"Moto umewawakia, hawawezi kuuzima" - Mengi

"Moto umewawakia, hawawezi kuuzima" - Mengi

..........................................[snip]
My Take:
Sasa magazeti kadhaa yanaanza kushindana kuandika nani anajua uchafu wa kiongozi gani zaidi na siku si nyingi hili litafika hadi kwa Rais, na mtu mwingine yeyote ambaye ataonekana kuwa ni fair target. Somebody got to stop this or as a people we ough to be prepared to pay a huge price for the silence we maintain.

Binafsi sioni ubaya wa kufahamishwa ubaya na hata upuuzi wa Rais wangu. Baya kwangu ni kuandika habari za uongo. Habari za ukweli ziandikwe hata kama zitakuwa ni za bedroom, zikitoka nje ziandikwe.

Hakuna haja ya kuchuja habari za viongozi tu. Tukumbuke kwamba ukishapanda jukwaa unajiweka hadharani kuliko aliyeko chini.
 
Ukiona mtu anajifanya mlokole sana hasa kwenye hadhara ujue kwenye faragha ni firauni mkubwa [haya si maneno yangu bali ni msemo wa waliotutangulia]
 
Unajua unapomwita mtu mwizi lazima uwe na ushahidi,wewe tueleze kuwa ushahidi ulionao ya kwamba Mengi ni mwizi ni upi?

halafu inaonekana kuwa unachuki binafsi dhidi ya Mengi, sasa hizo chuki zako binafsi usizilete hapa jamvini toa mada watu waijadili kama ina tija na kama huna mada kaa kimya.
Mengi hajawahi kuwa mtumishi wa umma, Mengi alikuwa Managing Partner wa Lyband Coopers ambayo ndo ilikuja zaa Price House Waters Coopers! So ukisema alikuwa ni mwizi sikuelewi kwa vile tunajua kipindi chake yeye cha uongozi kwenye hii Finance and auditing firm ndo kipindi ujamaa ukafa so by any means alikuwa jikoni na kujua mambo yanavyooenda kiuchumi ukiangalia Lybard Coopers ndo walikuwa mfilisi wa makampuni mengi ya serikali. So alitumia uwerevu wake kuachana na Lybard Coopers na kuingia private sector kujaza the void space left by governmental companies!
 
Katika magazeti ya Daily News alikuwa nani vile...?
 
TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa muda mrefu sasa, magazeti yanayofadhiliwa na watuhumiwa wa ufisadi yamekuwa yakiandika mambo mengi yaliyojaa fitina na uongo dhidi yangu na familia yangu. Kwa mfano:-

• Mengi anataka kumng'oa JK 2010?
• Mengi hatari kama Hitler
• Ndoa ya Reginald Mengi na CHADEMA yabainika
• Mengi na kashfa ya ufisadi – Tume ichunguze bilioni 40 za ukimwi.
• Mengi aoa tena – harusi yafungwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Kanali Fabian Massawe

Taarifa zote hizi ni za uongo mtupu.

Kama nilivyokwishasema awali, mafisadi wanaotuhumiwa kuiba fedha za umma ambazo zingetumika kwa kujengea shule na kupiga vita maradhi na umaskini wamekuwa wanazitumia fedha hizo kwa maslahi yao binafsi kwa kujijengea majumba ya kifahari huko Dubai, Uswisi na Afrika ya Kusini, na kubwa zaidi, sasa wanazitumia kudhoofisha nguvu zinazopiga vita ufisadi.
Mafisadi hawa wameanzisha magazeti zaidi ya 15 ambayo yanasambaza fitina na uongo uliotungwa.

Nia na madhumuni ya mafisadi kutunga na kusambaza fitina na uongo ni kuufanya umma uelekeze nguvu na mawazo yao katika fitina na uongo huo na kuacha kufikiria na kuzungumzia tatizo kubwa la ufisadi.

Fitina na uongo wa mafisadi hawa ni sumu inayosambazwa ndani ya jamii na inaweza kujenga chuki, kuwagawa wananchi na kuvuruga amani. Iwapo vurugu zitatokea, basi mafisadi hao wataanza hata biashara mpya ya kuuza silaha ili Watanzania wazitumie kuuana wenyewe kwa wenyewe.

Wengi wa mafisadi wanaishi maisha machafu mno. Hadi hapo Baraza la Habari Tanzania (MCT) litakapotoa msimamo wake juu ya uandishi wa mambo ya faragha (privacy) endapo waandishi wa habari wanaoheshimu taaluma yao ya kuandika ukweli wataandika uchafu wa maisha hayo, wasilalamike.

Ninarudia tena kusema kwamba ni lazima mafisadi waelewe kwamba kutapatapa kwao ni jitihada za wafamaji kwa sababu moto wa vita dhidi yao umekwishawaka na hawawezi kuuzima au kuukwepa. Hautazimika kamwe, na jitihada zao za kudhoofisha nguvu za vita dhidi ya ufisadi zitageuka kuwa kichocheo cha moto huo hata kama watafanikiwa kuwatokomeza watu wanaopiga vita ufisadi.
____________________
Reginald A. Mengi
Mwenyekiti Mtendaji
IPP Limited
10 Februari,2009

Heko Bwana Mengi kwa haya........
"Ninarudia tena kusema kwamba ni lazima mafisadi waelewe kwamba kutapatapa kwao ni jitihada za wafamaji kwa sababu moto wa vita dhidi yao umekwishawaka na hawawezi kuuzima au kuukwepa."

Bunge halina nguvu tena.
Raisi hana nguvu tena.
Wapinzani hawana nguvu tena.

Muulizeni Mh. Chikawe!
 
kwanioi busara isitumike katika kuongea, kutenda, kushauri.hadi kufikia hatua kuhukumu pasipo na hekima. Wote nyie ni kio katika jamii. Haipendezi kujiangalia ktk ukakuta picha yako kuwa ni kiumbe tofauti nawe. Kuweni na utu.
 
Jamani hata mimi niliwahi kuziona hizo picha. Lakini mbona kama yule ni sawa na mwanae?
 
Ndugu yangu, kwa kusema upinzani hauna nguvu unakosea sana....Upinzani kwa sasa TZ ni kama moto wa Mkaa wa mti wa MGUNGA, shauri yako.
 
Jamani hata mimi niliwahi kuziona hizo picha. Lakini mbona kama yule ni sawa na mwanae?

mtafutie mke mwingine. sasa mbona jukwaa limegeuka na kuwa la udaku? Haya yapelekeni kwenye jukwaa la mahusiano.
 
Wazee naomba mnisaidie hili gazeti la Taifa letu ni la nani .....Kwani leo limeamua kumtukana matusi ya nguoni Karamagi ! Gazeti hili kwa wale wasiojua ni la Mheshimiwa Mengi ambaye alijisema kuwa anafuata kanuni za uandishi ! Huyu mtu ni mnafiki sana , ndio maana nilisema inabidi uwe smart kujua michezo anayocheza ..

Huyu mtu ni mnafiki sana ....

kwa mengi umechemka,unalipwa na mafisadi nini?au unabishana na ukweli,nyie ni wale mnaoficha taa gizani.mengi ni tajiri anaelipa kodi kihalali ingekua hafanyi biashara zake kimagumashi kama hao kina karamagi unaowasifia wala asingeachwa na serekali ya kifisadi ya sisiemu.upumbavu wako mkubwa ni wewe kumlinganisha mengi na karamagi ambae kila mtu anajua kua ni mwizi.bwe..ge tu wewe huna lolote
 
""MA'MAKE YANGA"" gazeti moja la spot. Hili liliwezekana, ndo hayo mengne!!!! Hahahahahaha... Only in Tanzania
 
Mengi aboreshe maslahi ya wafanyakazi wake.

Haina maana boss kubwa anatoa misaada ya mabilioni wakati wafanyakazi wake wanalia njaa yeye anakalia kuuza sura kwenye TV zake. Ni lini ushawahi kumuona Ted Turner anatokea CNN?
 
kwani Mengi mzungu?
 
ukitaka kumfahamu huyu mengi dai chako,pana rafiki yangu alikuwa mpambe wake kazi yake ilikuwa kupeleleza habari za manji.hili nina ushahidi nalo kwani jamaa alipeleka kwa mengi ili wakamalizane cha kusikitisha ni kuwa hakupata haki yake licha suala lao kufika hadi kwa jk.kwa kifupi mengi anataka wananchi wamwone kama anaonewa.
 
Mengi hajawahi kuwa mtumishi wa umma, Mengi alikuwa Managing Partner wa Lyband Coopers ambayo ndo ilikuja zaa Price House Waters Coopers! So ukisema alikuwa ni mwizi sikuelewi kwa vile tunajua kipindi chake yeye cha uongozi kwenye hii Finance and auditing firm ndo kipindi ujamaa ukafa so by any means alikuwa jikoni na kujua mambo yanavyooenda kiuchumi ukiangalia Lybard Coopers ndo walikuwa mfilisi wa makampuni mengi ya serikali. So alitumia uwerevu wake kuachana na Lybard Coopers na kuingia private sector kujaza the void space left by governmental companies!

Bora mkuu umeniwahi na kuweka fact hz,maana Watanzania tulivyo ni wakurukupukaji na chuki hasa kwa Watanzania wenzetu wanapojipigania na kupata mafanikio,uliyemjibu hoja inaonekana hana data zozote za Reginald na amekua hata mvivu wa ku google,ila alichokimbilia ni kuleta fitna na chuki zake dhidi ya Mengi ambazo hazitamsaidia kwa kua always ukweli uwa unabaki kua ukweli hata uchukieje!kumsaidia hata Mr Mndolwa nae alitajirikia huko huko Lyband Coopers
 
mtafutie mke mwingine. sasa mbona jukwaa limegeuka na kuwa la udaku? Haya yapelekeni kwenye jukwaa la mahusiano.

Ndio hulka tuliyo nayo Watanzania wengi tuliyo nayo mkuu,udaku na husda ndicho tunavyoweza!kujadili mambo ya msingi hatuwezi!ndio maana magazeti ya udaku yana uzika sana
 
Anatakiwa awe na ngoz ngumu sio kulalamika kila siku utafikiri haijui siasa ya tanzania..take action mkuu mengi huitaj huruma ya watanzania..japo tunatambua mchango wako kwa watanzania.
 
Katika magazeti ya Daily News alikuwa nani vile...?

Mkuu hizi taarifa zako ni za kisanii/sadikika au ni fact?from what i know ni kua Mengi aliwahi fanya kazi TPC ambayo ilikua owned na Mdanish na alifanya Coopers & Lybrand tu kabla hajaanzisha makampuni yake!hiyo ya Daily News embu tu update ilikua mwaka gani mkuu,maana wengine tunaweza kua hatuna data
 
Back
Top Bottom