Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
693
1,000
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema watuhumiwa wanatakiwa kuheshimiwa na kutendewa haki kama watu wasio na hatia mpaka itakapobainika vinginevyo.

IGP Sirro alitoa kauli hiyo jana, wakati akifunga mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN-Women) pamoja na Mtandao wa polisi wanawake ndani ya jeshi hilo yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi (TPS).

Mafunzo hayo yalienda sambamba na uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo wa namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake. “Hakuna kitu muhimu kwetu kama kusimamia sheria na kutenda haki, kuwa wanyenyekevu na kuheshimu watu. Sisi leo tumevaa majoho haya na kesho tunarudisha kwa wenyewe na wenyewe ni Watanzania ambao wanalipa kodi ambayo inatufanya tufanye kazi.

Pamoja na mambo mengine, alisema zipo jitihada za utatuzi wa changamoto mbalimbali ndani ya jeshi hilo, ikiwamo masuala ya utumishi. “Nitajitahidi katika upangaji wa nafasi za utendaji kazi kwa maofisa wanaondelea na mafunzo vyuoni wanaomaliza hivi karibuni ili madawati haya ya jinsia yaweze kupata uwakilishi kuanzia ngazi za vituo, wilaya hadi mkoa,” alisema.

Alisema kwa sasa zipo changamoto za masuala ya ugaidi, vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake ambavyo vinapaswa kushughulikiwa kikamilifu. “Natambua mtandao wa polisi wanawake ni moja ya maboresho yaliyofanywa na Jeshi la Polisi Tanzania ili kushughulikia masuala ya askari wa kike pamoja na kuzuia masuala ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, mtandao wa polisi wanawake sasa umerasimishwa kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya mwakilishi mkaazi msaidizi wa UN Women, Lucy Tesha alisema wamekuwa wakifanya kazi ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake katika ngazi ya kimataifa na kitaifa.

“Tunalishukuru Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo wanashirikiana na sisi, ambapo tangu madawati kuanzishwa mwaka 2008 mmekuwa mfano bora wa uendeshaji wa dawati la jinsia kwa weledi katika kukabiliana na matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii” alisema Lucy.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,720
2,000
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema watuhumiwa wanatakiwa kuheshimiwa na kutendewa haki kama watu wasio na hatia mpaka itakapobainika vinginevyo...
Kuwa na imani na polisi kwa sasa ni sawa na kuwa na imani na jambazi.

Ugaidi unaofanywa na jeshi la polisi wa kubambikia watu kesi, upigwe vita kila mahali. Polisi magaidi ni maadui wa kila mpenda haki. Tunataka jeshi linalofanya kazi kwa kuzingatia sheria.

Maadamu akina Kingai, Mahita, na wengine wanaofanana na hao bado wamo humo ndani, jeshi la polisi litaendelea kuwa syndicate ya majambazi yanayotumia vibaya mamlaka ya polisi kwaajili ya kutekeleza uovu wao.

Gaidi Kingai apigwe vita
Gaidi Mahita apigwe vita
Polisi wabambikiaji kesi wapigwe vita
Polisi wapenda rushwa wapigwe vita
Polisi chawa wa CCM wapigwe vita
 

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
1,451
2,000
Kila kukicha zinaibuka tuhuma dhidi ya polisi kutesa na kupiga watuhumiwa kinyume cha katiba ya JMT.

Hili ni kosa kubwa sana maana katiba ya JMT inatamka wazi kuwa chombo pekee cha kutoa haki ni mahakama, na hakuna mtu atakuwa na hatia mpaka mahakama imtie hatiani.

Achana na mtuhumiwa mwenzanke na Mbowe Mohamed Ling'wenya kutoa madai ya kuteswa na kupigwa akiwa mahabusu, ukweli ni kuwa watuhumiwa wengi huwa wanateswa hapa Tanzania.

Hii ni sababu polisi wa Tanzania wanaamini kuwa mtuhumiwa hawezi kukubali mpaka awe ameteswa au kupigwa. Lakini sheria ya ushahidi inataka mtuhumiwa akiri kwa hiari.

Kitendo cha kupiga na kutesa watuhumiwa kinyume cha sheria ni kulichafua taifa letu

Soma: Moshi: IGP Sirro ataka Watuhumiwa watendewe haki
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
35,929
2,000
AUYZ3t.jpg
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
25,069
2,000
Hilo halitakuja kwisha, labda uhalifu ukome kabisa.

Watu wanakamatwa kwa connection sio ushahidi, hawawezi kukubali kosa kwa story.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom