Majeruhi ajali ya mwendokasi aruhusiwa kutoka hosptali

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,114
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesema majeruhi pekee wa ajali ya basi la mwendokasi iliyotokea tarehe 22/2/2023 Jijini Dar es Salaam, Osam Milanzi ameruhusiwa kutoka Hospitali baada ya afya yake kuimarika.

===
A869EC85-5646-4988-8E24-BAF117ED2032.jpeg
Tunapenda kuuarifu umma kwamba majeruhi pekee wa ajali ya basi la mwendokasi iliyotokea tarehe 22/2/2023 jijini Dar es Salaam ndugu Osam Milanzi ameruhusiwa kutoka Hospitali baada ya afya yake kuimarika.

Ndugu Milanzi alipokelewa MOI tarehe 22/2/2023 ambapo alipata huduma za kibingwa katika kitengo cha dharura (EMD), ICU, HDU na wodi 2A .

Ndugu Milanzi alipokelewa MOI akiwa ameumia maeneo ya kichwa, mguu wa kushoto, mkono na bega upande wa kulia

Ndugu Milanzi ataendelea na huduma kama mgonjwa wa nje na atarudi kliniki baada ya wiki mbili.

Aidha, Tunatoa shukran za dhati kwa watanzania wote, vyombo vya habari ambao kwa pamoja wameshirikiana nasi katika kumuombea na kumtangaza ndugu Osam Milanzi.

Imetolewa na, Patrick Mvungi Meneja uhusiano MOI

Pia soma:Aliyegongwa na mwendokasi atambuliwa na mkewe na ndugu yake
 
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesema majeruhi pekee wa ajali ya basi la mwendokasi iliyotokea tarehe 22/2/2023 Jijini Dar es Salaam, Osam Milanzi ameruhusiwa kutoka Hospitali baada ya afya yake kuimarika.

Meneja uhusiano MOI, Patrick Mvungi amesema “Milanzi alipokelewa MOI tarehe 22/2/2023 ambapo alipata huduma za kibingwa katika kitengo cha dharura (EMD), ICU, HDU na wodi 2A “

“Milanzi alipokelewa MOI akiwa ameumia maeneo ya kichwa, mguu wa kushoto, mkono na bega upande wa kulia ambapo ataendelea na huduma kama Mgonjwa wa nje na atarudi kliniki baada ya wiki mbili”

“Tunatoa shukran za dhati kwa Watanzania wote, vyombo vya habari ambao kwa pamoja wameshirikiana nasi katika kumuombea na kumtangaza Osam Milanzi”
 

Attachments

  • d7f082a0d739449dae86cd256fe7e084_338261448_214204171283375_3925332352557668815_n.jpg
    d7f082a0d739449dae86cd256fe7e084_338261448_214204171283375_3925332352557668815_n.jpg
    159.8 KB · Views: 3
Amen, Mungu mkubwa...

Huyu mtu nilimuonea huruma sana baada ya kushuhudia video zikimuonesha anavyogongwa na basi huku akiwa kapigwa pumbuwazi asijue wapi aende kujiokoa...
 
Amen, Mungu mkubwa...

Huyu mtu nilimuonea huruma sana baada ya kushuhudia video zikiomesha anavyogongwa na basi...
Hata mimi nimesikia furaha isiyo na kifani hasa nikikumbuka alivyogongwa. Maskini alikuwa anajipitia zake tena kando ya barabara kabisa.
 
Back
Top Bottom