MOI: Mwanaume aliyegongwa na Basi la Mwendokasi yuko ICU

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
apona.jpg

Taasisi ya tiba ya mifupa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) imesema Mwanaume aliyeonekana akigongwa na Basi la abiria “mwendokasi” Jijini Dar es salaam jana, amelazwa Hospitalini hapo kwenye chumba cha Uangalizi Maalum (ICU).

Meneja wa Kitengo cha Uhusiano cha MOI Patrick Mvungi ameiambia AyoTV kuwa Mtu huyo wamempa jina la ‘UNKNOWN’ kwa sababu mpaka sasa hawana taarifa zake rasmi.

Mvungi ameongeza kuwa mpaka sasa Mtu huyo ambaye amevunjika mguu, mkono na kuumia kichwani hawezi kuongea lakini anafungua macho.

Pia soma: Kisutu: Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road
 
Yule dereva wa Rav 4, anatakiwa apigwe marufuku kuendesha gari. Maana hana sifa ya kuitwa dereva.
Lile eneo kuna mataa pale ila baadhi ya madereva wa magari ya kawaida wanaletaga dharau sana pale.
Unakuta taa nyekundu imewaka ikimaanisha magari ya kawaida yasimame kupisha ya mwendokasi yapite, lakini ukiangalia kulia na kushoto hakuna gari la DART basi wao wanatumia nafasi hiyo kuvuka
 
Mabasi ya mwendokasi yanakimbizwa sana ajali zake uwa zinakuwa mbaya sana wakati yanapita ktk lane zilizowazi na hiyo ndio maana yake sio kukimbiza mabasi ovyo na kusababisha ajali ambazo zinaweza kuzuilika au kuleta madhara kidogo sana.
Lakini hii inayozungumziwa hapa ni kosa la mwenye land rover

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ebu elezea kidogo hapa mkuu
Gari la mwendokasi lilikuwa linapita katika njia kuu. Ila dereva wa gari ndogo alikuwa anatokea kwenye barabara ndogo.

Alitakiwa kwanza kusimama, na kuangalia pande zote mbili za barabara kuu; ndipo angekatiza. Ila yeye kaingia tu barabara kuu moja kwa moja, pasipo kuchukua tahadhari.

Dereva aliyekamilika, hawezi kufanya uzembe wa aina hiyo.
 
Mabasi ya mwendokasi yanakimbizwa sana ajali zake uwa zinakuwa mbaya sana wakati yanapita ktk lane zilizowazi na hiyo ndio maana yake sio kukimbiza mabasi ovyo na kusababisha ajali ambazo zinaweza kuzuilika au kuleta madhara kidogo sana.
Kwa pale nani mwenye kosa mkuu...? Dereva wa mwendo kasi au.. yule wa gari ndogo
 
Back
Top Bottom