Mohamed Said acha upotoshaji wa makusudi

Mohamed Said acha upotoshaji wa makusudi

Na Ndio Maana Huyo Tapeli Akapata Namna Ya Kumpenya
Nchi Kavu,
Soma tena habari za Jamal Yassin ili umuelewe.
Jamal kabla ya kufika kwangu alikwishaonana na
Mufti wa BAKWATA Sheikh Abubakar Zubeir na
akapewa barua ya kumtambulisha kwa Waislam:

DSCN0381.JPG
 
Huyu mzee ni mdini na mchonganishi mkubwa anapenda sana kutunga story za uongo..bla bla za mfumo kristo na upuuzi mwingine kama huo..taratibu ameanza kuumbuka
Leonard Robert,
Yuko mtu katika kunitetea akasema kuwa ikiwa mimi natunga
niandikayo basi mie ni zaidi ya Irving Wallace.

Ikiwa unamfahamu Irving Wallace utajua uzito wa maneno yale.
Aliesema maneno haya ni profesa wa African History Marekani.

Katika mjadala ukiingiza maneno ya matusi kama ''upuuzi,'' unatoa
ladha ya majadiliano kwani ni tabu mtu kujibu tusi.

Ikiwa una hoja ilete tu kwa heshima na adabu ijadiliwe.
Huu ndiyo uungwana.
 
Mohamed Said mada zake nyingi zimejaa mihemko ya Udini.Nilishawahi kumwambia hili siku nyingi wakati anajadili kuhusu Wazee wake wa kariakoo na Uhuru wa Tanganyika bila kumsahau Padre wake Sivallon.Huyu mzee ni mpotoshaji na inabidi aanzishe uzi humu wa kutuomba radhi wakati tunaendelea na taratibu za kumuumbua kuhusu hadithi zake nyingine alizokuwa akidanganya watu.Mimi naamini Mungu huwa hamfichi Mnafiki.
Farudume,
Umekuwa mwepesi mno wa kukata hukumu bila ya kupokea ushahidi.
Hakuna mihemko ya dini katika niandikayo ila kazi za kitafiti.

Padri Sivalon si padri wangu.
Sivalon ni Padri wa Kanisa Katoliki.

Wala mimi si mpotoshaji.
Angalia ni watu gani wamechapa kazi zangu.

Nimechapwa na Oxford University Press Nairobi
na New York kukutajia wachache.

Nimehadhiri University of Iowa, Northwestern,
Ibadan, Johannesburg, Berlin na kwengine kwingi
kwa mwaliko maalum.

Wala sijapata kuandika uongo kwani sina sababu
ya kufanya hivyo wakati ukweli naujua.

Maandishi yangu yamepewa reviews kwenye majarida
ya kutajika Ulaya na Marekani.
 
Lakini Mohamed Said amekiri kwamba amedanganywa na jamal yasin na sheikh mbaruk , mi nafkiri mwenye makosa ni huyo ambaye amemdanganya mwandishi,Kwa jinsi uongo ulivyotungwa ilikuwa rahisi kwa mwandishi yoyote kudanganywa

Kwanini asithibitishe? Alikuwa na haraka gani kuandika na kwa faida ya nani?
Hivi ikitokea akazusha taharuki ktk jamii anaweza akasema kwa urahisi tu kuwa "nilidanganywa".
 
Kwanini asithibitishe? Alikuwa na haraka gani kuandika na kwa faida ya nani?
Hivi ikitokea akazusha taharuki ktk jamii anaweza akasema kwa urahisi tu kuwa "nilidanganywa".
OK, Mtu aliyemthibitishia ni sheikh mbaruk aliyempeleka tapeli(jamal) kwa mzee Mohamed said, kumbuka watu wakija kwako kwa gia ya kidini ni rahisi kuwaamini
 
Basi hizo tabia za wamanyema wa mtambani uziache, post zako sometimes zinawa-radicalize waumini na kuwa jihad fanatics
Bowlibo,
Sina sababu ya kuwakwepa Wamanyema wa Mtambani au kwengineko kule.
Wamanyema wamefanya makubwa katika historia ya ukombozi wa Tanganyika.

Mwaka wa 1933 wakati African Association ilipokuwa chini wa uongozi wa Kleist
Sykes
kama katibu na Mzee bin Sudi (Mmanyema) kama rais ndipo walipounda
Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Hii Al Jamitul Islamiyya ndiyo iliyotoa viongozi wa kwanza katika TANU 1955 kama
Idd Faiz Mafongo (Mmanyema) aliyekuwa mweka hazina wa TANU na ndiye
aliyeaminiwa kukusanya fedha za safari ya Mwalimu Nyerere UNO 1955.

Hii Al Jamiatul Islamiyya ndiyo iliyomtoa Idd Tosiri (Mmanyema) ambae yeye na
Idd Faiz Mafongo ndiyo waliompeleka Mwalimu Nyerere kwa Sheikh Mohamed
Ramia
(Mmanyema) Bagamoyo kumjulisha.

Ndugu wawili Abdallah na Maulid Kivuruga (Wamanyema) ndiyo waliokuwa waasisi wa
TANU Tabora, 1955 pamoja na Bilal Rehani Waikela (Mmanyema).

Hawa biti Maftah, Dharura biti Abdulrahman na akina mama wengi mstari wa mbele
kupambana na ukoloni walikuwa wanawake wa Kimanyema.

Saadan Abdul Kandoro mmoja wa waasisi wa TANU 1954 ni Mmanyema.
Katika historia ya uhuru wa Tanganyika Wamanyema wamejaa wengi.

Jiulize kwa nini iwe Wamanyema.

Sasa tuje suala la ''radicalisation.''
Ningependa unifahamishe nini ubaya wa watu kuwa ''radical.''

Hilo la ''fanaticism'' ukweli ni kuwa inategemea umesimama upande upi.
 
OK, Mtu aliyemthibitishia ni sheikh mbaruk aliyempeleka tapeli(jamal) kwa mzee Mohamed said, kumbuka watu wakija kwako kwa gia ya kidini ni rahisi kuwaamini
Tracy Martins,
Jamal
alikuja kwangu na barua kutoka kwa Mufti wa BAKWATA Sheikh
Abubakar Zubeir
ikimtambulisha.

DSCN0381.JPG
 
Kwanini asithibitishe? Alikuwa na haraka gani kuandika na kwa faida ya nani?
Hivi ikitokea akazusha taharuki ktk jamii anaweza akasema kwa urahisi tu kuwa "nilidanganywa".
Kapiki,
Ulitaka nimthibitishe Mufti wa BAKWATA?
Angalia barua ya Mufti Abubakar Zubeir:

DSCN0381.JPG
 
Mzee Mohamed said, Assalaaam aleykum, Heshima kwako.

Pole na huo mkasa, nakupongeza umeonyesha uungwana kwa kutusahihishia hio habari.

wasomaji wanaopita humu wanakuelewa kwani ni wasomi na akili zinawatosha.

kuna baadhi ya watu humu wanatoa HATE SPEECH na kujaribu kulink hili tukio na kazi zako za kiuandishi ili kujaribu tu kuonyesha kazi zako zilizopita hazina AUTHENTICITY.

Kuna tofauti kati ya HATE na CRITICISM. Tumeshuhudia humu unapoweka kazi zako baadhi ya watu huzitolea hate speech, leo wamegeuka na kuonyesha huwa wanaziamini (after critical argument) na sasa wanatumia mkasa wa huyu anti christ Jamal kuhoji kazi zako zanyuma,huu ni Unafiki wa hali ya juu, kwani hawakuwahi kuamini kazi zako (after critical argument).Me nawaambia POPO HADONDOSHI MANYOYA.

on the other side Mzee Mohamed said angeamua akae kimya tungejulia wapi ?Wadanganyika huwa tunapotoshwa mambo mengi sana, je huwa kuna anaetusahihisha? mfano mwaka jana tumekaa gizani kwa mgao mkali wa umeme zaidi ya miezi mitatu, mliona drama tulivyokua tunadanganywa na viongozi kwa kauli zao, kuna aliyesahihisha kauli yake, je tumeshahoji legitimacy yao kundelea kua watumishi wa umma? let us be critical, tusirukie mambo kwa emotions za hate.

Ni matumaini yangu Mzee mohamed said utachukua ushauri uliotolewa humu, Ahsante.
Polite,
Ahsante sana.
 
je mzee MS wewe kama nguli katika machapisho nadhani utakuwa umefahamu ni kwa kiasi gani utakuwa umeipa taharuki jamii kwa habari yako kuhusu huyo tapeli

sasa je unawasaidiaje wale uliowapa mtikisiko wa kiakili kwa kuiamani habari yako

pia utalisafishaje jeshi la polisi machoni mwa raia wema waliochukizwa na jeshi la polisi kwa habari ya huyo tapeli
 
Rubawa,
Hilo la kuwa na kazi iliyo na makosa wala si jambo la mtu kulikataa.
Kazi yoyote ile ya mikono ya binadamu haiwezi kukamilika.

Ndiyo maana hapa tupo tunajadiliana.

Ikiwa Asigwa ameona kosa katika kazi yangu yoyote ni haki yake
kunisahihisha.

Nilipopata taarifa kuwa Jamal Yassin ni tapeli haraka sana nimefuatilia
habari zake na nikafanya masahihisho na kuwataka radhi wasomaji wangu.
Hili la kukiri ulidanganywa na kuomba radhi ni jambo jema haya mengine katika uzi huu nadhani yanakuwa nje ya mada.
 
Ndug kama huna taaluma ya uandish wa habari ni bora ukaachana kabisa na hyo kazi. Unajua makala zako watu wameziamin kias gani? Na ni kiasi gani waisilam wabeba chuki dhidi ya wakirsto waliposom makala zako? Nyie mnaojiita blogger naanza kuona ni kwa Musi anawanyonga.
Ebu ona hayo umeyakanusha na kukiri kuwa umetapeliwa lakin bado hapo hum mtu aoni anabaki kikubari maandko yako ya awali..
Nguvu ulizotumia kuyaandika maandiko Yale ya uchochezi zitumike mara kumi zaidi kuyakanusha ikiwezekana pita hata huko miskitin ukikanusha
Kwani ile story ya jamal ya kutunga si ilitokea wakati wa awamu ya nne (jk) ambapo kiongozi mkuu wa nchi alikuwa muislam
 
Mkuu haya unayoyaandika hpa ni yale yaliyomo kwenye mfululizo wa makala zake ambazo wewe unaziona kuwa "zimekutoa katika giza la ujinga(kutokujua)".

Kama ameweza kupotosha kwenye uzi wake huo, iweje nyuzi nzyingine zisiwe na upotoshaji??

Vipi kama upotoshaji huo ni wa kupanga na wa makusudi??
Sema sehemu gani ya makala zake za nyuma ambapo amekupotosha, yaani unataka kuniambia ukikosea leo basi siku zote utakosea ? mbona argument yako haina logic
 
Back
Top Bottom