Nashindwa kumsamehe huyu mpenzi wangu

Optimists

JF-Expert Member
Oct 17, 2021
278
686
Wakuu naomba mnipe msaada wa mawazo maana tunatofautiana experience humu ndani.

Nilikua na mpenzi tuliyedumu naye miaka mingi kidogo kama miaka mitano kama wapenzi, nilimfahamu nilipokua form five mpaka namaliza chuo tulikua pamoja, baada ya kumaliza chuo nilimpa huyu binti mimba, alinipa taarifa ya mimba wakati huo nilienda mikoani kujitafuta, niliikubali moja moja bila kupinga kwamba nitailea, maana nilikua nimekutana naye siku za hatari, pia nilimpa option ya kwenda nyumbani kwa wazazi wangu maana bado nilikua najitafuta, nilikubali kuilea kwa sababu alikua ni Mwanamke wa ndoto zangu, ilipita kama siku mbili mama yake na binti akanipigia simu kuhusu ujauzito wa binti yake

Alinambia anataka aitoe kwa sababu anataka kumrudisha yule binti shule akareset mtihani ya form four, mimi sikubaliana na ile hali kwa sababu niliona kama ni kosa kubwa sana kwa kufanya kile kitendo, licha ya kufanya jitihada zote za kumuomba yule mama asitoe mimba alifanikisha lengo yake na kumtoa mimba.

Ilipita miezi mitatu sikua normal hasira na chuki zilinitawala sana lakini nilimsamehe yule binti na kuendelea naye kwenye mahusiano baada ya kuomba msamaha sana kwamba sio kosa lake bali la mama yake.

Ulipita kama mwaka mmoja baada ya yeye kwenda kureset form four na kufeli, na kipindi hiko tayari nilikua nimeshapata kazi serikalini alikuja kunitembelea mkoa ambao nilikuepo, alikuja akakaa kama miezi 7, nilimpenda sana huyu binti na lengo langu lilikuwa nikipata likizo niende nyumbani kwao nikajitambulishe, kwa miezi hiyo saba sikua sawa na mama yake kwa sababu ya lile jambo alilolifanyia miaka miwili nyuma, kwa miezi yote saba huyu mpenzi wangu alipata tatizo dogo la kutoona siku zake, nipo sumbawanga akaanza kulalamika kwamba tokea amekuja huu mkoa niliopo hayo matatizo ndio yameanza kumkuta, basi alitaka kwenda kwao, nilimpa pesa kidogo kwa ajili ya matibabu

Nikweli alipoenda kufanya uchunguzi akakutwaa na hormonal imbalance akapewa vidonge vya kunywa mwezi mzima, na period yake inarejea kama kawaida, lakini cha kushangaza nilivyompa hiyo hela kwa ajili ya matibabu, mama yake aliitaka hiyo hela ilikua laki 4, akamletea madawa ya miti shamba, lakini uzuri ni kwamba binti alikataa kumpa huyo mama ake hela, inaonesha mama yake yupo na tamaa sana ya pesa.

Wakuu nimekuja kwenu kuwauliza mambo mbalimbali mnisaidie mawazo maana sina mtu wa karibu wa kumueleza.

Je ni kweli hormonal imbalance, au mwanamke kutokuona siku zake inaweza sababisha akapata matatizo ya kupata ujauzito?, Ananiomba sana kurudi huku nilipo lakini moyo wangu unakua mgumu sana kwa sababu ya mama ake, na hata nikisema nimuoe bado mama ake atakuja kuingilia tu hiyo ndoa ilo jambo linanipa ugumu sana wakuu, mliwezaje kuishi na wakwe ambao ni pasua kichwa?..
 
Mwanamke kama haoni siku zake ni ngumu kupata ujauzito maana inawezekana hapevushi mayai.

Je baada ya kutoa ujauzito aliziona siku zake? Na ni njia gani ya ku abort alitumia?
Kiukweli mama ake ndio anajua maana yeye ndio alimpeleka hospital kwa huyo doctor mtoa mimba, aliendelea kuingia period japo kwa kusuasua, alipokuja mkoa niliopo ndio akakaa miezi 7 bila kuingia.
 
Wakuu naomba mnipe msaada wa mawazo maana tunatofautiana experience humu ndani.

Nilikua na mpenzi tuliyedumu naye miaka mingi kidogo kama miaka mitano kama wapenzi, nilimfahamu nilipokua form five mpaka namaliza chuo tulikua pamoja...
Ushauru wangu.

Huyo mama mkwe ni tatizo. Ili kumuepuka

Kutana na binti, mkafanye uchunguzi kuhusu mifumo yenu ya uzazi wote wawili. Kisha kama hamna tatizo muoe ili uwe na full control of her coz hata mama yake itabidi asiwe na maamuzi kwa binti ambaye ameshaolewa.
Kuhusu hormonal imbalance, ni kweli ni tatizo coz kila hatua ya menstruation cycle iko controlled na hormones ila linarekebishika.
 
Kiukweli mama ake ndio anajua maana yeye ndio alimpeleka hospital kwa huyo doctor mtoa mimba, aliendelea kuingia period japo kwa kusuasua, alipokuja mkoa niliopo ndio akakaa miezi 7 bila kuingia.
Sawa, kama alifanya surgical abortion na hakufanyiwa na mtu ambaye ni mtaalam anaweza akapata majeraha kwenye uterus ambapo itakuwa ni ngumu kwake kupata ujauzito tena. Na dalili zake zinaendana na anazopitia.

Edit: Nimeona kwamba ulimpa laki nne kwa matibabu inawezekana ni kweli alifanya vipimo vya homoni.
 
Hormonal imbalance inaweza msababisha kabisa kukosa ujauzito!

Ila hilo linatibika,kisichotibika hapo na cha hatari zaidi ni huyo mama mkwe,
Hapo umesema binti alimnyima mama yake hiyo laki 4 nahisi imekupa moyo kuwa huenda anaweza kumcontrol huyo mama ila ukweli ni kwamba damu ni nzito kuliko maji, huko mbeleni hao wataungana wawe kitu kimoja na hakuna rangi utaacha kuona!

Unaonekana mstaarab, hiyo familia hutaiweza achana nae huyo binti!
 
Back
Top Bottom