Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni jamani. Huko kuuza nyumba za serikali ilikuwa ni shinikizo la Rais na Waziri Mkuu kwa hali hiyo mnadhani Maghufuli angefanya nini?
Kwa akili za kawaida kabisa hata kama mngekuwa ninyi (mnaomlaumu Magufuli) msingejiuzia hizo nyumba?

Jamani fisadi utamjua tu Magufuli hata kama anakula rushwa sio kama wengine, hawana hata aibu, Magufuli ni mchapa kazi bwana! Utamlinganisha Magufuli na huyo aliyeshika hiyo wizara ya miundombinu, sijui ndo Kawambwa, semeni hapa amefanya kazi gani tangu ameingia ktk hiyo wizara?

Ukiangalia nyumba aliyojenga Magufuli huko mwz huwezi kucompare na za mawaziri wengine. Compare nyumba ya waziri kijana na ya Magufuli, hizo nyumba zinatizamana ila zimetenganishwa na barabara tu ukiziangalia tu lazima utajua nyumba moja ni ya fisadi.

I like Magufuli, I appriciate his work. Big Up!
 
Nami napenda kutoa hn hongera kwa Magufuli. Nakumbuka alivyokuwa anatoa data za barabara ktoka kichwani tu bila ya kufanya reference. Inaonekana huwa yupo up to date na kazi zake!! He does his homework. Ebu muulize Waziri wa sasa ni kms ngapi za barabara ambazo zipo katika mpango wa kuweka lami, na zipo wapi. I bet he doesnt have a clue.
 
Sasa kazi gani amefanya naona mnalongolongo kibao ,nawashangaa ama kweli ukipenda chongo utaliona kengeza.
 
Kuna mtu ameniuliza na mimi nalipitisha hili swali kwa wahusika kwanini wale samaki wa meli iliyokamatwa ambao wanataka kupigwa mnada ikashindikana wasinunuliwe na serikali na kupewa wahanga wa mabomu ya Mbagala. Provided kwamba wako katika hali nzuri bado kwa matumizi ya binadamu? Au wataamua kuwatupa kwa kukosa mtu wa kula?

Siwezi kushangaa maana tunaangaliaga vitu kwa vipande vipande bila kuvihusisha.
 
. Provided kwamba wako katika hali nzuri bado kwa matumizi ya binadamu? Au wataamua kuwatupa kwa kukosa mtu wa kula?


Labda wanaogopa wananchi kupeleka ferry
 
Hao watu wakigundulika hawakufanya makosa itabidi wapewe hiyo hela itakayopatikana kwenye mnada. So wakiwagawa hao samaki linaweza kuwa tatizo.
 
Huyu waziri pamoja na tuhuma zote za kipindi cha bwana Benjamini, yaani kuhusiana na barabara na uuzwaji wa nyumba za serikali. Lakini mimi nafikiri tumpongeze kwa haya:-
1. Kufanikisha kukamata samaki ambao tumekuwa tunaibiwa toka tupate uhuru
2. Kupambana na uvuaji haramu wa samaki kule Nyumba ya Mungu na sehemu nyingine.

Nimesema hivi kwa sababu binafsi naona ni kati ya mawaziri wachache wanaojitahidi kulinda maslahi ya umma kwenye wizara yoyote ile ambayo amewahi kupelekwa kufanya kazi.
 
Of course is the only serious minister.the rest wababaishaji na mafisadi
 
Kwa kweli anastahili pongezi, ila anahitaji ushauri na mchango wa mawazo: Mathalani samaki waliokamatwa kwene zoezi la kuzuia uvuvi haramu, Wizara yake inahangaika kuwapiga mnada, wemewekwa kwenye hifadhi kwa karibu miezi miwili, serkali inalipa dola 800 kwa kuhifadhi tani moja sasa ukizidisha mara 296, kuanzia tarehe 10 mwezi wa tatu 2009 mpaka leo tumepoteza pesa ya walipa kodi kiasi gani? Kwa nini hao samaki wasigaiwe kwenye shule za serikali, mahospitali, mission, kwa watoto yatima, magereza, kwenye kambi za jeshi nakadhalika.
 
Sale of seized tuna catch put off again

2009-05-06 13:39:40
By Correspondent Edwin Agola


The Kisutu Resident Magistrate`s Court in Dar es Salaam has referred to the High Court the case involving 296 tonnes of tuna recovered from a pirate foreign vessel impounded while illegally fishing in Tanzania`s Exclusive Economic Zone (EEZ) waters recently.

Sources intimated to The Guardian yesterday that the decision to refer the case was made after the lower court had officially put on hold the auctioning of the fish.

It has been reliably learnt that the exercise has been stopped because the case, which involves 30 foreign crew members, is about to be taken to the High Court for hearing and that the fish in question will serve as an exhibit.

The sources further hinted that Kisutu court had referred the case because the vessel was impounded outside Dar es Salaam Region and the lower court has no jurisdiction to preside over cases arising from incidents occurring outside the region.

