Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,666
- 218,154
Kama wewe ni mgeni basi ni vema ukalihifadhi onyo hili lililotolewa na uongozi wa kituo hicho
----
Uongozi wa kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Msamvu mkoani Morogoro umeanza kutoza faini ya Sh50,000 kwa mtu atakayeingia au kutoka kituoni hapo bila kuvaa barakoa na kunawa mikono.
Meneja wa kituo hicho, Gilbert Changalima amesema hayo leo jumatano Agosti 18, 2021 wakati akizungumza na Mwananchi Digital akibainisha kuwa lengo ni kuifuata miongozo ya Wizara ya Afya ya kujikinga na Uviko 19.
Changalima amesema uongozi wa kituo hicho unashirikiana na Jeshi la Polisi katika kukagua abiria ama watoa huduma katika kituo hicho kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na miongozi ya wizara.
Amesema katika kila geti la kuingilia kwenye kituo hicho cha mabasi wameweka mapipa ya lita 500 yenye maji ya dawa akibainisha kuwa sabuni zinaibwa.
“Stendi yetu ya Msamvu ina mageti manane ya kuingia na kutoka na yote tumehakikisha tumeweka pipa moja na tumeagiza katika kila ofisi za kukatia tiketi waweke ndoo zenye maji pamoja na vitakasa mikoni,” amesema.
Mbali na faini hiyo, ametaja adhabu nyingine kuwa ni kumtaka atakayebainika na kosa kuchota maji na kujaza katika pipa.
Amesema pamoja na kuweka faini hiyo bado wameendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa kutumia vipeperushi vilivyotolewa na Wizara ya Afya vinavyoelezea namna ya kujikinga na Uviko-19, matangazo kwa njia ya spika zilizopo katika stendi hiyo na kwamba wamekuwa wakitangaza zaidi ya mara 10 kwa siku.
Baadhi ya abiria waliozungumza na Mwananchi Digital wamesema kuwekwa kwa faini hiyo kutasaidia watu kuzingatia na kukumbuka wakati wote uvaaji wa barakoa na kunawa mikono pindi wanapofika katika standi hiyo.
Asumpata Leonald amesema bado kuna changamoto ya watu kutojali uvaaji wa barakoa na hata kujikinga kwa njia yoyote na kuishi kwa mazoea bila kujali afya zao.
Mliga Selemani mkazi wa manispaa ya Morogoro ameshauri Serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya kufahamu Uviko-19, chanjo na jinsi ya kujikinga kwani wananchi wengi bado hawachukui tahadhari.
Chanzo : Mwananchi