"Moto umewawakia, hawawezi kuuzima" - Mengi

"Moto umewawakia, hawawezi kuuzima" - Mengi

Hii imekaa politically, you play your cards...!
__________________
Ficha upumbavu wako usiifiche hekima yako!

- Mkulu Invisible, ahsante sana kwa haya majibu yako, nafikiri ndio majibu hasa ya hoja yangu humu, binafsi nimekusikia very loud and clear.
 
Hilo bandiko na mimi nimeliona mahali likisema hivi


• HUYU REGINARL MENGI MBONA ANAMAMBO YA KITOTO JAMANI! AMAKWELI UZEE MBAYA NA HUYU ANAZEEKA VIBAYA, ETI KAANZISHA GAZETI LA KUMSEMA MUME MWENZIE MASHA ‘SEMA USIKIKE’ NA KAFUFUA LILE LA TAIFALETU NA KUMNANGA KARAMAGI KUWA KAKIMBIWA NA MKEWE ANACHUKUA WAKE ZA WATU, MBONA NAYEYE KAMUACHA MJASIRIAMALI MWENZAKE ANAFAKAMIA WATOTO ZA WATU NA WAKE ZAO.
ILA HONGERA ZAKE KWA KUMSOMESHA MTOTO WA LILIAN KIMARO ARUSHA INTERNATIONAL SCHOOL.



naomba kukuuliza kaka, lilian kimaro huyu mke wa dr kimaro?
 
Nimekumbuka wimbo mmoja wa Msondo kama sikukosea``ùkiona mtu mzima analia mbele za watu ujue kuna jambo....``

Nawaambieni engi kulialia mbele ya vyombo vya habari si kawaida kwa mtu mzima na mwenye uwezo kama mengi. Kuna mambo mengi na mazito yanafanyika nyuma ya pazia tupeani muda tu tutaliona. Lakini je nani ataumia na nani atafaidikia????? Lets wait

Mkuu kichakoro nahisi unajua kitu...mwaga hapa JF ndo penyewe!
 
Muonenei huyu kanjanja......yaani leo kaona ya mengi ati kachafuliwa....ila magazeti ya mengi yalipomuandika waziri mkuu wa zamani kuwa kamuweka kimada mbunge aaah hakuona....

Alafu leo anakuja kusema kuwa ati eeeh ooh! mengi anachafuliwa.......huyu anatofauti gani na Balile?....

.....alafu anasema mapambano ya kifikra....kuna fikra hapo?


Mwanzisha Thread mada yake ililenga " Vyombo vya habari kuchafuana, pasipo kuthibitiwa na mamlaka husika" bila kujali vya mmiliki yupi kumchafua yupi.

Posts zimeitwist upande mmoja. Na ndio huo MM ametoa ufafanunuzi kwa nini nao ujitetee nk.

...magazeti kumchafua PM mstaafu ni kazi ya mamlaka kuyaadabisha na si ya MM. Lakini kwa kuwa MM hakulisemea wakati ule haimfungi kusemea ya leo.

Vyombo vya habari kuchafuana, Law enforcers wako wapi???
 
Wana Jf natoa ushauri kwa mzee wetu ambaye ni mzalendo wa ukweli ambaye wengi tunamkubali kwa utendaji wake wa kazi na kujitoa kwake kwa jamii yetu.
mimi ni Mlokole ninaomba kuwasilisha ushauri wangu kama ifuatavyo kupitia kifungu cha Bible wana JF criticims hata kwenye bible. Plz read this to handle CRITICISM;-

Criticism
"He [Jesus] did not retaliate when he was insulted. When he suffered, he did not threaten to get even. He left his case in the hands of God, who always judges fairly."1

"He who fears criticism," declared Thomas Jefferson, "is hopeless. Only those who do things are criticized. The idler is lost sight of in the march of events—but the doer is watched and criticized. To hesitate for fear of criticism loses the battle while the doers march on to victory and triumphs.

"If your cause is right, be not afraid of criticism: Advocate it, expound it, and, if need be, fight for it. Critics always will be, but to the strong-minded they are a help rather than a hindrance. As the horse spurts forward when prodded with the spur, so the doers forge ahead under the lash of criticism. Take your part on life's stage and play your part to the end. Stand for that which is good [that which is right]. Be a doer, not a drone. Look the world in the face and let the critics criticize."

The fact is those who achieve anything worthwhile in life are bound to be the target for the jabs and jibes of jealous lesser men. Furthermore, the person who, for fear of criticism, tries to please everyone ends up pleasing no one.

Realize too, that an incessant, negative criticizer with a chip on his/her shoulder is basically an angry person. They have never resolved their hurts from the past and are looking for hooks to hang their anger on. That is, they are projecting their anger and/or failures on to others rather than accepting the responsibility for their own unresolved issues.

On the other hand, when constructive criticism is given, let's accept it in the spirit in which it is given, evaluate it realistically, and make changes where necessary. This is a characteristic of a mature person
 
Huyu mzee kwa kulia lia kila siku naye kazidi,sasa kama anajua kuna watu wana majumba huko Dubai na wapi mbona hawataji?blah blah kibao zisizo na msingi.Tunahitaji mtu jasiri ambaye atweza kuwafungulia mashtaka mafisadi na siyo kusema ukwasi walio nao.




Huwezijua kama keshatoa iyo taarifa ya mafisadi kunakohusika (PCCB),and by the way sheria (PCCA) inamkataza kuwataja kama tayari ameshatoa taarifa izo PCCB na wanachunguzwa.
He's not perfect but lets agree kuwa he's better than mafisadi ambao mambo yao ya nyumbani ni ya aibu na vilevile ofisini ndo wanaharibu kabisaaaaa!!!
 
Mimi nadhani Mengi anakosea kulia lia mbele ya jamii. Hilo tu mengine ya kumuoa nani sijui, ni private life yake na yeye si mwanasiasa na wala hatujamkabidhi majukumu yoyote ya kitaifa wala la kiserikali.

Kwahiyo mwacheni aoe wanawake millioni!!!! ni matakwa yake binafsi, naacheni udaku udaku na kupindisha topic ya Mzee Mwanakijiji.
 
Cha ajabu ni kuwa katika heading zote ambazo Mengi ameziquote katike tamko lake...Wachangiaji wameamua kuelekeza nguvu zao ktk hili la picha na harusi...Siwalazimishi ni kipi mjadili na kwa muda upi ila naona pana cherry picking hapa.
 
Ninapoona haya mambo mimi yananitisha sana, tunapoelekea ni kubaya, iwapo jambo hili kama raisi wa nchi ataliachilia likaendelea.

Haya mambo yameanza kwa wao wenyewe huko chinichini, kwa kupigana vikumbo bila ya kuambiana maneno, inafikia hatua ya kukunjiana sura, kutokukubali kukaa pamoja, sasa vita yao imefikia kuanikana hadharani. fikiria mtu anaamua kutumia mamilioni ya shilingi ili kumchafua mwenzake, wanapochafuana kunamtu ambaye litamuumiza zaidi, atataka kulipiza ili na mwenzake aumie kama alivyoumia yeye.

Unaweza ukafikiria ni hatua gani itafuata baada ya vita hii ya magazeti, tukumbuke vita hii haikuanzaia kwenye magazeti, hivyo lazima itazidi kuendelea kukua. naweza kuona baada ya vita kwenye magazeti kinachofuata ni kuanza kuana. kunauwezekano mkubwa sana vita hii haitaishia kuana wao wenyewe, bali hata inaweza kupelekea ikawa vita. Sasa ni wakati wa serikali kuingilia kati tatizo hili lisimame kabla ya madhara zaidi hayajatokea.

Cha pili ninachoona mimi, kwa ujumla tunapambana kuhamasishana kutengeneza jamii yenye kupenda kujisomea, sasa hawa jamaa na hii vita yao inapelekea kutengeneza jamii yenye kupenda kufuatilia habari za hovyohovyo, ambazo hazina maana, hivyo kuwa na taifa la watu ambao hawajaelimika, na kupelekea nchi kuendelea kuwa masikini
 
aliomba kura lini hadi atangaze alivyopata mali zake!? Na kwanini kati ya wafanyabiashara wote Tanzania yeye ndiyo unamuwekea kipimo hicho, unless una maana wafanyabiashara wote! Huwezi kuwa na selective justice!

Oh well, it is Mengi so there is a different standard. Kosa lakenini utajiri?

Mzee Mwanakijiji,

Kumbe lengo letu ni kuangalia wale viongozi wenye mali nyingi na tuseme ni wezi.Je ambao hawakuwahi kuomba kula tusiwaangalie?Hili ndilo tatizo la watu akama wewe kusema fulani ajiuzuru kwa kuw atu unaona ni mwiba kwako.

Mengi kosa lake ni kuwaahadaa watanzania kuwa yeye ni mtu safi na asiyecheza michezo michafu ya kisisaisa na kibiashara wakati ni uongo.Amewahi kufukuza watu katiika kampuni yake na hawakuwalipa hata kidogo(utasema kuwa yeye hauhusiki na utendaji wa kampuni).

Uliona jinsi alivyotaka kuwalostisha vijana wa ze Komedi,Hii yote inaonesha ni mtu mwenye visasi(yeye mwenyewe aliingilia suala hili binafsi wkati kuna utendaji).

Huyu huyu ndiye anayedaiwa Pesa na NBC ya kipiundi kile mpaka leo anadaiwa (hawa ndiyo wahujumu uchumi).

Invisible,
Kwa taarigfa yako Picha zile hazikuanzia Ze Utamu,Ziliaanzia hapa hapa JF.ina maana kama kuna habari ya kisiasa na iko Ze utama hautaiweka hapa?Mbona kipindi kile mlitaka kuweka zile picha za mwenyekiti wangu?Mkaacha tu?..No way!

Kwanini alikataa waandishi wa habari wasimuulize Maswali?kama kweli alitaka kueleza ya kweli?angekuwa Mkapa hapo mngesema nini?Yes kw ahili alichemka na inawezekana mambo yote wanayosema kuhusu yeye ni ukweli na time will tell

FMES umenena vyema na kwa upole ulionyamaa.Tupo pamoja Mzee wa sauti za Umeme!
 
Mzee mengi anachemsha!
Siku zote huwezi kushindana na waandishi wa habari ktk Udaku, na hasa habari kama hizi. Yeye kama anajua hakufanya makosa inabidi akae pembeni wako kina Mwanakijiji wangechukua jukumu la kuzungumza on his behalf...
Binafsi swala la kuwa ameoa au hakuoa halina mpango kabisa isipokuwa tu ushauri wangu ni kuwa anapokana ndoa anazidisha maswali mengi zaidi vichwani mwa waswahili kiasi kwamba kwa desturi zetu na hasa toka ukurasa wa Udaku - Mengi anaonekana ni PLayer na huyo Lilian ni Kicheche!..
Afadhali mara 10 habari za ndoa zinaweza kupotea mara moja kuliko kukana ndoa kwa sababu, sasa hivi waandishi wa habari watazidi kuwafuatilia zaidi yeye na huyo Lilian..
 
TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa muda mrefu sasa, magazeti yanayofadhiliwa na watuhumiwa wa ufisadi yamekuwa yakiandika mambo mengi yaliyojaa fitina na uongo dhidi yangu na familia yangu. Kwa mfano:-

• Mengi anataka kumng'oa JK 2010?
• Mengi hatari kama Hitler
• Ndoa ya Reginald Mengi na CHADEMA yabainika
• Mengi na kashfa ya ufisadi – Tume ichunguze bilioni 40 za ukimwi.
• Mengi aoa tena – harusi yafungwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Kanali Fabian Massawe

Taarifa zote hizi ni za uongo mtupu.

Kama nilivyokwishasema awali, mafisadi wanaotuhumiwa kuiba fedha za umma ambazo zingetumika kwa kujengea shule na kupiga vita maradhi na umaskini wamekuwa wanazitumia fedha hizo kwa maslahi yao binafsi kwa kujijengea majumba ya kifahari huko Dubai, Uswisi na Afrika ya Kusini, na kubwa zaidi, sasa wanazitumia kudhoofisha nguvu zinazopiga vita ufisadi.
Mafisadi hawa wameanzisha magazeti zaidi ya 15 ambayo yanasambaza fitina na uongo uliotungwa.

Nia na madhumuni ya mafisadi kutunga na kusambaza fitina na uongo ni kuufanya umma uelekeze nguvu na mawazo yao katika fitina na uongo huo na kuacha kufikiria na kuzungumzia tatizo kubwa la ufisadi.

Fitina na uongo wa mafisadi hawa ni sumu inayosambazwa ndani ya jamii na inaweza kujenga chuki, kuwagawa wananchi na kuvuruga amani. Iwapo vurugu zitatokea, basi mafisadi hao wataanza hata biashara mpya ya kuuza silaha ili Watanzania wazitumie kuuana wenyewe kwa wenyewe.

Wengi wa mafisadi wanaishi maisha machafu mno. Hadi hapo Baraza la Habari Tanzania (MCT) litakapotoa msimamo wake juu ya uandishi wa mambo ya faragha (privacy) endapo waandishi wa habari wanaoheshimu taaluma yao ya kuandika ukweli wataandika uchafu wa maisha hayo, wasilalamike.

Ninarudia tena kusema kwamba ni lazima mafisadi waelewe kwamba kutapatapa kwao ni jitihada za wafamaji kwa sababu moto wa vita dhidi yao umekwishawaka na hawawezi kuuzima au kuukwepa. Hautazimika kamwe, na jitihada zao za kudhoofisha nguvu za vita dhidi ya ufisadi zitageuka kuwa kichocheo cha moto huo hata kama watafanikiwa kuwatokomeza watu wanaopiga vita ufisadi.
____________________
Reginald A. Mengi
Mwenyekiti Mtendaji
IPP Limited
10 Februari,2009


My Take:
Nashindwa kuelewa kwenye nchi ambayo ina sheria kali ya magazeti na ambapo watu wanaimba kila siku suala la maadili ya "kitanzania", kwanini tumefika hapa tulipofika? Waziri wa Habari ataendelea kukaa pembeni na kuangalia kusambaa huku kwa habari za kupakana matope hadi kwenye vitanda vya watu?

Nimeshasema huko nyuma nikimnukuu mwalimu wangu "ukivunja kanuni kubwa, kanuni hiyo itatafuta namna ya kukuvunja". Sasa magazeti kadhaa yanaanza kushindana kuandika nani anajua uchafu wa kiongozi gani zaidi na siku si nyingi hili litafika hadi kwa Rais, na mtu mwingine yeyote ambaye ataonekana kuwa ni fair target. Somebody got to stop this or as a people we ough to be prepared to pay a huge price for the silence we maintain.

Haya mambo bwana si yetu ni ya hao hao wakubwa. Hii ni vita kati ya mafahali wa Tanzania kwani kama huu ni mchezo tu basi ungekwisha komeshwa. Kwani hakuna sheria za mtu binafsi kushitaki ? Kwanini Bwana Mengi asifanye hivyo na katika kufanya hivyo atathibitisha uongo unaoandikwa kwake.

Sisi wananchi wa kawaida hatuwezi kumsaidia Mengi au yeyote katika vita hivi kwani kama kauli zetu zina athari basi tungezuia kufungiwa kwa muda Gazeti la Saidi kubenea au kupigwa marufuku gazeti la Marehemu Ali Nabwa.
Nahofu kuwa pengine haya malalamiko ya mengi yana mwelekeo wa baadae kwani inashangaza kuona mtu aliesababisha kutumiwa kodi ya wananchi millioni 100 na kutumika chombo kikubwa kama Bunge kujadili malalamiko yaliyokuwa hayana msingi, leo ashindwe kuchukua hatua za kisheria kwa vigazeti vidogo? Hii ni Bongo na usikatae kitu kwa maelezo ya muhusika Cross your fingers.
 
Duh Mengi umechemsha babake. Nway pamoja na malalamiko yake bado tukubali kitu kimoja anacholalamik ayeye ni kwa mafisadi kupitia vyombo vya habari (magazeti) wanamchafua na kuwa privacy yake imebakwa na hii vyombo vya habari.... ninachopenda kujua mimi ni je si kweli kuwa haya magazeti mapya mawili ya IPP i.e. Sema Usikike na dada yake lile lingine si mali yake? Kama ni ya Mengi je kuandika habari za chumbani za Karamagi na mkewe au mke wa Mongela si kubaka privacy zao?

Au ndo yale ya Mkuki kwa........
 
Na hii inamhusu nani mkuu? Think of it...

Ile hoja ya masuala ya mapenzi na picha ambazo hatukuwa na hakika nazo zilikuwa kwenye blog inayohusiana na 'ufisadi wa mapenzi' (siitaji ushaijua) hivyo tukaonelea heri wao wacheze part yao.

Hii imekaa politically, you play your cards...!
.......mkuu JF ndio walianza kuweka picha zile..then wale wakakopi huku.....zilikuwa hapa siku nzima kesho yake zikawa kule........

aaww
 
Mafisadi hawatashinda kamwe kwani Mengi anawakilisha watanzania walionyonywa kwa muda sasa.Mengi endelea kuwatetea wanyonge utabarikiwa kama unavyoendelea kuwasaidia jamii kwa misaada mbalimbali.
 
Huyu Mengi nae bwana si akae kimya tu mbona hata yeye kaanzisha magazeti ya udaku?!Afanye kazi zake na aache kulalamika kila siku malalamishi tu!
 
Wapendwa wanaJF mmeandika sana, mmejadili sana na pia mmelumbana sana juu ya hili, itoshe basi. Hivi kama tukijiuliza watanzania wenzetu leo wamenufaika vipi na hili do we have answers?

I love JF kwa sababu most of the time iko forcussed, lakini leo I feel kama hatujawatendea haki watanzania, tukumbuke kitu kimoja sisi ni sehemu ya watanzania wachache ambao tumebahatika kupata avunue for views exchange and constructive discussion, na ambao tupeta bahati ya mawasiliano kama haya na kwa hivyo basi tuwawakilishe hawa mamilioni kwa kujadili issues of their best interest and concerns, hivi kweli ndugu zetu vijijini hivi sasa wanasuffer na njaa ukame, ukosefu wa fedha na umasikini badala ya sisi kujadli how we take our country forward, tunajadili ndoa ya mtu all day long? what do we get at the end of the day? hiyo ndoa inachangia kiasi gani katika pato la taifa hili, inakuza uchumi kwa asilimia ngapi? please let us get back, wapi tumeteleza tujisahihishe?
Chonde wanaJF watanzania wenzetu wanatutegemea sana kuokoa nchi yetu, kama hamjui hilo tafadhali take time to visit just part of this country, you are constructive idea is wasted in this.

Let others discuss about people and JFdiscuss about issues

with Love
 
WATANZANIA KWELI TUMECHOKA!

Hivi Mengi alishawahi kuiba hela zetu za EPA? Mengi alishawahi kuondoka na Kiwira? Mengi alishawahi kutuletea Richmond? Mengi alishawahi kusaini mikataba ya MANGUNGO iliyouza rasilimali zetu? Jamani tuwe serious! Huyu mzee anapiga kelele kama sisi tuu hapa. Hata kama ana udhaifu wake binafsi..hiyo haituhusu..sisi tunaangalia wabaya wetu MAFISADI...Kama Mengi ameoa wanawake..na kuwaacha does that bring food on my table at night? or will it take bed nets in rural hospitals? Not at all!..but Richmond which was commissioned by Lowassa..does affect that possibility, contracts signed by Karamagi does etc...... kinachofanyika hapa watu wanajaribu kupoteza mada kusudi Mengi awe topic yetu hapa! Mengi sisi hatuhusu! Hata kama ana matatizo yake...its him..as long as is making noise kama sisi dhidi ya haya mafisadi..thats what we want! Ndo maana wengine tukisikia mama Kilango Malecela anapigia kelele mafisadi tunasema amina! hata kama ni CCM!

Mwenye data kama Mengi na yeye alishawahi kuiba KODI ya watanzania popote pale...azimwage hapa tuzichambue! Hapendwi mtu hapa. Ni maslahi ya watanzania basi!

Who cares hata kama Mengi angekuwa na wake kumi? Who cares hata kama angekuwa anachukua m...ya Jolly`s?

Jamani...tusipoteze mwelekeo kwa cheap politics za namna hii za haya mafisadi. Hata kama ingekuwa ni Lowassa au Karamagi au Mramba...hata kama wangekuwa na wake..mia...it doesnt affect Tanzania. It will only affect us kama hao wanawake wanatunzwa kwa kodi zetu.

Again I say, Mengi is not an issue at all. Issue kubwa ni mafisadi. Tuache kugeuza mijadala hapa! Mengi kusimama na kuikemea system..siyo unafiki..ni kwamba alikuwa na hope kwamba watawala watabadilisha mambo lakini wamekuwa wezi kuliko..kwani ni wangapi wetu tulimpigia kura JK..lakini leo tunamlaani kama fisadi ambaye kashindwa kushika mafisadi wenzake? JK amekuwa dissapointment! Lakini haituzuii kumsema. He betrayed our trust.

Mengi is not an issue! Mafisadi ni issue! wanaoumia na na huu ufisadi ni mamilioni ya wananchi wenzetu...tuachane na akina Mengi ambao ni wananchi kama sisi....tule sahani moja na mafisadi ambao wanataka tuwe wakimbizi na makuli kwenye nchi yetu!
 
WATANZANIA KWELI TUMECHOKA!

Hivi Mengi alishawahi kuiba hela zetu za EPA? Mengi alishawahi kuondoka na Kiwira? Mengi alishawahi kutuletea Richmond? Mengi alishawahi kusaini mikataba ya MANGUNGO iliyouza rasilimali zetu? Jamani tuwe serious! Huyu mzee anapiga kelele kama sisi tuu hapa. Hata kama ana udhaifu wake binafsi..hiyo haituhusu..sisi tunaangalia wabaya wetu MAFISADI...Kama Mengi ameoa wanawake..na kuwaacha does that bring food on my table at night? or will it take bed nets in rural hospitals? Not at all!..but Richmond which was commissioned by Lowassa..does affect that possibility, contracts signed by Karamagi does etc...... kinachofanyika hapa watu wanajaribu kupoteza mada kusudi Mengi awe topic yetu hapa! Mengi sisi hatuhusu! Hata kama ana matatizo yake...its him..as long as is making noise kama sisi dhidi ya haya mafisadi..thats what we want! Ndo maana wengine tukisikia mama Kilango Malecela anapigia kelele mafisadi tunasema amina! hata kama ni CCM!

Mwenye data kama Mengi na yeye alishawahi kuiba KODI ya watanzania popote pale...azimwage hapa tuzichambue! Hapendwi mtu hapa. Ni maslahi ya watanzania basi!

Who cares hata kama Mengi angekuwa na wake kumi? Who cares hata kama angekuwa anachukua m...ya Jolly`s?

Jamani...tusipoteze mwelekeo kwa cheap politics za namna hii za haya mafisadi. Hata kama ingekuwa ni Lowassa au Karamagi au Mramba...hata kama wangekuwa na wake..mia...it doesnt affect Tanzania. It will only affect us kama hao wanawake wanatunzwa kwa kodi zetu.

Again I say, Mengi is not an issue at all. Issue kubwa ni mafisadi. Tuache kugeuza mijadala hapa! Mengi kusimama na kuikemea system..siyo unafiki..ni kwamba alikuwa na hope kwamba watawala watabadilisha mambo lakini wamekuwa wezi kuliko..kwani ni wangapi wetu tulimpigia kura JK..lakini leo tunamlaani kama fisadi ambaye kashindwa kushika mafisadi wenzake? JK amekuwa dissapointment! Lakini haituzuii kumsema. He betrayed our trust.

Mengi is not an issue! Mafisadi ni issue! wanaoumia na na huu ufisadi ni mamilioni ya wananchi wenzetu...tuachane na akina Mengi ambao ni wananchi kama sisi....tule sahani moja na mafisadi ambao wanataka tuwe wakimbizi na makuli kwenye nchi yetu!

......GAWIZA SANA.....Masanja!!
 
Back
Top Bottom