Moyo wangu unaungua, Akili inaharibika, Mwili unakonda, Mapenzi yanatesa sana

Usemacho ni kweli japokua hua siamini kwenye ushirikina ila naamini tulizikosa baraka za Mungu wetu kwa kujiweka mbali nae.
Ushirikina ni imani na unaaminika na dini zoote isipokuwa binaadamu tuu ndu huwa haamini sana japo anauogopa na wanaojua huwa wanauficha ukweli maana ni vita.
Kwenye jamii zetu ukipata maendeleo unapigwa vita kuanzia na ndugu, jamii na marafiki
 
Tutafute Jamaa aje abalance hii story..
Lakin wale wanaofunga ndoa mmoja anaishi mwanza mwingine Dodoma Hilo ni janga hakuna ndoa hapo
 
Pole na wewe ndugu yangu, napata moyo na mie nitayavuka haya na maisha yangu yatarudi kama kawaida,
Amiin
Nakuja PM tuwe close ndugu yangu, nothing last forever kikubwa usiache kufanya kitu ambacho kinakupa furaha, Kama kuzama JF kusoma mada Cheka furahi
When the door of happiness closes another opens but we look so long at the closed do then we don't see the one which has been open for us
 
Salaam waungwana wote,
Kwa kweli katika kitu najuta maishani ni kumpenda huyu mtu, nimekua nae kwa miaka 7 sasa, niseme tu nilimkuta hana kitu kabisa sikujali kitu nilijali mapenzi, tukaanza mapenzi na yalikua moto moto, alikua anafanya kazi sehemu kwa mshahara mdogo sana, wakati huo mie nipo chuo,

Nikaanza mizinga home jumlisha na mshahara wake tukaanza kununua vitu vya ndani, ndani ya miezi kadhaa chumba kilijaa, nikamshawishi tuhame ile nyumba na kuhamia eneo lingine tukapata chumba self na sebule,

Kufupisha story, nilivyomaliza chuo, tukafunga ndoa na kuanza rasmi maisha ya mke na mume, upendo ulikua mkubwa sana, mimi nikiwa nimejiajiri na yeye alikua bado na ajira yake ile ambayo hakua anaifurahia,

Nakumbuka siku moja, kaka yangu akanambia kuna ajira zimetoka ila ni mkoa X nimjulishe mume wangu ili amfanyie mpango , nikamjulisha alivyorudi jioni akampigia shemeji yake, kwa kweli ilikua shangwe maana mshahara ulikua mnono na marupu rupu tele, baada ya kufurahi, mwenzangu akabadilika ghafla, kumuuliza kisa akasema ataniacha peke yangu na hajazoea kua mbali na mimi, tulihuzunika lakini nilimpa moyo kua aende akatafute, kikubwa akumbuke familia aliyoiacha ambayo ni mimi (hatukua na mtoto) akaniahidi vitu vingi vya kunitia moyo na kunifariji...

Siku ya safari ikawadia, ilikua ni siku ngumu sana kwetu, tulilia sana hatimae akaondoka, nikaanza maisha rasmi ya upweke,

Ndani ya miezi sita akanitumia pesa ninunue kiwanja tuanze ujenzi chap, nilifurahi sana na tukaanza ujenzi wa nyumba yetu hadi ikaisha, alirudi baada ya mwaka mmoja, kipindi chote hicho hatukuwahi kukwaruzana, tulishirikiana kwa kila jambo, kurudi kwake ilikua ni likizo ya miezi miwili, akanunua tena kiwanja kingine akajenga foundation, kiufupi maisha yalikua mazuri, siku anaondoka tukaondoka wote nikapaone anapoishi, nilikaa kwa wiki 2 ila nikagundua anapata pesa nyingi sana na wala hatagemei mshahara, nikamuuliza akasema anapiga madili, nikamuonya awe makini asije akaishia jela na jasho lote likapotea akanijia juu na kudai Wanawake ndio tulivyo, tunapenda kuwaza negative muda wote ndio maana hua hatushirikishwi, basi nikamtaka radhi na maisha yakaendelea,

Nilivyorudi, akabadilika sana, akawa busy, anaweza asipokee simu hata wiki anadai busy, ila whatsapp anaonekana na kupost, akawa bata kwa sana, kampan ya kutosha, akanunua na gari ya kutembelea, nilikua naumia sana na mabadiliko yake siku moja nikaenda ghafla mkoa X, nilivyofika nyumba anayoishi nikamtumia msg kua nipo nje kama anaweza mtuma mtu aniletee funguo, akapiga video call akashtuka kuona ni kweli, akaja mbio mbio na lawama kibao kwann nimekuja ghafla, kufungua ndani nikakuta kusafi na nguo za mwanamke zimepangwa vema, kumuuliza akadai kuna mfanyakazi mwenzie aliomba hifadhi yeye alimpisha akaenda kulala hotel, sikutaka malumbano nikazitoa na kuziweka kwenye mfuko, nikamwambia atampatia akimuona, nilikaa pale nikagundua ana wanawake wanne na wote hufika pale kwake, akawastopisha eti mke wake amekuja, niweke wazi sikushiriki nae tendo nilimwambia hadi tupime magonjwa ya zinaa ikiwemo HIV akagoma, basi tuliishi kama marafiki tu hadi siku alipochoka tukaenda kupima wote tukawa poa, mimi nikaondoka, ila Moyo wangu alikua ameshaurarua sana, nikajikuta namchukia hata zile dua njema nilizokua namuombea mume wangu nikaacha, nikaamua kufocus na biashara yangu, nikawa simtafuti kama zamani hadi siku mwenyewe anikumbuke,

Mwaka jana akarudi likizo ya miezi mitatu, kumbe kasimamishwa kazi asiseme, mara akauza bajaji, mara piki piki kumbe anaenda kwa waganga mie khabari sina,

Mwaka huu ndio napata kujua na hasa baada ya miezi mitatu kuisha mtu haondoki, kumbana ndio anasema ukweli wote, wanajadiliwa wakikutwa na hatia wafukuzwe kazi ama washtakiwe, nikamwambia asiwaze amuombe tu Mungu amvushe ila aachane na Waganga wanammalizia pesa, nashukuru alinielewa, ila sasa akaanza kua mlevi yaan analewa hadi analala huko huko Bar, nikajaribu kuwashirikisha familia yake ikawa kazi bure, na mie kuja kushtuka ni mjamzito, kwa kweli ilitupasa tufurahi maana ni ujauzito wetu wa kwanza lakini kwa yanayoendelea tuliishiwa furaha kabisa,

Ujauzito ulikua unaniendesha sana ikanibidi niende kwa wazazi wangu, mwenzangu akauza kiwanja kile alichoanza kujenga foundation, nakumbuka alikuja kuniona na kunipa hizo taarifa, alikaa kwa siku 3 ujauzito ukiwa na miezi miwili tu, siku anaondoka akanipa laki 6 na kuahidi angerejea tena baada ya mwezi,

Mwezi ukapita na mawasiliano yalikua yakusua sua sana, siku moja akaniandikia waraka kua tuachane anahisi amefeli maisha na hawezi kunipa maisha aliyoniahidi na ujio wa mtoto ndio umemchanganya zaidi, anaona hawezi kua baba bora kwa hiyo nipambane mwenyewe, nilivyopata huo ujumbe ilikua mwezi wa tano, niliumia sana, nikampigia sana simu hakupokea, nikawashirikisha wazazi wetu wote, wa upande wangu hapokei simu, kwa mama ake anapokea na kumwambia yupo busy atakuja kuniona,

Mwezi wa saba familia yangu ikanambia niishi tu home, nimwambie anipe talaka nijiandae kwa kujifungua na maisha mengine, nikimwambia anipe talaka hajibu,

Kwa sasa najitahidi kuizoea hii hali ila nashindwa hasa nikiwaza kulea mtoto peke yangu, najiuliza nini kimempata hata kufikia kunifanyia hayo, natamani niondoke niende sehemu mbali sana, sehemu ambayo hakuna mtu ananijua nianze maisha upya ila sasa nina kiumbe kipo tumboni na soon kitazaliwa na kunitegemea,

Mapenzi haya sijui yalitoka wapi na sijui kwanini yanaumiza namna hii, natamani nisingeyajua 😭😭😭

Poleni kwa gazeti.
Karibu kwangu hata mimi mke kanizingua jimbo lipo wazi.
 
kwenye miti hakuna wajenzi...laiti kama mimi mwizukulu mgikuru ningempata mwanamke kama wewe, ningemshukuru allah saba mara sabini, mungu hawezi kukupa vyote
 
Pole sana la msingi kubali kuwa upo katika changamoto, unafuu ulionao kwenu wanakufariji, niliwahi pitia ugumu kiaina km huu umenifanya niwakumbuke wote walionifuta machozi hebu niwasalimie kwanza maana dah bila wao huenda ningejitia kitanzi,
 
Huu ni upande wako upande wake pia unaweza kuwa na story tofauti ila changamoto za maisha pambaneni
 
We nae hebu tutolee kichaa chako, umeona uzi wa mwenzio ndio wa kutolea nyongo, pambana na hali yako usitafute kiki kwa wengine,

Amesema pesa ilitumwa baada ya miezi sita wakanunua kiwanja na kuanza ujenzi, kinachokuuma nini sasa, na wewe tafuta hela ufanye maendeleo chap.
Tuassume alikuwa analipwa 1m kwa mwezi kitu ambacho ni impossible. kwa miezi 6 = 1m × 6 ~ 6m. Hivi kuna kiwanja cha 6m kweli, icho ni kiwanja ama kichanja

Mwambieni atafute hela aache kuota mapenzi. Yaani usingizi wake ni wa kuwaza kuumizwa umizwa tu ilihali mume mwenyewe hana

Tuweni siriazi basi, mshahara wa 1m wapi na wapi hapa bongo. Labda kama ni daktari wa moyo ambae kashindwa kuitibu moyo wake dhidi ya janga la mapenzi

Eti malupulupu, lupu lupu!!!?
Bado hajasema. Story yake imefanyiwa editing sana
 
Tuassume alikuwa analipwa 1m kwa mwezi kitu ambacho ni impossible. kwa miezi 6 = 1m × 6 ~ 6m. Hivi kuna kiwanja cha 6m kweli, icho ni kiwanja ama kichanja

Mwambieni atafute hela aache kuota mapenzi. Yaani usingizi wake ni wa kuwaza kuumizwa umizwa tu ilihali mume mwenyewe hana

Tuweni siriazi basi, mshahara wa 1m wapi na wapi hapa bongo. Labda kama ni daktari wa moyo ambae kashindwa kuitibu moyo wake dhidi ya janga la mapenzi

Eti malupulupu, lupu lupu!!!?
Bado hajasema. Story yake imefanyiwa editing sana
Wewe kweli kichwa box, hebu rudi kasome tena kwa utulivu amekwambia alivyofika huo mkoa aligundua mume wake anapesa nyingi na hagusi mshahara wake, alivyomuuliza akasema anapiga madeal akamwambia aache mwanaume akamjia juu,

Na ndio sababu ya huyo mumewe kusimamishwa kazi kisa kupiga madeal,

Wewe unakuja na ujuaji wako wa kishamba kumbe hata story hujaisoma na kuielewa, halafu ulivyoshangaa watu kulipwa milioni 1 (japo hakusema mshahara wa mumewe) ndio nimezidi kukuona kapuku uliyekosa dira, daaah!
 
Tuassume alikuwa analipwa 1m kwa mwezi kitu ambacho ni impossible. kwa miezi 6 = 1m × 6 ~ 6m. Hivi kuna kiwanja cha 6m kweli, icho ni kiwanja ama kichanja

Mwambieni atafute hela aache kuota mapenzi. Yaani usingizi wake ni wa kuwaza kuumizwa umizwa tu ilihali mume mwenyewe hana

Tuweni siriazi basi, mshahara wa 1m wapi na wapi hapa bongo. Labda kama ni daktari wa moyo ambae kashindwa kuitibu moyo wake dhidi ya janga la mapenzi

Eti malupulupu, lupu lupu!!!?
Bado hajasema. Story yake imefanyiwa editing sana
Unauliza kama kuna kiwanja cha milioni 6!!!
Hahaha hebu fanya mpango uhame hapo kwa mjomba ako ukajitegemee kwanza, wewe hata bei ya dawa ya meno huijui.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom