoke niende sehemu mbali sana, sehemu ambayo hakuna mtu ananijua nianze maisha upya ila sasa nina kiumbe kipo tumboni na soon kitazaliwa na kunitegemea,

Mapenzi haya sijui yalitoka wapi na sijui kwanini yanaumiza namna hii, natamani nisingeyajua 😭😭😭

Poleni kwa gazeti.
Pole SANA maam!

" Ni nyakati nzuri maishani ambazo hugeuka GHAFLA na kuwa nyakati mbaya bila HATA kutegemea"

Nakupa somo

Sisi wanaume tuliowengi tukiwa na fedha halafu tukiwa mbali na mke au wapenzi wetu,mchepuko au michepuko huwa natural solution!

YAANI wanawake kama mna akili usikubali kuishi mbali na mpenzi wako au mke kisa Biashara au kazi!YAANI pambana KILA siku moja mbili au tatu uwepo eneo husika!

Kwanini!!?

Coz mwiba ukisimama na kuchachamaa USIKU wa manane utachoma nani!!?!


Huyo JAMAA alipata pressure ya hela na pressure ya kukosa liwazo la KILA siku kitandani!

Mwambie umemsamehe japo hajaomba msamaha halafu mwambie asijali nyakati zitapita tu na mambo yatakaa sawa hata asijali!!!

Chukua hiyo!!
 
hadi huzuni dada rudi kwa Mungu sali sana kula vyema jichanganye na watu wenye maadili sikiliza nyimbo za furaha utapata mwingine wa kukupenda tena sana kwa Mungu linawezekana
 
Najitahidi sana, mwanzoni ilikua nalazwa sana na presha ila sasa hata presha zimepungua ila ni moyo tu bado unauma na akili haijakubali, naishukuru pia family yangu kwa kua na mie bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu
Natamani kujua unaendeleaje, ulishajifungua na mumeo alifanikiwa kurudi??
 
Natamani kujua unaendeleaje, ulishajifungua na mumeo alifanikiwa kurudi??
Ndio Dada nilifanikiwa kujifungua salama mwezi Disemba alhamdulillah mtoto mzuri wa kiume,
Mume bado hajarudi na hata kumuona mtoto hajaja, niliacha kulia sasa nina furaha na amani kila nikimuangalia Simba wangu ananipa sana nguvu na ujasiri,

Allah anikuzie kwenye maadili mema, amiin
 
Ndio Dada nilifanikiwa kujifungua salama mwezi Disemba alhamdulillah mtoto mzuri wa kiume,
Mume bado hajarudi na hata kumuona mtoto hajaja, niliacha kulia sasa nina furaha na amani kila nikimuangalia Simba wangu ananipa sana nguvu na ujasiri,

Allah anikuzie kwenye maadili mema, amiin
hongera sana , hongera.
salamu nyingi kwa mtoto, namtakia kukua vizuri nawe ujaliwe kila uwezo wa kumlea vizuri.
 
Ndio Dada nilifanikiwa kujifungua salama mwezi Disemba alhamdulillah mtoto mzuri wa kiume,
Mume bado hajarudi na hata kumuona mtoto hajaja, niliacha kulia sasa nina furaha na amani kila nikimuangalia Simba wangu ananipa sana nguvu na ujasiri,

Allah anikuzie kwenye maadili mema, amiin
Wow! Hongera sana nimefarijika kwa ujasiri wako, hakika watoto ni zawadi kubwa sana, angalia PM yako tuyajenge huko.
 
Pole sana dada,jitahid uwezavyo kumsamehe na kujisamehe pia,then muombee yeye,familia Yako na ww mwenyewe . Kwenye maisha mitihan ipo japo inapita
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom