Bazazi
JF-Expert Member
- Aug 18, 2008
- 2,806
- 3,524
Mohamed SaidBazazi,
Ijumaa ndiyo siku Waislam tunapokutana katika misikiti yetu na kupeana taarifa
za juma zima.
Kuhusu Mfumokristo msome J Van Bergen (1981) na John Sivalon (1992)
hawa ndiyo watu wa kwanza kueleza habari hizo.
Baada ya vitabu hivyo ndipo mimi nikaja na kitabu cha Abdul Sykes (1998)
kwa lengo maalum la kuokoa historia ya Waislam katika kupigania uhuru.
Baada ya hapo ndipo nikaandika mswada ''Christian Hegemony and the Rise of
Muslim Militancy,'' (bado kuchapwa).
Sasa kama kuna suala la ushabiki ingefaa tuanze na Bergen na Sivalon.
Utetezi wako hauna mashiko kabisa hasa kwa mtu kaka wewe uliye mweledi ktk uandishi. Kuletwa na Sheikh anayeaminika, kuwa na barua ya Mufti, kuandikwa na gazeti hakukuondolei ufahamu wako. Kinachokuondolea ufahamu ni Uislamu wako kwani anayeeleza kutendwa na polisi wa "mfumo kristo" ni Muislamu mwenzako.
Waandishi na vitabu ulivyotaja wala sio hoja kwangu kabisa. Ukiwa mwanazuoni huru huwezi tegemea tu maandishi ya watu wengine lazima ufikiri ukiwa peke yako. Kikubwa kinachokusumbua ni Udini wa kudhani waislamu wanaonewa na kupuuzwa.
Unasema ugaidi ni hoja yenye utata; Labda kweli. Ila ninachojua na kuamini ni kuwa kuna waislamu magaidi na wengi ni kutoka madhehebu madogo ndani ya madhehebu makubwa ya Sunni. Madhehebu hayo yana majina mengi kutokana na maeneo. Tanzania yanaitwa Answar Sunna lakini Uarabuni ni Salafi au Wahabi lakini mikoa ya kusini huitwa Chimumuna. Inajulikana lengo kuu ni kusimika utawala wa Kiislamu Tanzania. Na kwa jinsi unavyotetea hoja zenye utata nahisi nawe ni mmoja wapo wa Waislamu hao. Unachojaribu kufanya ni kuwaonesha Waislamu jinsi wanavyopuuzwa na serikali ya "mfumo Kristo" hivyo kushawishika kirahisi wakielezwa kuwa wajiunge ktk uasi na kupigana Jihad kwa ajili ya kuitetea dini. Ukwel ni kuwa hakuna dini pale badi siasa kupitia upenyo wa dini.
Mzee! Ktk taratibu za asili, tunategemea uanze wewe kuondoka duniani. Ninaomba uende zako kwa amani lakini tuachie Tanzania yetu isiyo na makovu ya damu kisa dini. Ulishindwa kurekebisha ukiwa kijana kwa "kula starehe" unataka kutuharibia ujana wetu kwa woga wako? Hapana hiyo haikubaliki mzee.