"Moto umewawakia, hawawezi kuuzima" - Mengi

Nakuelewa, sisemi ban udaku, nilichokua na maanisha ni sisi watanzania hatuna luxury ku intertain udaku katika kupitisha mada, tunachotaka ni kutumia taaluma katika kupitisha mada.

Wenzetu dunia ya kwanza have different problems not basic problems tunazokumbwa nazo sisi. Udaku is for leasure reading, na kuleta kicheko na utani katika siku iliyojaa ishuzz, hatuwezi tumia hizi wakati wa vita.

Mimi nikiamua kusoma udaku nasoma kwa burudani tu. Napembua pumba na mchele. Sasa kama wapo ambao wao huchukulia udaku kama taarifa ya habari za uhakika hilo ni juu lao.

Ninachojua ni kwamba hata iweje udaku hauwezi kupigwa vita. Ulikuwepo, upo, na utaendelea kuwepo.

Nakumbuka sana stori za Mchonga na kifimbo chake....nakumbuka sana stori Mchonga kuwashikisha watu ukuta na kuwacharaza mboko, mmojawapo akiwa Cigwiyemisi Malecela..lol.....huo haukuwa udaku

Au stori za Mwinyi kutoka na binti aliyekuwa akisoma Jangwani Sekondari....
 
Hivi Bongo kuna waandishi uchwara?

waandishi uchwara mbona wapo kila mahali, ka vile wapo wahandisi uchwara, wahasibu uchwara, wanasiasa uchwara, walimu uchwara n.k Huwezi kuundoa uchwara wote kwenye fani yeyote. Watu uchwara wapo kila kona and as a matter of fact hata huko majuu kwenyewe wamejazana!
 
Hata kama wana ndege hayamhusu ni za kwao mbona yeye anavyotumia brand za watu hatusemi ?? Radio 1 , itv si brand za watu wengine ? The gurdian si brand ya watu wengine ?? Kwanini asiwe mbunifu awe na vyake ??

We dogo growup sasa yani kweli unategemea kama angekuwa anatumia hizo brand illigal hayo makampuni yasingechukua hatua mpaka leo ambapo Itv wanazaidi ya miaka kumi?? some times u have to be serious kidogo shy maana unaboa sasa kha
 
waandishi uchwara mbona wapo kila mahali, ka vile wapo wahandisi uchwara, wahasibu uchwara, wanasiasa uchwara, walimu uchwara n.k Huwezi kuundoa uchwara wote kwenye fani yeyote. Watu uchwara wapo kila kona and as a matter of fact hata huko majuu kwenyewe wamejazana!

shhhhh, nyamazeni. Kama waandihi uchwara wapo, waacheni waendelee na kazi zao za uandishi.

Vinginevyo say no to double standard, baadhi ya habari ziandikwe na waandishi uchwara mzishikie bango ni za uongo, nyingine mzishikie bango ni za kweli.

Shoddiest ....... crummy......
 
gembe wewe sasa umezidi blah blah,yaani unakuja huku kutoa madudu tu,je wewe kweli umeenda shule bwana?au jamm wamekuahidi kazi ya u house boy kule ikulu 2010.ndio mana unakinga hawa mafisadilos.duh miye nimechoka na we....
 
Lakini kubwa zaidi kwangu ni kitu ambacho watu wanakiona kinakubalika. Mara zote tunasema watu wasijichukulie sheria mkononi, lakini inakuwaje wakati sheria inayotakiwa kukulinda inaonekana haikulindi?

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa hakuna ulazima wa Mengi kujibu mapigo kwa jinsi hiyo hiyo, lakini inakuwaje kama kwa kutofanya hivyo kunakaribisha mashambulizi zaidi? Kwamba mtu akae kimya na kushambuliwa kwa sababu ya hadhi yake wakati kinachoshambuliwa ndiyo hadhi hiyo hiyo?

Kama kuna habari imeandikwa "Mengi kama Hitler" kweli anatakiwa akae kimya?

Hata huku majuu mtu akiandikwa vibaya au wakimnukuu vibaya au wakisema kitu ambacho si kweli juu yake mtu huyo ana haki ya kujitetea. Kutoa matamko mara kwa mara kusahihisha uongo ni jukumu la mtu kufanya huwezi kufanyiwa. Kwa sababu ukiuacha uongo uendelee juu yako watu wataanza kuuamini.

Mengi hakutakiwa kutoa kauli hii, wala hakupaswa kutoa kauli hii, lakini alilazimika. Angalau yeye anaujasiri wa kufanya hivyo, hao kina Kalikaro kwanini na wenyewe wasitoke kusema tu tukajua it on?

Hatari ni kuwa sheria isipokulinda, na wewe ukaamua kutumia njia chafu wanazotumia wabaya wako, upo uwezekano, na mizengwe ambayo tumekuwa tukiishi nayo, wabaya wako wakatumia kuiga kwako kukufix. Kumbuka, MwanaHalisi halikuwa gazeti la kwanza kuandika kuwa kuna njama za kumtoa Kikwete mwaka 2010, lakini liliadhibiwa peke yake.
Kwa kuwa tayari Mengi alikuwa na magazeti ambayo yamejipambanua kupiga vita ufisadi, ingekuwa vema angeendelea kuyatumia hayo hayo kwa kuwa tayari yameshajijengea credibility, naamini kwua angeweza kupambana na uzushi huo kwa ufanisi zaidi kuliko kuiga 'ujinga' unaofanywa na hao wanaotapatapa.
 
Hili gazeti za Tazama Tanzania linaelekea kupotoka kabisa. Nadhani wanadhani kuwa Tanzania ya sasa imejaa malimbukeni tuuuu.

Uongo na uzandiki ulioelezewa kwenye gazeti hilo (kijarida hicho) unatia aibu kubwa. Yaani kuna Mtanzania mwenye akili timamu anaeweza kufikiria (licha ya kusema) kuwa vita ya ufisadi haina maana? Nadhani kama yupo, basi inabidi kujenga shule nyingi zaidi na kusomesha walimu zaidi. Maana ni dhahiri shule zilizopo zitamaanisha kuwa hazitoshi.
 
Hili gazeti za Tazama Tanzania linaelekea kupotoka kabisa. Nadhani wanadhani kuwa Tanzania ya sasa imejaa malimbukeni tuuuu.

I dont think so. Waliolianzisha walikuwa na kusudi maalum na sasa naona linaanza kutimia. Wameshamuingiza mkenge Mengi kwani yeye, kama walivyo wengi walidhani kuwa lengo la magazeti hayo ni kupakazia. Walijua tangu mapema kuwa watu wengi hawatauamini uongo wao. lakini mbinu imesaidia kumuondoa Mengi alikokuwa ameshikilia, na sasa anaanza kurusha matope kama wao. Nakuhakikishia, watu wenye kufikiri kwa kina watapata shida sana kuanza kumtofautisha Mengi na maadui zake hivi sasa. Huko ndiko walikokuwa wanataka kumpeleka na wala si kumchafua kama ambavyo wengi tunaamini.
 
I think you are right. Maana ukicheza na kichaa, inakuwa shida kutofautisha nani hasa ni kichaa.
 
I think you are right. Maana ukicheza na kichaa, inakuwa shida kutofautisha nani hasa ni kichaa.

Kwa hilo, nguvu zake kupambana na mafisadi zimepungua kiasi. Atakapobaini kuwa amepelekwa kusiko, ataanza jitihada za kujitoa huko na kurudi katika mstari, concentration yake dhidi ya mafisadi itazidi kupungua zaidi. Na nani anajua kwua mafisadi wana mikakati gani zaidi ya kumfanya Mengi ajikaange kwa mafuta yake mwenyewe????
 
Kwanza kabisa nampongeza R. Mengi kwa kuja na statement hii.

Pili, sisi watanzania tunapenda sana story za udaku na kuongea mambo ambayo hatuna uhakika nayo. I think hata ingekuwa wewe, jiulize, ukiwa unasakamwa na watu, watu wanapenda kuingilia maisha yako, je ungefanya nini.

It is my hope kwamba we are clever enough kujua right from wrong. Sasa badala yakuongea vitu visivyo na uthibitisho, tuchague moja:

1: Kumuunga mkono Mengi kuwawashia moto hawa mafisadi wanaokula nchi na jasho letu.

2: Kutokumuunga mkono Mengi, na kuzorotesha juhudi zake za kupambana na mafisadi.

Wengi wetu humu if not most tunatumia "aliases" tukiogopa kuwa linked with whatever we say, sasa huyu jamaa, including Dr. Slaa, Anne Kilango, Zitto et al wanapambana wazi wazi na haya mahujumu uchumi.

Let's try and rally behind these guys in whatever form we can.

Kama huna uthibitisho au credible reference (sio from udaku) basi its best we dont chafuana or endorse kuchafuana.

ps: ngoja nikanyunyizie petroli kwenye huo moto, get ridance to fisadiz!!

huwezi kumweka MENGI kwenye listi ya wapiganaji kama akina Dr. Slaa. MENGI ni mbabaishaji kwani huwa anaongea kwa kuzunguka zunguka bila kusema wazi. ooh wananionea mara oooh waziri kijana wapi bwana. Binafsi huwa naona anawaacha watu waendeleze majungu.
Dr. Slaa anakupa kitu kilicho kamili kama ni jina linatajwa, kama ni document ilakuwa referred. hakuna kuuliza wala kupika majungu.
 
Je mnajua kwamba kuna wengi tu wanaoiona JF kama jukwaa la udaku - je , hiyo ni sababu tosha ya kutuzuia kumkoma nyani ? no never. Ni kwa sababu JF inawakuna na kuwanyima usingizi na moto uliowashwa na JF unazidi kuwaka. JF imeweza kuwafanya mafisadi wachanganyikiwe kiasi cha kuanza kunyosheana vidole wao kwa wao - haya ni mafanikio makubwa.

Mafisadi yanapenyeza watu humu JF lakini judging by the number of vigilantes wanaochipuka kila kukicha tumeshuhudia umoja wao ukimomonyeka kwa kasi na kuanguka kama mnara wa Babeli. Tunaona thamani ya rupia wanazopenyeza ikishuka mbele ya wapambanaji wa kweli wanaosukumwa na dhamira, nia na ujasiri wa watu waliochoka na ulafi wa wachache.

Mwaka 2005, Reginald Mengi kwa imani alizokuwa nazo wakati huo, alivitumia vyombo vyake hivyo kuwapigia debe mafisadi - maybe then he was blind but now he can see. Kwa vile kathubutu kuingia kwenye uwanja wa mapambano kama wengi wetu, lazima tujiulize kama wagomvi wake ni hao hao tunaopambana nao - na kama ni hivyo hatuna budi kumuunga mkono.
 
Hivi ni vita vya Kunguru sio,inaweza kuwa furaha yetu! Itafika siku hatutataka kuamini habari zozote kutoka kwenye hayo magazeti yao, kwani yanaishia kuchafuana na kutetea maslahi ya wale wanaowalisha hao waandishi. It's a shame for a profession to be turned to this kind of rubbish, I stand to be corrected. Hakuna watu serious kwenye hiyo fani ya uandishi wa habari, ambao wanaweza kusimama against odds kutetea ukweli?
 
huwezi kumweka MENGI kwenye listi ya wapiganaji kama akina Dr. Slaa. MENGI ni mbabaishaji kwani huwa anaongea kwa kuzunguka zunguka bila kusema wazi. ooh wananionea mara oooh waziri kijana wapi bwana. Binafsi huwa naona anawaacha watu waendeleze majungu.
Dr. Slaa anakupa kitu kilicho kamili kama ni jina linatajwa, kama ni document ilakuwa referred. hakuna kuuliza wala kupika majungu.

Ng'azagala..
Wewe na mimi ndio wababaishaji! Angalia tunaogopa hata kuweka utambulisho wetu. Afadhali yeye anayeonekana anaongea mbele za watu. By the way ni nini mchango wako kwenye hii vita ya ufisadi? Au ndio umekaa kama uko kwenye TV screen ukiangalia soka? Tatizo letu Watanzania ni maneno meeeeeeeeeeeeengi..... ukosoaji mwiiiingi matendo hakuna. Hata mimi huwa najiuliza hivyo hivyo... nimefanya nini kwa nchi yangu tangu hii vita ianze? Amka
 
Hatari ni kuwa sheria isipokulinda, na wewe ukaamua kutumia njia chafu wanazotumia wabaya wako, upo uwezekano, na mizengwe ambayo tumekuwa tukiishi nayo, wabaya wako wakatumia kuiga kwako kukufix. Kumbuka, MwanaHalisi halikuwa gazeti la kwanza kuandika kuwa kuna njama za kumtoa Kikwete mwaka 2010, lakini liliadhibiwa peke yake.
Kwa kuwa tayari Mengi alikuwa na magazeti ambayo yamejipambanua kupiga vita ufisadi, ingekuwa vema angeendelea kuyatumia hayo hayo kwa kuwa tayari yameshajijengea credibility, naamini kwua angeweza kupambana na uzushi huo kwa ufanisi zaidi kuliko kuiga 'ujinga' unaofanywa na hao wanaotapatapa.

Mkuu MN,

Hapa umesema yote, wakati mwingine kimya ni silaha kubwa kuliko kusema.

Mengi akae kimya na kuyaachia magazeti yake yafanye hiyo kazi ya kupambana na mafisadi.
 
Mwaka 2005, Reginald Mengi kwa imani alizokuwa nazo wakati huo, alivitumia vyombo vyake hivyo kuwapigia debe mafisadi - maybe then he was blind but now he can see. Kwa vile kathubutu kuingia kwenye uwanja wa mapambano kama wengi wetu, lazima tujiulize kama wagomvi wake ni hao hao tunaopambana nao - na kama ni hivyo hatuna budi kumuunga mkono.

Tangu 1995, 2000 vyombo vyake vya habari vimekuwa upande wa CCM sana wakati wa kampeni. Wacha ajifunze, akili imsogee. Japo namuunga mkono kila mpinga mafisadi!
 
Watu wakishaelewa kuwa haya ni mapambano ya kifikra wataelewa hata mbinu zinalenga huko huko!!
 
..kwani hajaoa na picha zipo...kamuoa lilian kimaro wa BRELA.....

kwakweli kumbe hiki ndio chanzo chake cha habari kuhusiana na makampuni hayo anayoyaandama, kumbe alikuwa akitoa rushwa ya ngono kwa bint ndani taasisi ya usajiri wa makampuni nchini?!!!
 
Mimi sidhani kama hii ishu inahusiana na ufisadi nadhani Mengi anatafuta scapegoat tuu hapa . Zile picha speak for themselves na kiasi kikubwa zimeharibu taswira yake katika jamii period. Was it a wedding ? ....that is debatable. lakini najua ya kuwa kwa mzee mwenye umri kama wake kumdate mtoto kama yule katika jamii ya kitanzania ni NO NO !
 
Back
Top Bottom