The auction aborted last Saturday following a low turnout of potential buyers, with the few who turned up saying the quotation given by the government was too high for them.

The planned auction has also drawn criticism from some quarters over apparent lack of transparency and accountability.

The foreign crew members stand charged before Kisutu court principal resident magistrate Addy Lyamuya, their case scheduled for hearing on May 18.

It is understood that a Dar es Salaam-based company known as Bahari Foods Ltd, which has been storing the fish on behalf of the government at a rate of USD 800 per tonne a day since March 10, has since suspended some of its routine operations because the 296 tonnes surpass its storage capacity.

``Previously, we were told that the vessel was loaded with only 70 tonnes of tuna and we agreed to accommodate that,`` said Ramesh Chauhan, the firm`s general manager.

A Southern Africa Development Community (Sadc) joint patrol team led by South Africa seized the vessel on March 10, while it was on an illegal fishing mission in Tanzania�s EEZ. The 296-tonne load is believed to be worth 2bn/-.

The Kisutu court recently mandated Dar es Salaam-based court broker Yono Auction Mart Company to sell the fish on behalf of the government.

Following the abortion of the planned auction, it is unclear how the fish will finally be disposed of.

Tanzania benefits little from its marine resources, the fishing sector contributing a meagre 1.6 per cent to the gross domestic product, the main reason being illegal fishing by foreign trawlers.

SOURCE: Guardian
 
Huyu waziri pamoja na tuhuma zote za kipindi cha bwana Benjamini, yaani kuhusiana na barabara na uuzwaji wa nyumba za serikali. Lakini mimi nafikiri tumpongeze kwa haya:-
1. Kufanikisha kukamata samaki ambao tumekuwa tunaibiwa toka tupate uhuru
2. Kupambana na uvuaji haramu wa samaki kule Nyumba ya Mungu na sehemu nyingine.

Nimesema hivi kwa sababu binafsi naona ni kati ya mawaziri wachache wanaojitahidi kulinda maslahi ya umma kwenye wizara yoyote ile ambayo amewahi kupelekwa kufanya kazi.

Bravo Magufuli....

TUNATAMBUA NA KUITHAMINI KAZI YAKO TOKA KIPINDI KILEEEEEEE

CHA MABARABARA NA WAKANDARASI MAKANJANJA, JAPO

UNABANIWA KIAINA NA `MWENYE NCHI` WA SASA...
 
Bravo Magufuli....

TUNATAMBUA NA KUITHAMINI KAZI YAKO TOKA KIPINDI KILEEEEEEE

CHA MABARABARA NA WAKANDARASI MAKANJANJA, JAPO

UNABANIWA KIAINA NA `MWENYE NCHI` WA SASA...

hili ni kweli kabisa hata mimi nimeliona, mkuu wa nchi anajitahidi sana kumficha mshikaji. Kwa kumpeleka wizara za mafichoni. Lakini kila anapompeleka anaibuka kidedea
 
Anastahili pongezi tena kubwa sana. Hata umuhamishie kwenye wizara ya kuzibua vyoo yeye ata shine tu. Wengi walifikiri kuwa kwa kumpeleka samaki ndo wamemmaliza lakini wapi katokeza tena katufungua macho na kujua utajiri mkubwa tulionao kwenye bahari yetu. Na kizuri zaidi ni pale ambapo analazimika kufanya kazi ambazo watendaji waliopo chini yake wanapaswa kuzifanya. Na yeye ameligundua hilo na ndio maana kasema hao watendaji wasipotimiza wajibu wao wataburuzwa mahakamani. Alipotoka tu pale alipokubali kucheza ngoma ya mafisadi ya kuuza nyumba (labda walitaka kumpunguza kasi yake ya kuja kugombea urais?)

Bravo Magufuri, ila uamuzi wenu wa kuwahifadhi samaki kwa karibu miezi miwili kwa gharama ya dola 800 @ ton mara 296 tons @ day unanitia shaka! Hakukuwa na njia nyingine ya kuwapunguzia wananchi gharama za kuwahifadhi hao samaki?
 
Anastahili pongezi tena kubwa sana. Hata umuhamishie kwenye wizara ya kuzibua vyoo yeye ata shine tu. Wengi walifikiri kuwa kwa kumpeleka samaki ndo wamemmaliza lakini wapi katokeza tena katufungua macho na kujua utajiri mkubwa tulionao kwenye bahari yetu. Na kizuri zaidi ni pale ambapo analazimika kufanya kazi ambazo watendaji waliopo chini yake wanapaswa kuzifanya. Na yeye ameligundua hilo na ndio maana kasema hao watendaji wasipotimiza wajibu wao wataburuzwa mahakamani. Alipotoka tu pale alipokubali kucheza ngoma ya mafisadi ya kuuza nyumba (labda walitaka kumpunguza kasi yake ya kuja kugombea urais?)

Bravo Magufuri,
  1. ila uamuzi wenu wa kuwahifadhi samaki kwa karibu miezi miwili kwa gharama ya dola 800 @ ton mara 296 tons @ day unanitia shaka! Hakukuwa na njia nyingine ya kuwapunguzia wananchi gharama za kuwahifadhi hao samaki
?

ili inabidi aulizwe popote atakapo-onekana akikatiza ili isiwe ni sawa na kujaza gunia maji. Linahusika sana coz hizi gharama ni kubwa sana!!
 
Tuhuma za Magufuli zamng'oa kamanda wa polisi Mwanga
broken-heart.jpg
Na Daniel Mjema, Moshi
JESHI la Polisi limemuondoa mkuu wa polisi wa wilaya ya Mwanga (OCD), Evance Mwijage siku chache baada ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, John Magufuli kumweleza ofisa huyo mwandamizi kuwa anatuhumiwa kwa rushwa na wananchi.

Magufuli alimweleza waziwazi OCD huyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika wiki iliyopita kuwa wananchi wanamtuhumu kwa kupokea rushwa kutoka kwa wavuvi haramu na habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa Kamanda Mwijage sasa hayupo tena Mwanga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alithibitisha kuondolewa kwa OCD huyo akisema hilo limefanyika ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizotajwa dhidi yake kwa kuwa ni nzito.

Ng’hoboko alisema nafasi ya OCD huyo itachukuliwa na SP Ramadhan aliyekuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ingawa hakusema hatima ya polisi wa vyeo vya chini wa Mwanga ambao pia walilalamikiwa na wananchi.

Hivi karibuni katika mkutano wa hadhara, uliofanyika katika Kijiji cha Kagongo, Waziri
Magufuli alisema polisi wa Mwanga wanahusishwa sana na rushwa na kwamba ndio maana
hawakushirikishwa katika operesheni iliyoendeshwa katika bwawa hilo ya kupambana na wavuvi haramu.

Baada ya kutamka maneno hayo, Waziri Magufuli alimgeukia OCD Mwijage, aliyekuwa amekaa meza kuu na kumpasulia hadharani kuwa hata yeye wananchi wanamtuhumu na kwamba yeye (Magufuli) alipokea 'meseji' nyingi za simu zinazomtuhumu kamanda huyo wa polisi.

Waziri Magufuli alisema wananchi wamewataja waziwazi polisi wa Mwanga kuhusika na uchafu huo na aliahidi kwenda kuwashitaki kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema, kwamba wamekuwa kikwazo cha ulinzi shirikishi.

Kutokana na uzito wa tuhuma hizo, Jeshi la Polisi limeamua kumuondoa OCD Mwijega katika wilaya ya Mwanga na kumrudisha makao makuu ya mkoa wa Kilimanjaro ambako atapangiwa kazi nyingine.

Mbali na Waziri Magufuli, naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe alisema wavuvi haramu katika bwawa hilo wameunda umoja wao mithili ya vyama vya kuweka na kukopa, Saccos, ambacho alidai kinatumika kuwahonga polisi.

“Nilipokuwa Waziri wa Maliasili na Utalii nilileta boti la doria, lakini likalipuliwa
kwa baruti, kibaya zaidi hapa kuna umoja wa wavuvi haramu, wana Saccos, wanachanga pesa, wanakwenda Mwanga, wanawahonga polisi,” alisema.

Profesa Maghembe alisema polisi wa Mwanga wamekuwa wakipewa rushwa ya hadi
Sh400,000 kiasi kwamba makokoro yaliyokuwa yakikamatwa yalikuwa hayachomwi
moto na badala yake yanarudishwa kwa wavuvi haramu.

Kwa mujibu wa Profesa Maghembe, mtandao huo ndio uliolipua boti la serikali la doria na kwamba baada ya polisi kupewa hongo, wamekuwa wakifunga macho huku samaki wadogo wakisafirishwa mbele yao.

Tangu ateuliwe kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Waziri Magufuli amekuwa akipambana na uvuvi haramu unaofanyika kwenye maziwa na bahari na hivi karibuni ushirikiano baina ya Tanzania na nchi nyingine zilizo pwani ya Bahari ya Hindi ulisaidia kukamata samaki zaidi ya tani 270 aina ya tuna kwenye pwani ya Tanzania.
 
Mwaonaje mbinu hii ingetumiwa kwa Hosea,Mattaka,Masha.... etc?


Date::5/11/2009
Tuhuma za Magufuli zamng'oa kamanda wa polisi Mwanga

RPC-Ng’hoboko alisema nafasi ya OCD huyo itachukuliwa na SP Ramadhan aliyekuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ingawa hakusema hatima ya polisi wa vyeo vya chini wa Mwanga ambao pia walilalamikiwa na wananchi.

Hivi karibuni katika mkutano wa hadhara, uliofanyika katika Kijiji cha Kagongo, Waziri ........+
.

Kutokana na uzito wa tuhuma hizo, Jeshi la Polisi limeamua kumuondoa OCD Mwijega katika wilaya ya Mwanga na kumrudisha makao makuu ya mkoa wa Kilimanjaro ambako atapangiwa kazi nyingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom