Mojawapo ya masharti ya STATUS ya Lissu nchini Ubelgiji

Lissu juzi kafanya mahojiano na BBC kuhusu uchaguzi mkuu ulivyokuwa wa maigizo Tanzania, sijui ulikuwa kijiji gani hukuona, au hayo mahojiano yalitangulia masharti? au shida yako unaogopa selfie za Lissu tu? wewe kweli katuni.

Kiuhalisia hata kama anasubiri status ambayo naamini ataipata tu kulingana na situation yake halisi ilivyokuwa na ushahidi wa wazi uliopo, hiyo status ikisha kuwa approved maana yake ataendelea kuwatandika vile viboko vyake, kumbe huwa vinawauma, poleni sana.

Mleta mada ni sawa na unafurahia kupona maumivu ya kichwa wakati unaumwa malaria, sindano za Lissu bado ziko palepale ni suala la muda tu, wacheni kujiliwaza.
 
Duuh,sasa hili balaa.Na maringo yote yale !
Kumbe MATAGA ndio mnavyomtazama Lissu kwa jicho hilo, ndio maana hamkuhangaika kumpa ulinzi aliohitaji, matokeo yake ameondoka Ndugai anaanza kulia lia watanzania wasikimbie nchi, mwambie it's too late.

Tatizo la Lissu sio maringo ukweli kawazidi akili, ndio maana hoja zake hamzijibu, na huwa hawacheki kwa hilo tatizo lenu mna inferiority complex.
 
Mkuu Belgium wapo kibao toka Rwanda, Burundi, Sudan etc tena waliokuwa na vyeo vikubwa kwao mpaka ma IGP, wakuu wa majeshi etc. Ila ukiingia Kama mkimbizi una MUTE. Ukileta ujuaji unarudishwa kwenu unaambiwa kumbe wewe msumbufu ndo maana umekimbia. Bongo ndo mnamjua ni nani!?, kule Belgium hawajui hata Lissu ni mdudu gani duniani.
Ahaa kumbe ishu ni kujulikana hapa bongo na sio ubelgiji, hiyo mbona inatosha kbs...muhimu ni ajulikane hapa nyumbani huko aliko hata akitambulika kama mkimbizi inatosha kabisa!

Nawe tumikia watawala upate mkate wa watoto hy inakutosha...kila mtu ashinde mechi zake!
 
Si wameshaliona bwege fulani tena fitna kuliko hata mchawi ambaye kwake anatamani mamilioni wateseke kwa sababu kakosa.Roho mbaya.
Nchi ina shida moja kubwa na watu hawataki kuiongelea...Kuna wahamiaji haramu wengi kutoka Rwanda na Burundi (Hutu na Tutsi)toka miaka ya 1950 kundi kubwa liliingia Tanzania alafu miaka ya 70 na lingine miaka ya 90 achilia mbali mmoja mmoja kila siku...hawa watu wameingia kwenye serikali yetu ndio maana wako tayari kuuwa ili CCM ibakie madarakani..wanaogopa wakija upinzani mwisho wao utakuwa umefika...na wote wanatabia kama zako👆
 
Sasa mtu yupo ulaya,nyie huku makalio yanawasha,badala ya kupambana mjennge uchumi ambao mnaendelea kuharibu,nyie ni kumuongelea Lisu tu. Jiwe, kaiba kura, wabunge wake wote wamepita! Cha ajabu na "ushindi wote huo wa kishindo"hakuna mwenye furaha,nafasi zinawasuta,mambo hayaendi,sukari shida,mafuta shida,pesa hakuna,sasa hv TRA, inapora tu pesa za watu binafsi.
 
Lisu anapigania tumbo lake, na ndio maana yupo tayari kuuza utu ili tumbo lake lijae.
Tundu hana historia ya kusaidia nchi zaidi ya harakati zisizotumia akiri bari kichwa tupu.
So what ? Lissu tunajua alichopigania kwa maisha yake yote. Wewe je unapigania nini na mchango wako kwa nchi yetu ni upi?

I doubt if you have moral and intellectual authority to question the intelligence of Lissu.
 
Mkuu Belgium wapo kibao toka Rwanda, Burundi, Sudan etc tena waliokuwa na vyeo vikubwa kwao mpaka ma IGP, wakuu wa majeshi etc. Ila ukiingia Kama mkimbizi una MUTE. Ukileta ujuaji unarudishwa kwenu unaambiwa kumbe wewe msumbufu ndo maana umekimbia. Bongo ndo mnamjua ni nani!?, kule Belgium hawajui hata Lissu ni mdudu gani duniani.

Ni hivi, tunashukuru Lisu kwa kuondoka salama vinginevyo angeuwawa na shetani. Huko alipo yuko hai hilo kwetu ni faraja fullstop.
 
Mbona alishiriki kikao cha kamati kuu ya Chadema kilichowavua uanachama akina Halima Mdee?

Ninachojua nu kuwa Lissu ana permanent residence ya Ubelgiji kabla hata hajarudi nchini kugombea urais.

Halafu usidhani EU ni kama Congo eti wakuondolee haki yako ya kuleta mabadiriko chanya katika nchi yako kwa kufanya mambo ya kidemokrasia yasiyo Illegal. Siasa siyo Illegal Tanzania na Ulaya sasa EU itamzuiaje mtu kufanya kitu ambacho siyo Illegal?. Mleta mada umeleta mada ambayo huna uhakika nayo.

Kama angekuwa anaorganise mapinduzi hapo mada yako ingekuwa sawa, lakini tunamuona Lissu akiendelea kuwa makamu mwenyekiti wa Chadema na vikao anashiriki, na video conference kibao za kujadili mambo ya nchi na wanaharakati wengine bado anafanya sasa wewe mleta mada unaongea kitu gani?
 
Jerusalem wewe na Lissu nani ana mchango wowote nchi hii ?!. Huna lolote la faida na nchi hii , piga debe huenda ukakumbukwa.

Lissu amefanya yake na history itamkumbuka. Je wewe ?!. Sababu zinazosababisha watu wazikimbie nchi zao si za kujivunia kama taifa bali ni aibu yetu .
Wewe ulichokiona hapo ni namna alivyo na mchango ktk nji hii ama kuzuwiwa kujihusisha na siasa angali akikamisha shariti la kuitwa kimbizi la kisiasa?
 
Hizi siasa zenu hizi za kijinga ni taabu sana na kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu...

Nilichojifunza tokana na mawazo yako haya, ni kuwa wewe na wenzako mna hofu na siasa za Lissu na wafuasi wake. Nothing more, nothing less...!

By the way kwanini unatufanya sisi ni wajinga kama wewe?

Na hivi tafsiri yako ya "kufanya siasa" kwako ni ipi has a?

Je, una maana ya kuendesha maandamano na kampeni kama zile za uchaguzi uliopita?.

Then you've to admit that you are an ignorant of politics. Politics is not only about that. Politics is more than that dude..!!!

Sasa, sikiliza wewe Jerusalemu2006. Siasa ni maisha ya kila siku. Siasa ni uchumi. Siasa ni afya. Siasa ni maji. Siasa ni elimu. Siasa ni chakula. Siasa ni utawala wa na uongozi wa kila siku ktk familia, na taasisi yoyote na nchi kwa ujumla. Siasa iko mpaka kwenye dini. Kwa kifupi siasa is everything. Politics is everyday's life of all people in the globe...

For this case, kumkataza Tundu Lissu kuzungumza au kufanya moja kati ya hayo, maana yake, unamfungia ndani ya chupa au mtungi....!!!

Do you think that's possible? No way, it's impossible and the UN can never put that kind of restrictions..!!

Moja ya mambo makuu yanayolindwa na dunia kupitia UN ni uhai wa mtu na freedom ama uhuru wa watu kwa ujumla hususani wa kutoa maoni....

Kwa hiyo, the truth is that, atafanya siasa kwa kadiri apendavyo katika "STATUS" yoyote atakayokuwa nayo LAKINI si katika mtindo na style mnayodhani ataitumia...

Alisema wakati anaondoka na anasema hata sasa, kuwa, aina ya mapambano ya kisiasa atakayofanya ni ile iliyo katika level ya juu zaidi na iliyo very effective kubomoa utawala wowote wa kishetani kama huu wa kwetu chini ya CCM na Magufuli...

Tundu Lissu ni mwanasiasa. Tundu Lissu ni International Law professional. Anaweza kufanya kazi popote duniani na kuingiza kipato cha kuwalisha wewe na ukoo wako wote...

Tundu Lissu atafanya na ataendelea kufanya siasa popote na wakati wowote. Tundu Lissu is a genius human being. Tundu Lissu artificial immortal. Tundu Lissu is chosen one...!!
 
Hili chapisho halina ushahidi unaoonesha kama Lissu ameomba ukimbizi. Hio copy paste ni general info kuhusiana na wakimbizi nchini Belgium haiprove kama mtu ameomba ukimbizi.
 
Ila nimegundua Lissu ana kipaji kingine cha uigizaji. Wewe huwezi kupiga kampeni nchi nzima ukijibweda na chopa, Halafu umemaliza kampeni unakimbilia balozi za Germany 'eti' wanataka kuniua. Sasa kama ni kweli kile kichopa si wangekinasisha kwenye miti huko huko angani ..! Akirudi nashauri apelekwe ...tena kinguvu TASUBA Bagamoyoooo..! kuongeza ujuzi na cheti cha sanaa akabidhiwe.
Wewe haujielewi kwani waliompiga risasi wamepelekwa mahakaman ? Au kwa kuwa wewe hauviziwi kuondolewa uhai wako ndo unabwata ngoja yakukute ndiyo utaelewa .Tafakar kabla ujaongea.
 
Nadhani tuwe tunasoma japo kwa kugoogle itatusaidia kufungua fikra zetu, naangalia alichoweka mtoa mada Kama citation na zuio lakisiasa nakosa connection.

Tujifunze kujua nani mwomba hifadhi? Nani mkimbizi? Je, Lisu nimkimbizi? Ni muomba hifadhi?

Tukipata majibu ndipo tujadili ana haki gani na anakosa haki gani? Ila pia wakati tunajadili tutafute watu wenye sifa za akina Lissu wanapata benefits gani tofauti na Mimi na wewe?

Kinacholindwa na Dunia ni uhai wa mtu ( haki ya kuishi) na uhuru wakutoa maoni, Dunia ya leo haifungi watu fikra na mawazo yao. Ukimbizi si kifungo Cha fikra na uwezo wa mtu kutenda au kukosoa Bali Ni sifa yakukufanya uishi salama nje ya eneo ambalo uasalma wako upo hatarini.
Safi Sana mdada Ubarikiwe kwa hoja yako
 
Back
Top Bottom